Rais Mstaafu wa Tanzania Mhe. Benjamin Mkapa akihitimisha mjadala kuhusu Mpango wa Tohara ya Hiari kwa Wanaume ili kupunguza maambukizi ya UKIMWI kwenye mojawapo ya mikutano ya Kongamano la UKIMWI kwenye Ukumbi wa Mikutano wa mjini Washington D.C.
Mkutano ukiendelea.
Ma-Champion wa HIV Free-Generation Rais Mstaafu wa Tanzania Mhe. Benjamin Mkapa, Rais Mstaafu wa Msumbiji Mhe. Joachim Chisano na Rais Mstaafu wa Zambia Mhe. Kenneth Kaunda pamoja na wadau wengine wakiwa kwenye Ukumbi wa Mikutano wa mjini Washington D.C kuhudhulia mikutano ya Kongamano la UKIMWI.
Mkapa alikuwa rais poa sana na aliimarisha uchumi wa kibongo kiaina na thamani ya tshs ilikuwa stable sana ktk uongozi wake ingawa ana mapungufu mengi ya kutumia madaraka wakati ule wa urais kwa maandalizi ya baadaye ya kujiwekea vyeo kibao ,mara ununuzi wa songwa songwa ,vyeo kibao mkuu wa uni Dom ,mavyeo kibao mtu mmoja na mshahara wake kama raisi mstaafu ankula mpaka mwisho wa maisha yake.Je ni nini maana ya kustaafu?Huyu huyu anaiwakilisha nchi na cheo kingine tena USA.Ina maanisha hakuna mtu mwenye sifa za kufanya kazi hizi bongo?Au ameweka maslahi yake mbele kama rais wa urus Puttin ambaye amediliki kubadilisha katiba ya nchi na kugombea tena urais?Je tunaelekea wapi?Haya yote enzi za mwalimu hayakuwepo au kipindi cha Mwinyi hayakuwepo.Yetu macho ,je kikwete atakuja na staili gani baada ya kipindi chake kuisha?Ustadhi Michuzi niwekee tafadhali comment yangu hewani ,Mdau
ReplyDeleteWanaume wafanye tohara kujiepusha na ukimwi, na sisi wanawake tufanyeje kujiepusha na ukimwi? au sisi mmetutoa sadaka ya kuteketezwa.
ReplyDeleteWanawake epukeni ngono zembe,mtapona. Wewe unaelalamika Ben kuiwakilisha nchi jua kwamba hajaenda kama mwakilishi wa nchi. Ben ana taasisi inayojishughulisha na UKIMWI, ndio sababu kaalikwa so be polite about it.
ReplyDeleteMdau hapo juu ,kwa wanawake pia mna chance ya kujizuia ,ila ninasikitika sana kama wewe haujui njia ya kujizuia.Kuna condom hadi za wanawake hivyo dunia ya sasa acha kufanya ngono zembe ,hii imekaa vibaya sana.Nenda na umpendae mara kwa mara kupima.Mimi nina mke wangu lakini hatuaminiani ,ninatumia condom,kwani ukimwi haupimwi kwa macho.Mdau
ReplyDeleteMdau hapo juu ,kwa wanawake pia mna chance ya kujizuia ,ila ninasikitika sana kama wewe haujui njia ya kujizuia.Kuna condom hadi za wanawake hivyo dunia ya sasa acha kufanya ngono zembe ,hii imekaa vibaya sana.Nenda na umpendae mara kwa mara kupima.Mimi nina mke wangu lakini hatuaminiani ,ninatumia condom,kwani ukimwi haupimwi kwa macho.Mdau
ReplyDeleteThu Jul 26, 12:51:00 PM 2012
KAAZI KWELI KWELI!