Waziri wa Uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe akitambulishwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Mhandisi Kipallo Aman Kisamfu kwa viongozi wa TRL na wale wa Chama cha Wafanyakazi wa Reli TRAWU mara alipowasili katika Karakana ya TRL.
Waziri Mwakyembe akipata maelezo ya jinsi ya ukarabati wa mabehewa 14 unavyoendelea kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Mhandisi Kipallo Aman Kisamfu wa kwanza kulia.
Baadhi ya mabehewa yanayokarabatiwa kwa ajili ya huduma ya usafiri kwa Wakazi wa jiji la Dar.
Viberenge viwili malum vikijitayarisha kuondoka kuelekea Ubungo wakati wa ukaguzi wa njia ya reli ambayo itatumiwa na treni ya abiria ya Wakazi wa jiji la Dar es Salaam inayotarajiwa kutoa huduma hapo Oktoba mwaka huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 26 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 10, 2012

    HIvi ni Kweli NIna furaha Sana
    Hii itamaliza folen Jamani. Ila umakini uanagaliwe swala la Ajali

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 11, 2012

    Hongera Mwakyembe,Kwani mwanzo tulikua wapi? sasa treni lingine liende mpaka mbagala,lingine mpaka kimara, kwisha mchezo.hakuna haja ya mabasi ya kasi,yatakufa tu kama uda
    Viva TZ
    Zongwe

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 11, 2012

    Asante Mwakyembe, asante Kikwete. Endeleeni kututatulia kero hii kubwa ya usafiri. Tunaomba muongeze kasi sana, yaani sana.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 11, 2012

    Nafurahi sana pia.JK atafute wachapa kazi wengine kama Mzee Mwakyembe ili tuinusuru CCM.pia tujiandae tuwekeze kwenye treni za speed taratibu.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 11, 2012

    Mwakyembeee kanyaga mwendo twendeee! Haya ndo mambo sasa,Tungepata kina Mwakyembe 50 hakika Tanzania ingekuwa Paradiso! Tukishamaliaza ya matreni tuingie majini , kigamboni, kawe, bunju,kunduchi yaani chombo kinaambaambaa kandokando mpaka bagamoyo yaani shida ya usafiri, foleni itakuwa kwisha!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 11, 2012

    Hii huduma kama inakuja mbona itakua mkombozi kwenye foleni. Kwa hii foleni ya sasa, I can not wait!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 11, 2012

    lakini kwanini watu wakamtenda hivi Mwakyembe? hivi kweli watanzania tumefika huko kweli?? Ahhh, inatia uchungu sana.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 11, 2012

    Yarabii, muliyoko nje rudini, tena kwa mwendo wa mabasi ya kasi, mambo huku bongo sasa kama Tokyo, treni zipo, daladala zipo, mabasi ya kasi yapo. sasa tena nini kinawakalisha huko ??? mashoping center ya nguvu yapo, rusha roho hiyo ni kila siku mpaka saa 9 za asubuhi-yaani mpaka treni ???? hii leo hata mimi nimeihusudu babu kubwa-kwa mwendo huu !!!! labda CCM itashinda tena uchaguzi-lakini bado uoza bado mwingi , Tannesco je ??? Zebedayo msem kweli.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 11, 2012

    Mbona hiyo railway track iko moja tuu meaning one way, they should construct another one to make it two way. Otherwise good job Mwakyembe! Thats how we roll, the railway is long due

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 11, 2012

    Saaafiiiiiii. sasa mabidiliko yana kuja. mwakyembe na magufuli ndo majembe ya kweli. tunataka wachapakazi kama nyie. sio bla x2.

    ReplyDelete
  11. A commendable idea!

    Marvellous..!

    Asante Mwakyembe Mungu akupe nguvu na uhai mrefu..

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 11, 2012

    Hii ni Taarifa nzuri sana kwetu sisi wakazi wa Dar es Salaam itatupunguzia adha ya Usafiri. Kikwete tafuta majembe kama kina Mwakyembe ili kukata ngebe za jamaa fulani.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 11, 2012

    tatizo kubwa litakuwa kwenye junctions kama tabata reli, tabata dampo, buguruni kwa mnyamani na jirani na tazara, maeneo ya kariakoo, nk. Kama reli ingekuwa inapita chini/juu ya barabara kwenye junctions basi ingekuwa nafuu. lakini kwa madereva wa daladala tulionao basi tusubiri ajali kibaaaaaaao.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 11, 2012

    Hivi hawajaiba machuma yale. Itabidi kuwe na ulinzi wa hali ya juu. Wasiopenda CCM isifike wataweza wakaharibu tu, kama walivyomharibu Dr. Ulimboka.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 11, 2012

    waw...i cannot believe it! big up Mwakyembe!

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 11, 2012

    Hwa waliokuwa wanakalia mradi wa mabasi ya mwendo kasi walipe hizo pesa za world bank wenyewe. Wanajulikana na walikuwa wanahofia daladala zao kukosa kazi. wananchi hatuwezi kubebeshwa mizigo na wachache kwa faida zao binafsi, tunawajua wawajibishwe.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 11, 2012

    Hongera mwakwembe na magufuli, hawa ndio watanzania, wanoipenda nchi yao Tanzania na kujivunia na nchi yao.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 11, 2012

    watu kama mwakyembbe ndio tunawahitaji. tabia ya kutoa nzi wa chooni na kuleta wa sebuleni ife. tuwape watu vitengo kwa kuangalia uwezo na uzalendo. aahhhsante mwakyembe hapo ulipo panakufaaa jembe.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 11, 2012

    nauliza hiyo train itapita wapi? maana kule mbezi watu wamejenga juu reli.
    otherwise big up na tunasubiri kwa hamu

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 11, 2012

    Tanzania inawezekana .Hongera Rais Kikwete na Serikali.
    Cha kuangalia ni kuweka ulinzi mkali kwa wasiopenda maendeleo na Serikali wanaweza kuweka mizengwe na kusababisha uharibifu.

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 11, 2012

    Mwakyembe hongeraaaaaaaaaaaaaa!! kweli wewe u mtu wa Mungu.Wabaya wako wamevaa aibu iliyoje? Mungu na akutangulie uwakomboe watanzania wake kwa maana wameteseka mno kutokana na viongozi wabovu wasiomwogopa Mungu. Just imagine the possibilities of the sleeping railway resources in the country to solve transportation problems and save our roads from being overwhelmed by the heavy loads on transit.

    ReplyDelete
  22. AnonymousJuly 11, 2012

    Nampongeza waziri mwakyembe kwa kubuni mambo na kuyafuatilia ili yafanyike naomba hiyo njia ya
    treni ijegwe mpaka mbezi hata chalinze kwa kuwapa wachina hiyo kazi pia gorofa la tanesco lisivunjwe badala yake barabara ipite mbele yake na wao waingilie kwa nyuma au kwa chini ili kuepusha hasara kubwa

    ReplyDelete
  23. Hongera Dr.mwakyembe kazi unaijua sana, unauchungu na watu wa nchi hii hakuna kusubiri, mabadiliko ni sasa unaonyesha njia na wengine wajitahidi kwenye maeneo yao si lazima kusubiri mpaka Rais aonyeshe njia. Kila mtu ana uwezo wake kwenye kazi hakuna kutazamia kwa mtu. Kila mtu atimize wajibu wake.Tanzania iliyo na neema inawezekana. Kidole kimoja hakivunji chawa, watumishi wa TRL msaidiyeni DR.

    ReplyDelete
  24. AnonymousJuly 11, 2012

    Mdau aliyesema walioko nje warudi! tatitzo si usafiri tu. Tunahofia masuala ya afya pia. Mtu ukiumwa mpaka uende Afrika ya kusini oo sijui india! Hapa tulishapazoea na bila shaka hapo kaeni tu. Hivyoo hivyo kila mtu kivyake vyake! au vipi!

    ReplyDelete
  25. AnonymousJuly 12, 2012

    Jamani kumbukeni kuwa huu mradi uliibuka kwanza enzi ya Mwinyi kisha ukafa kifo cha mende! Kweli twahitaji wawajibikaji. Mipango tunayo ila utekeleza sufuri.Mfumo mzima wa serikali na mashirika unawakwaza wachapa kazi. Wachapakazi wanaonekana wanoko au wanga! Twahitaji 'udikteta wa kimaendeleo'.
    HT.

    ReplyDelete
  26. AnonymousJuly 12, 2012

    subiri waosha vinywa, utasikia viti vibovu, kutu nk. watagoma watake kama za ulaya. Hongera Dr. Mwakwenyembe na wataalamu wako. Kuna jamaa wa TRA alikuwa akigombana sana na wahindi yeye ni fundi alikuwa nafufua injia wahindi wanagoma yupo wapi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...