Ofisa wa Sera na Utafiti CHADEMA Makao Makuu Bw. Waitara Mwita Mwikwabe
---

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)
Tamko Kuhusu Yaliyojiri Katika Mkutano wa Hadhara wa CHADEMA Uliofanyika Kata ya Ndago Siku ya Jumamosi Tarehe 14 Julai 2012
1. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kiliandaa mikutano ya hadhara katika Jimbo la Iramba Magharibi. Mikutano hiyo ilitolewa taarifa polisi na jeshi hilo lilitoa baraka zake kama utaratibu wa sheria unavyotaka kwa barua yake ya tarehe 12 Julai 2012 Kumb. Na. KIO/ B1/1/VOL.V/268
2. Mkutano wa kwanza ulipangwa kufanyika katika Kata ya Ndago katika viwanja vilivyo karibu na kituo cha mabasi ambapo pia ni hatua chache karibu kabisa na Kituo cha Polisi Ndago. Mkutano huu ulipangwa kuanza saa nane mchana.
3. Msafara wa kitaifa unaofanya ziara ya ukaguzi wa chama, katika mkoa wa Singida chini ya uratibu wa Ofisa wa Sera na Utafiti Makao Makuu, Mwita Mwikwambe Waitara, (ikiwa ni maandalizi ya operesheni nyingine kubwa mkoani humo itakayofanyika baadae), uliwasili katika eneo la Mkutano majira ya saa tisa na nusu alasiri. Tulikuta wananchi wengi
wakiwa wanatusubiri. Kabla ya Mkutano kuanza tulipewa taarifa kwamba kuna kikundi cha vijana kimeandaliwa kuvuruga mkutano wa CHADEMA kwa kufanya fujo, ikiwemo kurusha mawe ili mkutano huo usifanyike. Suala hilo lilielezwa mkutanoni mapema na Mheshimiwa Waitara, mbele ya askari polisi.
4. Wakati tukijiandaa kuanza hotuba, vijana wapatao wanane walianza chokochoko kwa kutoa matusi na punde mawe yakaanza kurushwa kutoka sehemu mbalimbali. Wakati fujo zinaanzishwa na kile kikundi, Mheshimiwa Waitara alikuwa bado anazungumza na wananchi kuwaandaa kusikiliza wazungumzaji wengine. Vurumai hiyo ilizimwa na wananchi
wenyewe wa Ndago waliokuwa na hamu ya kusikiliza ujumbe wa viongozi wa kitaifa wa CHADEMA.
5. Kwa kweli tunawashukuru wananchi wengi wa Ndago walioonesha ujasiri mkubwa kuweza kuwaondoa vijana wale eneo la mkutano, kisha mkutano ukaendelea, huku wananchi wakionesha kila hamasa ya kufurahia hoja kutoka kwa wazungumzaji, akiwemo Mheshimiwa John Mnyika, ambaye aliombwa ahudhurie ziara hiyo kwa nafasi yake ya Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CHADEMA.
6. Mpaka tunamaliza mkutano huo ambao wananchi waliufurahia sana kwa namna ulivyohutubiwa kwa amani na utulivu huku wazungumzaji wakijenga hoja juu ya mstakabali wa jimbo na taifa lao kwa ujumla, mamia ya wananchi waliohudhuria walitaka tuendelea kuhutubia, lakini tulibanwa na ratiba ya kuwahi mkutano wa pili, eneo la Kinampanda.
7. Lakini kutokana na vurugu hizo zilizokuwa zikisababishwa na kikundi cha vijana ambao tayari ilishatolewa taarifa yao kwenye mkutano huo, lakini askari waliokuwepo hawakuthubutu kuchukua hatua, tulilazimika kuomba msaada kutoka kwa OCD na R.P.C, ambapo baadae wakati mkutano unakaribia kuisha tuliona gari la polisi kutoka Mjini Singida likiwa na askari waliojipanga rasmi kwa ajili ya kuzuia vurugu likifika pale
eneo la mkutano, lakini wakati huo hali ilishatulia na hotuba zimetolewa vizuri.
8. Kutokana na hali hiyo ya vurugu, zilitolewa taarifa Kituo cha Polisi cha Ndago, ambapo lilifunguliwa jalada NDG/RB/190/2012. Katika jalada hilo tulitaja baadhi ya majina ya watuhumiwa waliokuwa vinara wa kundi lililokuwa likifanya fujo kwenye mkutano mbele ya askari polisi. Majina hayo ni; 1. Daniel Sima, 2. Tito Nitwa, 3. Bakili Ayubu, 4. Yohana Makala Mpande, 5. Ernest Kadege, 6. Abel John, 7. Athuman Ntimbu, 8. Martin Manase, 9. James Ernest, 10. Simion Makacha, 11. Anton John, 12. Frank Yesaya
9. Kwa hakika askari polisi wa Ndago waliokuwepo mkutanoni mbali ya kutochukua hatua yoyote dhidi ya fujo tulizofanyiwa ikiwemo kupondwa mawe na kikundi kidogo cha wahuni, fujo zilipozidi askari wote walikimbia eneo la mkutano, akabaki OCS pekee ambaye naye alionekana dhahiri kutotaka kuchukua hatua stahili. Hakuonekana kufanya juhudi zozote za kuhakikisha amani inalindwa na ulinzi unaimarishwa katika eneo la mkutano na hatua zinachukuliwa dhidi ya watu walioonekana kudhamiria kufanya fujo.

Mtu yeyote makini angeweza kuona kuwa askari wale walikuwepo pale mkutanoni ‘almuradi’ tu lakini kama vile walikuwa na maelekezo maalum ya kuhakikisha hawachukui hatua yoyote katika kuzuia mpango wowote wa kusababisha vurugu na kuvunja amani.
10. Baada ya kumaliza mkutano wa Ndago kwa amani, tulikwenda Kinampanda ambako tulifanya mkutano mwingine mzuri kwa amani kabisa, ambapo mbali ya wananchi kuwa wametusubiri kwa hamu kubwa na kutusikiliza kwa makini hoja zetu, polisi katika eneo hilo walitupatia ushirikiano mzuri tangu wakati tunafika mpaka tulipomaliza mkutano
huo.
11. Jioni wakati tumerudi hotelini, tukasikia kuna taarifa zinasambazaa kuwa kuna mtu/watu wamekufa katika eneo la Ndago. Habari hizo zilikuwa zinakanganya kwa sababu zilikuwa zikitaja idadi tofauti tofauti. Lakini kwa vyovyote vile kama ni kweli kuna tukio la mtu
kufariki, CHADEMA tunasikitika sana kwa tukio hilo la uhai wa mtu.
12. Tunalaani taarifa zinazozidi kusambazwa ambazo zinawataja polisi kuwa wanatuhusisha CHADEMA na tukio la mtu aliyefariki. Hii ni ajabu kubwa kwamba tumetoka kwenye mkutano ule kwa amani kabisa mpaka tumemaliza mkutano wa pili kwa amani na polisi wakiwepo sehemu zote mbili, kisha tunasingiziwa masuala ambayo wenyewe hatukuwa na habari nayo tangu mkutano wa kwanza ukiwa unaendelea mpaka mkutano wa mwisho
ulipomalizika.
13. Kutokana na habari hiyo ya kifo cha mtu inavyoenezwa kwa kuihusisha CHADEMA, tumebaini kuwepo kwa mbinu na mikakati ya chama tawala pia vyombo vya dola vikihusika kutaka kuwatisha wananchi waSingida, Watanzania wote wapenda mabadiliko na viongozi wa CHADEMA katika mkoa huu, wasifanye kazi ya kisiasa kwa kuwabambikizia tuhuma
na kesi na pia kuwafanya waonekane ni watu wa vurugu.
14. Tunapenda kusema hapa kuwa njama hizo hazitafanikiwa. Zitashindwa kama zilivyoshindwa njama zingine zote ambazo zimekuwa zikifanywa na vyombo vya dola, viongozi wa serikali na chama tawala dhidi ya CHADEMA na vuguvugu la mabadiliko nchini.
15. Tunawataarifu wananchi kuwa ratiba ya kufanya Operesheni nyingine kubwa katika Mkoa wa Singida, ikiongozwa na Katibu Mkuu, Dkt. Willibrod Slaa, itafanyika baadae kama ilivyoazimiwa na kikao cha Kamati Kuu.
Imetolewa leo Singida, Julai 15, 2012 na;
Waitara Mwita Mwikwabe
Ofisa wa Sera na Utafiti CHADEMA Makao Makuu

hivi bwana waitara,hili ni tamko ama umehadithia?? sikuelewi..hii haijakaa kama tamko..zingatia profesionalism af jipangee!
ReplyDeleteAu ndio kauli ya mh mbowe kuwa tuko tayari kuchukua nchi hata kwa kumwaga damu??
ReplyDeleteMaelezo haya hayana mfuatano linaloonekana hapa labda mwandishi anataka kueleza aliyonayo kichwani badala ya kueleza kilichotokea. Kwa kweli natatizika kwani sijaelewa kutu labda nisaidiwe.
ReplyDeleteKwa kifupi lengo la taarifa hii sidhani kama limetimia.
Hebu jaribuni kuwa serious kutoa tamko linaloeleweka kusudi wasomaji tuelewe kilichotokea jamani mnatupeleka wapi?
Nadhani hivi sasa ni muhimu kutekeleza ile sera ya jino kwa jino, yaani haiwwzekani mtu auliwe bure bure tena kwa kufukuzwa kama kuku hata baada ya kutafuta hifadhi ndani ya nyumba!
ReplyDeleteKule Arusha mona mlimchinja kada wa CDM? Wewe unayeongelea jino kwa jina hujui ndo imeshaanza hivyo. Hata hivyo si dalili nzuri kwa nchi yetu. Viongozi wana nafasi kubwa ya kuepusha mabaya zaidi kama wakitaka. Ila kwa sababu wanaangalia maslahi ya vyama, basi yetu macho na masikio.
ReplyDeleteWaitara, cheo chako kinakustahilisha kujiita 'mheshimiwa'?
ReplyDeleteHaishangazi kuona watu wengine na itakuwa ni wafuasi wa chadema waki-support vitu kama hivi, kwani hii ndio sera yao, waliahidi kuwa damu itamwagika na tutahakikisha hapatawaliki.
ReplyDeleteHuyo Waitara Mwita Mwikabe ni mtu wa musoma, kule musoma wamezoea kuuwana kama wanyama wa porini, wala kuuwa kwao sio shida ndio maana wakampa kazi yeye kwenda singida kuteleza ilani ya chama chao, ya kumwaga damu.
Na 2015 kitaeleweka tu, nina uhakika wananchi wengi tutakuwa tumeamka nani anayetaka chama chenye vurugu kama hiki? Kila kukicha niwao kutaka kuonyesha kuwa wanamisuli ya kisiasa, kwa bahati mbaya wanaanika upumbavu wao na uchu wao wa madaraka.......hivi hakuna shughuli nyingine za maendeleo ni mikutano tu ya kulaghai wananchi na maandamano yasiokuwa na tija.
Huoni hata siku moja mbunge wa Chadema yuko katika shughuli ya kuhamasisha wananchi kujenga tabia ya kujitegemea na jinsi ya kujikwamua kimaisha. Wamepewa hela na mzee sabodo kuchimba visima kwenye majimbo yao, hivi kuna mtu aliepata kuona hata kisima kimoja kikijengwa kwa shangwe? Kutwa kwenye majukwa serikali hivi serikali vile, wao wana-alternative gani? Kitu wanachotuonyesha kikubwa ni kuwa wao ni mahodari wa kuiba siri za serikali na kuzianika hadharani, basi wakiwa wao ndio serikali itakuwa kazi yao kuwachunguza wapizani na kuweka siri zao hadhari ndio ajenda tena hizo, maana sioni kabisa kazi yao ni nini.
Mimi nasema hata kama CCM haitakiwi kama wanavyofikiria wao wajue kabisa kuwa wao sio mbadala, sioni kabisa chance ya Chadema kushinda wasijisahau kuna vyama vingine pia, CUF, NCCR-Mageuzi, TLP, UDP na vinawafuasi vile vile na vinaendesha shughuli zao kama kawaida, sasa wasijone wao ni bora kwa vile kutwa wako mahakamani kwa hakika tumeshaanza kuwachoka................hamna kitu.
Hii ndiyo tatizo la kwuwa na watu wasioelewa kazi zao sasa hapa hili ndiyo tamko gani? Upumbavu mtupu yani kama unatoa ushadili vile Chama hakiwezo kutoa tamko kieneji kama hivi. Sasa watu kama hawa wakipewa uongozi watafanya nini? Hapa chadema ndiyo wanaharibu na wanaonyesha kuwa hawafai kupewa nchi hawajajiandaa. Ungwana ni vitendo watz tupendane tusiuwane
ReplyDeleteMDAU MKEREKETWA