Wanachama wa CCM tawi la DMV tunaungana na watanzania wenzetu popote duniani kutoa salamu Za rambi rambi kwa Kuondokewa na MZEE WETU MKONGWE WA CHAMA CHA MAPINDUZI, NDUGU AZZAN ALLY MANGUSHI.
Mzee wetu, atakumbukwa kwa hoja zake za kuchangia mambo mbali mbali ndani ya chama cha mapinduzi hasa kipindi alivyoweza kushika nafasi ya mjumbe wa halmashauri kuu ya kinondoni-Dar es salaam na mambo mengi yaliyoweza kulijenga taifa la Tanzania. Wanachama wa ccm wameondokewa na kiongozi imara na shupavu katika siasa.
Sisi wananchama wa CCM tawi la Washington, DC Maryland na Virginia tunatoa salamu za rambi rambi kwa ndugu wa marehemu na wanachama wa CCM popote duniani katika kipindi hiki kigumu.
Mungu ailaze roho ya mzee wetu huyu peponi - Amin
Uongozi
Tawi la ccm-DMV
Marekani
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...