Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Ali Mohamed Shein, (wa tatu kushoto) akijumuika na Viongozi na wananchi wa Mkoa wa kaskazini Pemba katika Futari aliyowaandalia katika viwanja vya Ikulu ya Wete pemba jana. 
Baadhi ya wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, wakiwa katika chakula cha Futari waliyoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Ali Mohamed Shein,katika viwanja vya Ikulu ya Wete Pemba jana. Pichana Ramadhan Othman,Ikulu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 31, 2012

    Hii ndio namna nzuri ya kuftari

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 31, 2012

    Sasa hao wote watakuwa wana CCM kesho.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 31, 2012

    Naomba kupata ufafanuzi juu ya hili neno KUFUTURISHA hasa KISARUI. Naelewa kitenzi ni KUFUTU. Unaposema Raisi afuturisha KISARUFI MAANA YAKE NINI. Nauliza maana tupo katika kuboresha lugha yetu ya kiswahili.

    Asante.

    ReplyDelete
  4. Asili ya neno hili ni Futari chakula kinacholiwa baada ya kufunga. Kufutari ndio kitendo cha Kula futati. Futuru, kwa waswahili wazawa ni neno lisilofaa kutumika km linavyotumika kwa baadhi ya watu kufuturisha,kiserufi ni sawa lkn kimaana halifai kumaanisha kufutari.

    ReplyDelete
  5. KUFUTARI LIMETOKANA NA NENO FUTARI KAMA ILIVYO CHAKULA LILIVYOTOKANA NA NENO KULA NA SI KAMA WATU WENGINE WANAVYOSEMA KUFUTURU KWASABABU KILA NENO LINA MZIZI WAKE KISARUFI
    NAWAKILISHA

    ReplyDelete
  6. Anon. no 3. uliyeomba ufafanuzi, hilo neno unalotaka kufahamishwa kisarufi, kwanza kwa nnavyofaham mie, neno hilo limetokana na lugha ya KIARABU ambalo ni 'IFTAR' au kwa lugha ya kiarabu ni ( إفطار‎ ) likimaanisha ule mlo wa jioni wanaokula WAISLAM wakati wakifunguwa SAUMU zao katika MWEZI MTUKUFU WA RAMADHAN au hata siku nyinginezo tu endapo mtu anapokuwa kathibitikiwa kufunga for some reasons. Nadhani hata hicho kitenzi ulichokiandika wewe KUFUTU, kina mushkel kidogo, maana ukitaka kukinyambua nacho kitaleta maneno yenye maana anuwai na kuipotosha maana husika uliyoidhamiria wewe.

    Na tunaposema Raisi anafturisha/anaftarisha, tunamaanisha badala ya kufturu/kuftari yeye pengine na jamaa/familia yake tu, basi anaamuwa kuwaalika WAUMINI wenzake wote wa KIISLAM, khalafu zinaandaliwa FTARI kadha wakadhalika, then wakishamaliza kusali swala ya Maghrib, hapo tena wanajumuika kwa pamoja katika KUFTRATI (kula mlo huo kama nlivyofahamisha maana yake hapo juu) na ndio kama uwaonavyo hapo kwenye picha.

    N.B. Hilo neno "IFTAR" sometimes tunatofautiana kimatamshi, wengine husema FUTARI na wengine FTARI na kwenye kutenda kadhalika, wengine husema FUTURISHA/FTURISHA na wengine husema FUTARISHA/FTARISHA, bado maana ni hiyo hiyo moja. Nimefahamisha kwa upande wangu, utaniwia radhi kama nimekosea, wataalam zaidi kama wapo, basi watatufahamisha vizuri.

    ReplyDelete
  7. kitenzi ni KUFUTURU (wengine husema KUFUTARI)na siyo KUFUTU.

    ReplyDelete
  8. Kufuturisha maana yaje ni kuwa ameghalimia (ameandaa) huo mlo na kuwaita watu wengine kujumuika kula pamoja.

    ReplyDelete
  9. Kaeni mwzani; nendeni na wakati! Sio enzi za mahema mahema jangwani!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...