Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Balozi Tuvako Manongi kuwa Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, New York.

Taarifa iliyotolewa leo, Jumatano, Julai 25, 2012 na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Bwana Peniel Lyimo kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Dar es Salaam imesema kuwa uteuzi huo ulianza jana, Julai 24, 2012.

Kabla ya uteuzi wake, Balozi Manongi ambaye ni ofisa wa miaka mingi wa masuala ya nchi za nje, alikuwa Mshauri Mwandamizi katika Ofisi ya Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, New York.

Balozi Manongi anachukua nafasi ya Balozi Ombeni Y. Sefue ambaye aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi Desemba 30, mwaka jana, 2011.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
25 Julai, 2012

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 25, 2012

    Hii imekaa vizuri. Balozi Manongi yupo hapo hapo UN kwa hiyo gharama sio nyingi. Halafu bi mkubwa alikuwa hapo juzi ndio amemshauri nini?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 25, 2012

    Zanzibar hakuna mwenye akili kwanini watoke bars tu. Udumu Muungano!!.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 26, 2012

    wale wale kutoka kitivo cha sheria UDSM

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 26, 2012

    chaguo lililo bora mhe rais umemteua mtu anaestahili na anaijua UN na mchapa kazi asdiyependa majivuno. mungu ibariki tanzania mungu ibariki afrika.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 27, 2012

    Hivi huu msiba wa IKULU kutumia YAHOO EMAIL ADDRESS utaendelea mpaka lini, yaani hakuna kweli mtu mwenye uchungu na nchii hii anayeliona hili au watu wamekalia kuvuta posho na mishahara tu na mawazo mgando bila kuwa na vision yoyote na kazi? maskini nchi yangu Tanzania

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...