Kwa sababu ya Poor copyrights and Income Managment , naamini Serikali Huenda ikawa inapoteza Fedha Zisizopungua Shillingi za Kitanzania Million Hamsini (50,000,000.00) kwa kila watanzania Millioni Moja (1,000,000) wanatumia Simu au Kuingiza nyimbo kwenye simu au kurekodiwa kwenye CD.

Hii ni kwa hesabu zangu za darasa la nne :-

Nyimbo sasa hivi zinaingizwa kwa 200/= hadi 500/= kwenye CD au SIMU / Per Song.

Hivi kama kungekuwa na utaratibu wa kusimamia hizi kazi za wasanii kwa asilimia ndogo tu, unafikiri vijana wangekimbia mashamba?

Banana, Dully, Diamond, Ally Kiba na wengineo wengi wangekuwa na mashamba makubwa na wala kusingekuwa na shida ya chakula.

Anyway, back to my subject.

Kama Kukiwa na usimamizi mzuri naamini kila msanii anaetoa nyimbo na ikasimamiwa vizuri na Serikali au wasimamizi wengine watakaolindwa na serikali basi kila nyimbo inaweza (Rate Ya Watu 1,000,000 tu) :-

Kumpatia Muuzaji / Anayeweka nyimbo kwenye simu : Tsh 150 - 300 kwa nyimbo.
Kumingizia Kipato Msanii : Tsh 50,000,000 kwa nyimbo x (1,000,000 x Tsh 50).
Kuiingizia Kodi Serikali : Tsh 50,000,000 kwa nyimbo = (1,000,000 x Tsh 50).

Ni Hayo Tu.

TAFAKARI - CHUKUA HATUA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 25, 2012

    Dream on ndugu. Serikali cant even regulate its major source of income, taxes, and you are thinking about songs and copy rights? Nyimbo zenyewe unaongelea bongo fleva which rarely portray "Tanzanianism". I praise you for the simple math to show when magnified can made much difference but music industry (and economics behind it) is tougher than you can simply think.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 25, 2012

    Siyo "kila nyimbo" bali ni "kila wimbo."

    Sasa zikiwa nyingi utaziitaje? Utaziitta "zimbo"?

    Kuwaiga Wakenya na Kiswahili chao kibovu ni ujuha. Hii ni lugha yetu tuacheni uzungukuku.

    Matinyi.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 25, 2012

    AHSANTENI, HAYA NDIO MAMBO YA KUYAFUATILIA KWA KUTUMIA SHERIA, WENZENU WANAPATA FEDHA KIULAINI KWA KUTUMIA NYIMBO ZENU MLIOUMIA KUZITUNGA NA KUZIIMBA ZIKAPENDWA, NAWAKUMBUSHA NYIMBO NI NYINGI N MMOJA NI WIMBO, KICHWA CHA HABARI HAKIKO SAWA.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 25, 2012

    Nashukuru Matinyi kwa somo,

    Huwa nakereka sana utamsikia unasema hii nyimbo naipenda sana! badala ya wimbo.

    Tafadhali!

    Ukiwa mmoja ni WIMBO na zikiwa nyingi ni NYIMBO

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 25, 2012

    Tuko vizuri katika kuendeleza mijadala sio kuanzisha!

    sesophy

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 26, 2012

    ndo maana wabongo atuendelei mtu katoa hoja yakunufaisha watanzania wote, badala yakufikiria jinsi ganiyakufanya ili iweze kufanikiwa mnaanza kupinga nakumsaisha kiswahili chake, kweli tutasonga kweli? jamani naomba tuwe watu wakufikiri na kuwapositive, negativity doesn't take us anywhere...

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 26, 2012

    Wewe Matinyi hacha hizo. Kwa hiyo Wakenya Kiswahili siyo lugha yao? Haluu... Wakenya na Watanzania wote wanakosea kwenye kuzungumza lugha fasaha. Si ajabu kuna Watanzania wengi tu walianguka mtihani wa Kiswahili wakati ndio "lugha mama"

    Hivyo usiwajumlishe watu. Sema fulani... kwa maana "Wakenya" hawazungumzi lugha kwa pamoja. Vivyo hivyo "Watanzania" hawazungumzi lugha kwa pamoja.

    Kuna wanaozungumza lugha fasaha na kuna ambao wanakosea.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 26, 2012

    Na wewe Matinyi hakuna neno 'zungukuku'... ni zumbukuku.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 26, 2012

    Pia namkumbusha mdau hapo juu kwamba hakuna neno "hacha" bora ungesema "acha" au "wacha".

    Hata hivyo mbona wabongo kuibiwa mlishaona ni sehemu ya utamaduni wenu? Mnawachoma vibaka wanaowaiwaibia simu za sh 50,000/= mnawaacha wanaowaibia mabilioni! Shame on you!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...