Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili unawatangazia Madaktari wote ambao hawafiki kazini kuwa wanatakiwa kurudi kazini mara moja kwa kujiorodhesha majina yao kwa wakuu wao wa Idara.
Aidha, tangazo hili pia linawahusu Madaktari wote wanaokuja kazini lakini hawafanyi kazi, nao wajiorodheshe kwa wakuu wao wa Idara.
Wakuu wote wa Idara wanatakiwa kuwaorodhesha Madaktari wote watakaofika kazini kuanzia leo (2/Julai/2012) na kuhakikisha wanafanya kazi kwa mujibu wa sheria, kanuni, na taratibu zilizopo.
Zoezi hili litafungwa kesho tarehe 3 Julai 2012 saa tatu asubuhi.
Tangazo hili haliwahusu Madaktari walio katika Mafunzo kwa Vitendo (Interns).
Dr. Marina Njelekela,
Mkurugenzi Mtendaji
Saa 06:00 Mchana
Nakala: Wakurugenzi - Kwa usimamizi
kwa nini msiwafukuze tu maana hawataki kazi mkiwalaimisha watatuua jamani,mfano mtu anaumwa malalia anapasuliwa kichwa nk,hebu waacheni wapumzike kwanza watulize hasira zao,pia muwape hela awanazotaka kama mnazo kama hakuna tafuteni kwanza ndipo muwaite
ReplyDelete....na mkuu wangu wa idara amegoma....
ReplyDeleteSafi sana Madaktari mnatakiwa mrudi kazini na kufanya kazi, tunaiomba serikali iwafukuze kazi wale wote watakaokaidi amri hii.
ReplyDeleteSafi sana boss, wasipotii fukuza, kudadadeki...
ReplyDeleteBinafsi sioni sababu ya watumishi hawa wa umma kubembelezwa kupita kiasi, ni bora serikali iwape talaka ili wakatafute mume mwingine atakaeweza kuwatimizia haja zao zote.
ReplyDelete