Jumuiya wa Watanzania waishio nchini Korea ya Kusini imepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa sana taarifa ya ajali ya Meli ya MV.SKAGIT iliyotokea wiki hii wakati ikisafili kutoka Dar es salaam kwenda Unguja Zanzibar tarehe 10 Julai 2012.

Tunapenda kuungana na watanzania wote kuwapa pole ndugu na jamaa waliopoteza wapendwa wao vile vile tunawatakia heri majeruhi wote waweze kupona haraka ili waendelee na shughuli za ujenzi wa Taifa.

Tunawapongeza wote waliofanya juhudi za oukoaji na kuitoa miili ya marehemu kwenye meli iliyozama, Mwenyezi Mungu awape maarifa na moyo wa uvumilivu katika kuitenda kazi hii.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehma azipokee roho za marehemu na azihifadhi mahali pema peponi milele – AMINA

Imetolewana:

Emmanuel Lupilya-
Mwenyekitiwa Jumuiya ya Watanzania nchini Korea

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 22, 2012

    Kila kukicha majanga, majanga, majanga, na sasa Zanzibar inaongoza kwa ajali za majini. Hii maana yake nini kwa watu wa Imani na wanaomcha Mungu? Je kuna mahali tumekosea? Basi tumrudie Mola na kutubu dhambi zetu.....

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 22, 2012

    Haya ni madhara ya kuendelea kutumia vyombo ya usafiri vilivyo chakaa, tunapenda dezo na gharama yake ndo hii.Mungu Ibariki Tanzania

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 22, 2012

    Haya ndo madhara ya kuendelea kutumia vyombo chakavu, mamlaka husika hakikisheni vyombo ya usafiri ni salama ili tuondokane na haya majanga ya mara kwa mara.Mungu tusaidie

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...