Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam leo ilifurika umati wa watu waliofika kufuatilia kesi inayomkabili Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk. Namala Mkopi (pichani).
Dk. Mkopi amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam ambapo alisomewa mashitaka mawili.
Mashitaka hayo ni kukiuka amri halali iliyotolewa na Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Kazi iliyomtaka yeye na wanachama wake kutoshiriki au kujihusisha na mgomo wa madaktari na kuhamasisha mgomo kinyume na amri hiyo.
Dk. Mkopi alisomewa mashitaka hayo leo na Wakili wa Serikali Mwandamizi Tumaini Kweka akisaidiana na Wakili wa Serikali Ladislaus Komanya,mbele ya Hakimu Mkazi Faisal Kahamba.
Wakili Kweka akisoma mashitaka alidai kati ya Juni 26 na 28, mwaka huu, Dar es Salaam, mshitakiwa akiwa Rais wa MAT hakutii amri halali ilitolewa na Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Kazi ambayo ilimtaka atoe tangazo kwa kupitia vyombo vya habari kwa wanachama wake kutoshiriki au kujihusisha na mgomo.
Amri ambayo ilitolewa na mahakama Juni 22, mwaka huu.
Shitaka la pili, Dk. Mkopi anadaiwa Juni 27, mwaka huu, Dar es Salaam, waliwashawishi wanachama wa chama cha MAT Tanzania Bara kushiriki mgomo ikiwa ni kinyume na amri iliyotolewa na Mahakama ya Kazi, Juni 22, mwaka huu.
Dk. Mkopi alikana mashitaka hayo, ambapo upande wa mashitaka ulidai upelelezi haujakamilika.
Mawakili wa Dk. Mkopi Isaya Matambo, Dk. Maurid Kikondo, Dk. Gaston Kenedy na Dk. Rugemeleza Nshala waliomba mteja wao apatiwe dhamana kwa kuwa mashitaka yanayomkabili yanadhaminika.
Hakimu Kahamba alitoa masharti ya dhamana ambayo mshitakiwa awe na wadhamini wawili waajiriwa wa serikali au kutoka taasisi inayotambulika kila mmoja atatia saini dhamana ya sh. 500,000.
Wakili wa Serikali aliiomba mahakama izingatie kifungu cha 148(6) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA), kinachoelekeza masharti ya nyongeza wakati wa kutoa dhamana ambayo ni mshitakiwa kuwasilisha polisi hati za kusafiria na kutotoka nje ya mkoa husika bila ya kibali cha mahakama.
kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 6, mwaka huu, kesi itakapotajwa kutokana na kutimiza masharti hayo Dk huyo yuko nje kwa dhamana.
God bless you Dr. Mkopi and your fellow doctors!!
ReplyDeleteEtienne
Poleni Watz, hivyo watu wakidai haki zao wanashitakiwa, myself i think mtawasababisha wagome tena na ndugu zetu wanapokufa serikali haitakuwepo kutusaidia kulia, maana wagonjwa wa vigogo wote wanapelekwa nje ya nchi kutibiwa. Government u should give them what they want!!!!, angalieni wafanyakazi wa benki kuu, na wengine wanavyopewa hadi maziwa ya kuwapelekea watoto wao wakati hawanusi mavi,mkojo,damu,usahau or hawana risk kubwa kama wafanyakazi wa afya!!!!
ReplyDeleteThat is not the only solution to tackle their concerns. Something should be done by the government by having a dialogue on how to solve all their concerns. This action on suing their president will act like a catalyst of making them more and more demoralized.
ReplyDeleteIs this the start of the Tanzanian Revolution?
ReplyDeleteJAMANI MGOMO SI TUMEAMBIWA UMEISHA! SASA HII KESI YA NINI TENA?
ReplyDeletekuto poteza hela za walipa kodi mnaweza kumuua na huyo ili shuguli za kujenga uchumi ziendelee, tumechoshwa na hawa wapuuzi njaa zao wanataka kutuletea tz nzima bana
ReplyDeleteacha upumbavu angekua ni mama yako ungesema hivyo
ReplyDeleteNingefurahi kusikia kutoka kwa wataalam wa sheria kama mahakama ilitenda haki kwa kutoa amri ile, na kama ilizingatia sheria pia ama ilitumia ubabe. Baada ya kuelimishwa hilo nitatoa comment yangu.
ReplyDeleteHii ndo safi sana, siyo ile ya kuwapiga au kuwaua hapana, ukisha kataza kitu sasa subiri anayekuwa m'bishi ndo huyo unampandisha kizimbani na wala siyo kumpiga au kumuua hapana.
ReplyDeleteNa huu ndo ukomavu wa akili.
Mgomo umeisha..kesi za nini?
ReplyDeleteDavid V
Sijui kama Dr. Mkopi ana uwezo wa kuwazuia madaktari kugoma pia baada ya amri ya mahakama kutolewa, alisikika Dr mmoja mwanamke kiongozi wa madaktari bingwa akisema kwamba madaktari bingwa nao wanagoma sasa huyo ambaye ametoa tamko baada ya amri ya mahakama itakuwaje? mimi nadhani njia pekee ni kukaa na madaktari na kukubaliana yanayowezekana njia hizi nyingine zote ni kukosa busara na kuongeza matatizo.
ReplyDeleteMahakama ni mahakama bwana ndio utawala wa kisheria. Watanzania hata mkikamatwa mmemgonga mtu mnataka kutoa fedha yaishe. Kudharau kauli ya mahakama ni kosa la jinai. Someni humu mtandaoni. Watanzania ni wajinga. Bora umpige kiatu raisi utasamehewa kuliko kupinga hukumu ya mahakama kuu. Katiba isomeshwe tokea darasa la kwanza watu wajue mipaka ya vitendo vyao. Ushenzi sio kabila ila matendo ya watu. Watanzania wengi wamesoma lakini hawajaelimika, hasa madaktari.
ReplyDeleteNyinyi mnaowapendelea hamjaugua mkalazwa Muhimbili halafu daktari akakuacha bila kukutibu bila ya kumlipa chochote. Mimi yamenikuta, sina hamu nao kabisa, ni wauwaji.
Hata wakipewa vifaa, mamilioni ya fedha za mshahara ndio watadai zaidi kwa wagonjwa wakiambiwa kwamba vifaa vinavyotumika ni vya kitaalamu sana. Pesa ilimtosheleza nani, tajiri kila siku anataka zaidi. Pale Moi unalipa fedha nyingi, Daktari anakaa siku mbili hakupita, yuko kwenye hospitali yake binafsi.
ReplyDeleteWewe Etienne wacha unafiki. Wewe unadhani kule kwenu Rwanda hawa madaktari wangelithubutu kugoma? God will never bless killers! God will punish severely all murderers!
ReplyDeleteHivi kwa wale maenda hospitali huyo ni daktari wa hospitali gani? mbona wale madaktari ninaowajua wa Ilala, Temeke , Amana na Muhimbili ninaopishana nao wakichacharika na kazi huyu siwahi kumwona. Watu kama hawa wala siwafanyakazi wazuri kutwa wanatafuta maslahi yao zaidi kuliko umoja wa kitaifa na kudai haki kwa amani. Wanavyokufa watu kwa mgomo anafurahia sijui hana ndugu hapa tz? NIDA harakisha vitambulisho vya uraia ili tujuane.
ReplyDeleteduniani kitu wema, wema haujaonekana,
ReplyDeleteyamebakia mateso, waafrika (wanyonge) ndio wauwawa,
ni mashaka yaanza hivyo, wema hawana maisha.
By the late Patrick Balisidya
HIVI HUYU NI DAKTARI KWELI, AU NI WALE WANAOTAFUTA MASLAHI BINAFSI UKITAZAMA HATA SURA YAKE KAMA KIBAKA TU, HANA WITO WOWOTE HUYU NI KATI YA WALE WALIOKUWA VINARA WA MIGOMO UDSM, SASA BADO WANAWAVURUGA WALE WENYE WITO WAO. SIJAWAHI KUMUONA SIJUI ANAFANYIA HOSPITALI GANI AU NI AKINA NANIHII KIONGONZI WA MGOMO
ReplyDeleteukiona dakitari hafanyi haki kasomee udakitari au shawishi watoto wako wachukue fani hii sio kukwepa masomo ya sayansi jamani.
ReplyDeleteWe unayejiita ETIENNE sidhani kama ni M-TZ halisi! Nadhani uko nje ya nchi na kama ni M-TZ. Ungekuwa hapa ungepita katika hospitali na ukaona huo mgomo ulivyoua watu! Mie mke wangu na mwanangu walifariki kwa kukosa kufanyiwa operation ya uzazi leo unaandika hivyo kweli!? Ningekuona kwa macho nadhani hata nami ningenyongwa kwa sababu ningekuua kabisa!! tena wale wote wanaounga mkono wasithubutu kwani hawakufiwa na watu wao wa karibu!
ReplyDeleteOMG we Anony wa (Wed Jul 11, 10:29:00 AM 2012) hapo juu. USHINDWE NA ULEGEE KABISA. You cant judge a book by its cover. How would you say he is Kibaka jamani? This is sad, sad, sad. Ndio nyie wa kukatisha watu tamaa katika maisha yao. Go..Go..Dr. Mkopi. Good luck in what you are facing bro. Achana na hawa wanaokuona wewe Kibaka. Hivi angekuwa kaka yako ungemuita Kibaka. NonSense kabisa!
ReplyDeleteNadhani sarikali sasa ifanye kile ambacho Watza wengi tunakitarajia.
ReplyDeleteWaoneshe kwamba tumewaamini na kuwapa mamlaka sio kuchezewa chezewa na CDM na associates wao!
Acheni unafiki, nyie mnaomsema Huyo Dr. Wanahaki ya kudai maslahi yao. Ni kweli kuna Taasisi nyingi za Serikali pia TRA wanapewa pakiti za maziwa, wakati kazi wafanyazo si za RISK kiasi hicho, WHY NOT DOCTOR!!!? ambao wakati wote na mahali popote mikono yake inaogelea kwenye MADIMBWI YA DAMU.
ReplyDeleteNchi hii hata kama inaongozwa na utawala wa Sheria, haimaanishi ndio kutisha wananchi. Hebu tumuogope Mwenyezi Mungu na tuambiane ukweli kama huu;
(1) Wabunge wetu mpaka sasa wana lipi jipya? Wanalipwa mishahara minono na allowance kibao, pia wakiumwa wanapelekwa nje, kwa nini tusipiganie haki ya kuwa na wao pia watibiwe hapa?
(2) Naamini Dr huyu alichaguliwa na wenzie, kuwaongoza, ameaminika kwa hiyo asimamapo ni kwa niaba ya wenzie. Mbona tunapiga kelele hali ngumu hali ngumu, hali Landcruiser kibao za Serikali ziko mitaani zimezagaa kwenye mambo yasiyo ya msingi kwa mfano sasa hivi zinapeleka watoto shule, mama sokoni, kwenye mashamba, kwa vimada. Kwani tusiyauze kwa asilimia 90 na kuwakopesha magari ili tubane matumizi na kupata mishahara ya madaktari na waalimu.
MNYONGE MNYONGENI, HAKI YAKE MPENI.
HAKUNA KAZI YA WITO HAPA, MBONA NYIE MMEKWENDA DODOMA NA ALLOWANCE KIBAO?
WATANZANIA AMKENI. HAWA MADKTARI SIO WANATAFUTA MASLAHI YAO TU, WANACHOPIGANIA NI SERIKALI KUJALI SEKTA NZIMA YA AFYA. KUANZIA WAO WENYEWE KUJALIWA NA KUTHAMINIWA, PIA WANATAKA VIFAA BORA VYA KUKUTIBU WW NA FAMILIA YAKO KWA UFANISI ZAIDI.
ReplyDeleteWATANZANIA BADO HATUJUI MAANA YA SACRIFICE. LEO HAWA MADAKTARI WAKISACRIFICE , PAMOJA NA WW KUATHIKA KWA HILO, KESHO, WW AU MWANAO NDIO WATAKAO NUFAIKA KAMA SERIKALI ITATIMIZA MATAKWA YAO.
mimi nashangaa watu wanaowatetea hawa madaktari,hatukatai madai yao ila mfumo wanaoutumia ni wauwaji wakubwa na wanakiwa kulipia haya matokeo ya vurugu zao,hawa watu wanasomeshwa bure hawana nusu ya mkopo mpaka wanamaliza na bado wakiagiza magari nje ya nchi wanapewa exemption hawalipi ushuru bado hawaridhiki wanatutesa tu watanzania
ReplyDeleteKuna hawa wanaojifanya watetezi wa haki za binadamu ndio wanaowaunga mkono kitu cha ajabu wanaona watu wanakufa sasa hao wanaokufa hawako kwenye hizo haki za binadamu?au wako kwenye haki za kunguni??Nyie watu wa haki za binadamu ningekuwa na mamlaka ningewafungia hivyo vi ofisi vyenu wapuuzi kabisa nyie
Mi kwa mtazamo naona madaktari sheria haiwaruhusu kugoma, sekta zote kwenye nchi zinaumuhimu wake. wadai haki zao bila kusabisha maafa tena ilibidi wt waliogoma wakamatwe na warudishe hela zt za walizosomeshewa
ReplyDeleteMadaktari wana haki ya kudai maslahi bora ... lakini kitendo cha kuacha watu wafe ... ili serikali iwape haki zao ... mie kwa kweli kimeniuma saaaana ... nakuambia hakuna kitu kizuri kama kumjali mtu .... PESA INAPITA ... IKO SIKU ... UNA PESA .. LAKINI UKAKOSA HUDUMA MUHIMU .... PESA SIO KILA KITU ... UTU KWANZA ...
ReplyDeleteTUWE NA UTU NDUGU ZANGU ... UHAI WA MTU HAUNUNULIWI NA KITU ...
KWANI UTAKUFA NA UTAACHA PESA ZOOTE NA NDUGU WATAZIPIGANIA ..... LAKINI SIFA/ MATENDO YAKO HAYATASAULIKA .... UTU KWANZA MENGINE YANAFUATA.....
...WAPO WALIOKUWA TAYARI KUONA WAGONJWA WAKITESEKA ILI MRADI TU MASLAHI YAO KWANZA...HUYU KAMWE HAWEZI KUITWA DAKTARI NI MUUAJI TU.
ReplyDeletePILI, PAMOJA NA KUJUA FANI YAO LAKINI IMEONESHA MADAKTARI WETU BADO WANAUPEO MDOGO WA KUFAHAMU WAJIBU WAO KWA MUJIBU WA FANI UTABIBU. KWA VILE NAAMINI KUWA HII FANI INA PROFESSIONAL COUNCIL BASI MZIZI WA FITNA UTAKATWA HUKO...N AIKIBIDI WATAKAOBAINIKA WALIKWENDA KINYUME NA MAADAILI YA FANI HIYO BASI WAFUTIWE LESENI ZAO KABISA...NI HERI KUWA NA MADAKTARI WACHACHE WANAOJALI KAZI YAO KULIKONI KUWA NA MAMIA WASIOTAKA KUFUATA TARATIBU ZA FANI HIYO
NDUGU YANGU MKOPI ALISHINDWA KUTOFAUTISHA BAINA YA MTAALAM NA MWANASIASA...ALIPOTAKIWA KUTII AMRI YA MAHAKAMA, HAKUTAKIWA KUFANYA UBABE KAMA WALIVYOWAFANYIA WAGONJWA...BALI NI KUFUATA MKONDO ULEULE WA MAHAKAMA AIDHA KWA KUTII AMRI AU KUKATA RUFAAA...KUSHINDWA KUTAMBUA HILI KUMEONESHA UDHAIFU MKUBWA SANA
Jamani wale wote wenye akili na'exposure' ya mambo ya kidunia nauliza: Ni kwa nini ktk nchi zilizoendelea madaktari na manesi wanapata mishahara mikubwa SANA ukilinganisha na wafanyakazi wa sekta nyingine ? Utaratibu huu pia unaonekana ktk baadhi ya nchi za kiafrika. Na kwa nini utaratibu huu umekubalika kwa wananchi wao?
ReplyDeleteTanzania kwa nini karani wa benki kuu au TRA analipwa kuliko daktari, tena wengine wanadiploma tu?
Uganga huu wa kisasa tumeletewa toka ughaibuni lakin wao hawang'ang'anii kuwA kazi ya afya ni wito hivyo posho stahili iwe ndogo. Kwa nini?
Watanzania kwa nini hatupendi afya zetu ziwe mikononi mwa watu walioridhika kimapato na kimazingira ya kazi?
Kwa nini udaktari unasomea muda mrefu, miaka mitano hadi sita?
Fani hii kwa nini ni ngumu kimasomo?
Jamani kwanini fani hii ni ya ajabu na heshma kote ulimwenguni kasoro Tanzania ?
Kwanini...
Mchunguzi.
hana sura ya udaktari
ReplyDeleteJamani wale wote wenye akili na'exposure' ya mambo ya kidunia nauliza: Ni kwa nini ktk nchi zilizoendelea madaktari na manesi wanapata mishahara mikubwa SANA ukilinganisha na wafanyakazi wa sekta nyingine ? Utaratibu huu pia unaonekana ktk baadhi ya nchi za kiafrika. Na kwa nini utaratibu huu umekubalika kwa wananchi wao?
ReplyDeleteTanzania kwa nini karani wa benki kuu au TRA analipwa kuliko daktari, tena wengine wanadiploma tu?
Uganga huu wa kisasa tumeletewa toka ughaibuni lakin wao hawang'ang'anii kuwA kazi ya afya ni wito hivyo posho stahili iwe ndogo. Kwa nini?
Watanzania kwa nini hatupendi afya zetu ziwe mikononi mwa watu walioridhika kimapato na kimazingira ya kazi?
Kwa nini udaktari unasomea muda mrefu, miaka mitano hadi sita?
Fani hii kwa nini ni ngumu kimasomo?
Jamani kwanini fani hii ni ya ajabu na heshma kote ulimwenguni kasoro Tanzania ?
Kwanini...
Mchunguzi.
Hawa madaktari kwanza mishahara yao wawelipwe nusu mshahara wanaogoma au wafukuzwe kazi kabisa,masikini wakubwa nyie.
ReplyDelete