Jumuiya wa Watanzania waishio nchini Korea ya Kusini imepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa sana taarifa ya ajali ya Meli ya MV.SKAGIT iliyotokea wiki hii wakati ikisafili kutoka Dar es salaam kwenda Unguja Zanzibar tarehe 10 Julai 2012.
Tunapenda kuungana na watanzania wote kuwapa pole ndugu na jamaa waliopoteza wapendwa wao vile vile tunawatakia heri majeruhi wote waweze kupona haraka ili waendelee na shughuli za ujenzi wa Taifa.
Tunawapongeza wote waliofanya juhudi za oukoaji na kuitoa miili ya marehemu kwenye meli iliyozama, Mwenyezi Mungu awape maarifa na moyo wa uvumilivu katika kuitenda kazi hii.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehma azipokee roho za marehemu na azihifadhi mahali pema peponi milele – AMINA
Imetolewana:
Emmanuel Lupilya-
Mwenyekitiwa Jumuiya ya Watanzania nchini Korea
Kila kukicha majanga, majanga, majanga, na sasa Zanzibar inaongoza kwa ajali za majini. Hii maana yake nini kwa watu wa Imani na wanaomcha Mungu? Je kuna mahali tumekosea? Basi tumrudie Mola na kutubu dhambi zetu.....
ReplyDeleteHaya ni madhara ya kuendelea kutumia vyombo ya usafiri vilivyo chakaa, tunapenda dezo na gharama yake ndo hii.Mungu Ibariki Tanzania
ReplyDeleteHaya ndo madhara ya kuendelea kutumia vyombo chakavu, mamlaka husika hakikisheni vyombo ya usafiri ni salama ili tuondokane na haya majanga ya mara kwa mara.Mungu tusaidie
ReplyDelete