Abiria wa wakishushwa kupitia madirishani baada ya Basi la Dar Express lililokuwa linatoka Arusha na Basi la Simba mtoto lililokuwa linaenda Tanga kugongana uso kwa uso maeneo ya Wami kiasi cha masaa mawili hivi yaliyopita. Mwanahabari wa Globu ya Jamii aliyekuwa eneo la tukio muda mfupi baada ya ajali kutokea anasema hadi anaondoka mahali hapo hakuna maafa yaliyoropotiwa ila watu kadhaa wamejeruhiwa na kuna mtu mmoja amebanwa katikati ya mabasi ambayo kisa cha kugongana kwake bado hakijafahamika.
Uso kwa uso
Abiria wakijaribu bila mafanikio kumuokoa mwenzao aliyenaswa
Mmoja wa majeruhi
Mama akiwa anaugulia pembeni mwa barabara
Abiria wakiendelea na juhudi za kuwatoa wenzao kutoka katika mabasi hayo
Simba Mtoto haipo kwenye upande wake wa barabara
ReplyDeleteAjali hupangwa na Mungu:
ReplyDeleteLakini sasa imekuwa kama vile Tanzania pekee ndio trunaomiliki vyombo vya usafiri kama MELI na MABASI huku wengine nchi zingine wakiwa wapo katika zama za Ujima wakitumia Usafiri wa punda!
1.Baharini hakuezekani ndio kama yale ya MV.SPICE ISLAND na MV.SKAGIT !
2.Aridhini katika barabara MABODA BODA na MABASI !
Imebaki tusafiri kwa miguu sasa !
jamani hawa madereva watamaliza uhai wa watu hapo kuna dereva mwenye kosa inakuwaje wakutane uso kwa uso lazima dereva mmoja alikuwa anaovertake i hope serikali ianze kuwaweka jela miaka mingi hawa madereva wanaosababisha ajali
ReplyDeleteHivi bongo tunaelekea wapi?yaani hakuna siku inayopita bila kusikia ajali,tena ya vyombo vikubwa vya abiria wengi!! inawezekanaje mabasi makubwa kama haya yagongane uso kwa uso tena mchana, ktk barabara iliyo nyooka?mbona zamani wakati barabara zilipokua mbovu enzi za KAMATA hakukua na matukio ya mfululizo kama sasa?waajiri hivi nikweli madereva mnaowapa kazi nikweli madereva au mambo tu yakujuana?nchi inatia aibu sana kwakushindwa kusimamia kwaujumla tatizo hili ambalo kwasasa linatishia sasa unapopanga safari unakua hauna uhakika wa kurudi.
ReplyDeleteushirikina sana wa bongo . wanatoa sadaka
ReplyDelete....HACHA KUJIDANGANYA WEWE, AJALI HATA SIKU MOJA HAIPANGWI NA MUNGU, NI UZEMBE WA BINADAMU!!!!!
ReplyDeleteKukishakuwa na complaints ya kimifumo katika jamii haya ni mambo ya kawaida kabisa na ndo characteristics.researchers inabidi wafanye kazi.hatuna haja ya kulalamika.
ReplyDeleteHivi serikali haipo,nyang'anya leseni kwa dereva yeyote mzembe au heft ban ya muda mrefu,na lazima wa re-take driving lessons, malipo yake yawe mara tatu au nne perhaps they will think again, they are ruin some others people lives man.
ReplyDeleteKama kweli Dar expr. alikuwa akitoka Arusha kwenda Dar basi ndiye mwenye makosa. Nijuavyo mimi bongo tunapita kushoto, Dar Expr. anaonekana yuko kulia, tena kama driver alikuwa akijaribu kujiokoa kwa kwenda even far left akagongesha upande wa kushoto kwake! Any ways...Nionavyo mimi! Bado bongo tuna changamoto kubwa ya kubadilika!!!
ReplyDeleteEddy
Van.
Mdau mkubwa wa Dar Express
unahitaji picha moja inayoonyesha mapana zaidi ili uweze kuamua!!
ReplyDeleteSI walisema wanatoa leseni mpya kwa madereva baada ya mafunzo kama suluhisho la hajari.
ReplyDeleteMimi nilipinga nikasema dawa ni kuwa na sheria kali including kifungo hata cha miaka ishirini kama nchi za wenzetu (mfano Japan ukigonga ukaua unaozea jela) hakuna short cut. WEKA SHERIA KALI WATU WATAACHA UPUMBAFU. Ajali zote ni careless overtaking.
Ubaya huko hamna cha fidia ungekuwa hapa ajali kama hiyo mahela unalipwa kibao
ReplyDeleteILE SHERIA YA KUWEKA MILANGO YA DHARURA IMEISHIA WAPI?
ReplyDeleteKwa kutafsiri picha inaonekana dereva wa simba mtoto sio anayeendesha kila siku kwani yeye kangangania upande wake. Inavyosomeka madereva wa magari haya wakikutana husalimiana kwa kubadilishana site. ( wa kulia kwenda kushoto na kushoto kulia)Sasa dereva huyu mgeni wa simba mtoto ujinga huo haujui. Hayo ni mawazo yangu kwani ilishatokea hivyo na madereva wakafariki konda akatoa maelezo kwamba dereva hakuwa yule dereva mwenzie aliemtegemea. Ujinga mkubwa sana.
ReplyDeleteUso kwa uso si wangegongana upande wa dreva?
ReplyDeletemtoa maoni wa kwanza kama ni dereva, basi uendeshaji wake utakuwa kama wa dereva wa Dar Express wa basi hilo lililopata ajali maana hajui hata upande gani tunaendesha Tanzania, halafu amekuwa kimbelembele kutoa maamuzi mabovu kwa uhakika kabisa! kama ameanza kupata busara na aombe msamaha.
ReplyDeleteUkiangalia vizuri hii ajali utagundua kuwa madereva ni washenzi sana, unaona walivyompelekea upande wa konda tu wakati wakipishana huwa ni dereva kwa dereva ndo wanaonana....hii noma
ReplyDelete