Balozi wa Tanzania nchini Japan Mhe. Salome Sijaona akiwaelezea wageni wake  uzuri wa nchi ya Tanzania. Katika maelezo yake, Mh. Sijaona alisisitiza kuwa Tanzania ni moja kati ya nchi 54 zinazounda Bara la Afrika na kuwataka Wajapani kuacha imani kuwa Afrika ni nchi moja.
 Maafisa Ubalozi wa Tanzania nchini Japani, Mama Scolla Kavishe na Agnes Lukwago wakitoa maelezo ya namna kanga zinavyovaliwa baada ya kuwavisha wanawake wote waliohudhuria shughuli hiyo.

 Francis Mossongo, Afisa Ubalozi wa Tanzania akisikiliza swali kutoka kwa washiriki kuhusiana na mambo ya uwekezaji Tanzania.
 Mheshimiwa Balozi Sijaona akiwa pamoja na maafisa ubalozi, baadhi ya watanzania walioko Tokyo na Wajapani waliokuwa kwenye Lunch Trip.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 25, 2012

    Vazi la Taifa,

    Tusipoteze muda bureee vazi la Taifa tusimamie kwenye Mgolole wa Kimasai!

    Asiye taka atakuwa si mwingine bali ni Mtani wetu sisi Wamasai!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...