Abiria wa wakishushwa kupitia madirishani baada ya  Basi la Dar Express lililokuwa linatoka Arusha na Basi la Simba mtoto lililokuwa linaenda Tanga kugongana uso kwa uso maeneo ya Wami kiasi cha masaa mawili hivi yaliyopita. Mwanahabari wa Globu ya Jamii aliyekuwa eneo la tukio muda mfupi baada ya ajali kutokea anasema hadi anaondoka mahali hapo hakuna maafa yaliyoropotiwa ila watu kadhaa wamejeruhiwa na kuna mtu mmoja amebanwa katikati ya mabasi ambayo kisa cha kugongana kwake bado hakijafahamika.
 Uso kwa uso
 Abiria wakijaribu bila mafanikio kumuokoa mwenzao aliyenaswa
 Mmoja wa majeruhi
 Mama akiwa anaugulia pembeni mwa barabara
Abiria wakiendelea na juhudi za kuwatoa wenzao kutoka katika mabasi hayo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 24, 2012

    Simba Mtoto haipo kwenye upande wake wa barabara

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 24, 2012

    Ajali hupangwa na Mungu:

    Lakini sasa imekuwa kama vile Tanzania pekee ndio trunaomiliki vyombo vya usafiri kama MELI na MABASI huku wengine nchi zingine wakiwa wapo katika zama za Ujima wakitumia Usafiri wa punda!

    1.Baharini hakuezekani ndio kama yale ya MV.SPICE ISLAND na MV.SKAGIT !

    2.Aridhini katika barabara MABODA BODA na MABASI !

    Imebaki tusafiri kwa miguu sasa !

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 24, 2012

    jamani hawa madereva watamaliza uhai wa watu hapo kuna dereva mwenye kosa inakuwaje wakutane uso kwa uso lazima dereva mmoja alikuwa anaovertake i hope serikali ianze kuwaweka jela miaka mingi hawa madereva wanaosababisha ajali

    ReplyDelete
  4. Hivi bongo tunaelekea wapi?yaani hakuna siku inayopita bila kusikia ajali,tena ya vyombo vikubwa vya abiria wengi!! inawezekanaje mabasi makubwa kama haya yagongane uso kwa uso tena mchana, ktk barabara iliyo nyooka?mbona zamani wakati barabara zilipokua mbovu enzi za KAMATA hakukua na matukio ya mfululizo kama sasa?waajiri hivi nikweli madereva mnaowapa kazi nikweli madereva au mambo tu yakujuana?nchi inatia aibu sana kwakushindwa kusimamia kwaujumla tatizo hili ambalo kwasasa linatishia sasa unapopanga safari unakua hauna uhakika wa kurudi.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 24, 2012

    ushirikina sana wa bongo . wanatoa sadaka

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 24, 2012

    ....HACHA KUJIDANGANYA WEWE, AJALI HATA SIKU MOJA HAIPANGWI NA MUNGU, NI UZEMBE WA BINADAMU!!!!!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 24, 2012

    Kukishakuwa na complaints ya kimifumo katika jamii haya ni mambo ya kawaida kabisa na ndo characteristics.researchers inabidi wafanye kazi.hatuna haja ya kulalamika.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 24, 2012

    Hivi serikali haipo,nyang'anya leseni kwa dereva yeyote mzembe au heft ban ya muda mrefu,na lazima wa re-take driving lessons, malipo yake yawe mara tatu au nne perhaps they will think again, they are ruin some others people lives man.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 24, 2012

    Kama kweli Dar expr. alikuwa akitoka Arusha kwenda Dar basi ndiye mwenye makosa. Nijuavyo mimi bongo tunapita kushoto, Dar Expr. anaonekana yuko kulia, tena kama driver alikuwa akijaribu kujiokoa kwa kwenda even far left akagongesha upande wa kushoto kwake! Any ways...Nionavyo mimi! Bado bongo tuna changamoto kubwa ya kubadilika!!!

    Eddy
    Van.
    Mdau mkubwa wa Dar Express

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 24, 2012

    unahitaji picha moja inayoonyesha mapana zaidi ili uweze kuamua!!

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 24, 2012

    SI walisema wanatoa leseni mpya kwa madereva baada ya mafunzo kama suluhisho la hajari.

    Mimi nilipinga nikasema dawa ni kuwa na sheria kali including kifungo hata cha miaka ishirini kama nchi za wenzetu (mfano Japan ukigonga ukaua unaozea jela) hakuna short cut. WEKA SHERIA KALI WATU WATAACHA UPUMBAFU. Ajali zote ni careless overtaking.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 24, 2012

    Ubaya huko hamna cha fidia ungekuwa hapa ajali kama hiyo mahela unalipwa kibao

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 25, 2012

    ILE SHERIA YA KUWEKA MILANGO YA DHARURA IMEISHIA WAPI?

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 25, 2012

    Kwa kutafsiri picha inaonekana dereva wa simba mtoto sio anayeendesha kila siku kwani yeye kangangania upande wake. Inavyosomeka madereva wa magari haya wakikutana husalimiana kwa kubadilishana site. ( wa kulia kwenda kushoto na kushoto kulia)Sasa dereva huyu mgeni wa simba mtoto ujinga huo haujui. Hayo ni mawazo yangu kwani ilishatokea hivyo na madereva wakafariki konda akatoa maelezo kwamba dereva hakuwa yule dereva mwenzie aliemtegemea. Ujinga mkubwa sana.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 25, 2012

    Uso kwa uso si wangegongana upande wa dreva?

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 25, 2012

    mtoa maoni wa kwanza kama ni dereva, basi uendeshaji wake utakuwa kama wa dereva wa Dar Express wa basi hilo lililopata ajali maana hajui hata upande gani tunaendesha Tanzania, halafu amekuwa kimbelembele kutoa maamuzi mabovu kwa uhakika kabisa! kama ameanza kupata busara na aombe msamaha.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 25, 2012

    Ukiangalia vizuri hii ajali utagundua kuwa madereva ni washenzi sana, unaona walivyompelekea upande wa konda tu wakati wakipishana huwa ni dereva kwa dereva ndo wanaonana....hii noma

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...