Waziri wa Mamboya ndani wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Emanuel Nchimbi alifikakatika Eneo lililohifadhiwa Maiti wa Ajali ya Meli ya Skagit ili kutambuliwa na Ndugu zao na Kupata maelezo kwa Daktari Kiongozi hayupo pichani Hapo katika Viwanja Vya Maisara Zanzibar.
Baadhi ya Maiti zilizookolewa kutoka katika Meli iliozama na kukosa watu wake zikipelekwa kuzikwa na Serikali katika Eneo la Kama lililotayarishwa makusudi kwa ajili hio.
Balozi wa Marekani Nchini Tanzania Learnhat Alfonso wakatikati akionekana na huzuni Baada ya kuziona Maiti zilizookolewa katika Meli iliozama hapo jana katika Bahari ya Chumbe Zanzibar.Balozi alifika katika Viwanja vya Maisara ili kuona namna shughuli za kushughulikia maiti zinavyoendelea.
BOFYA HAPA KUONA PICHA ZINGINE
BOFYA HAPA KUONA PICHA ZINGINE


Jamani Tanzania viongozi milopewa dhamana mtatumaliza kwa sababu ya rushwa. Iweje meli iruhusiwe kubeba abiria bila hata maboya ya kujiokolea? Halafu meli haizami kama jiwe ilikuwaje hii ikazama haraka namna hiyo? Hata kutuma ujumbe wa dharura kuomba msaada ilishindikana? Watu wenye pesa wanatumia pesa zao kwa kutoa rushwa na kupewa leseni za kusafirisha abiria bila kujali usalama na maisha ya abiria hao. Hayati Baba wa Taifa alisema "Ubepari ni Unyama" na huu nao ni unyama. Rushwa itaendelea kuleta maafa kwa wanyonge Tanzania. Kuzama kwa meli sasa inaelekea kuwa kitu cha kawaida tu.
ReplyDeleteSiku moja tu haitoshi kusema kwamba maiti za wahanga wamekosa ndugu!
ReplyDeleteeeeh mungu wetu .... this is crazy!
ReplyDeleteR.I.P. kwa wale wote waliohusika. Swali humu ndani, hivi maiti INAOKOLEWA au KUOPOLEWA toka kwenye maji? Msinielewe vibaya mie elimu yangu ya 1979 labda sijaelewa vizuri tu.
ReplyDeleteInahuzunisha sana jamani. lakini mbona hawa watu wanazikwa kwa imani moja tu? kila anayekwenda Zanzibar ni wa imani hiyo? just curiosity to know
ReplyDeleteMaiti inaopolewa toka kwenye maji, majeruhi wanaokolewa toka kwenye maji.
ReplyDelete