Taswira hizi  zimedakwa na Globu ya Jamii jijini  London, Uingereza, ambapo wafugaji wanalalamika kuhusu kushushwa kwa bei ya maziwa. Hii imekaaje?



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 14, 2012

    Yeye kashughulika kuwapiga picha wenzake na yeye kadhalika 'anapichuliwa' bila kujijuwa.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 14, 2012

    Michuzi uk migomo ipo kila siku ila inatofauti na kwetu.Mwezi uliopita kulikuwa na mgomo wa madaktari wa masaa 24 na huduma za muhimu zilikuwa zikitolewa kwani wengine walikuwa kwenye mgomo lakini alikuwepo daktari mmoja au wawili na sio kufunga hosptali zote.
    Ni sawa kuwa na mgomo lakini inabidi pia kufikiria hali za rai wa kawaida kwani kuna watu wanaopata ajali,wanaojifungua watoto sasa mkifunga huduma zote mnaowatesa ni raia wa kawaida.Hao unaowaona michuzi waliandamana kuhusu bei ya maziwa waliyopangiwa kuwa ndogo,lakini waliendelea kusambaza maziwa kama kawaida ila ujumbe wao ulifika kwa serikali na wananchi na serikali wasikilizeni watu wanapokuwa na maombi yao na ikiwezekana mnayashughulikia.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 14, 2012

    MDAU WA PILI UMEONGEA LA MAANA NAKUPA MKONO NA KUMBATIO LA HONGERA HIZI NDIO MADA ZENYE AKILI KAMA TUTAELIMISHANA WA-TANZANIA HIVI NI VIZURI. TUIGE YA MAANA SIO UPUUZI KAMA MASTAR WETU WABONGO UNAFIKIRI WATOTO WETU WATAKUWA NA ADABU AU AKILI KILA SIKU STORI ZA KINA WEMA NA WOLPER HAYA NDIO YA KUIGWA SIO KINA RIHANNA. NA COMMENT KAMA ZA MDAU WA PILI NDIO ZA KUSOMWA. MZ

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 14, 2012

    Hiyo ingekuwa BONGO.. hao wafugaji wangekuwa tayari wapo wodi ya ICU au MOCHWARI kutokana na vipigo vya FFU.

    .. Civilazation in Tanzania!!..Safari bado ni ndefu.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 14, 2012

    NA HUYO KIKWETE WETU ALIKUWEPO HAPO HAPO KAJIONEA JINSI GANI NCHI ILIOKUWA NA DEMOCRASY INAVYOJALI IDEA NA MALALAMIKO YA JAMII, SIO KIPIGO TU KILA WAKATI KAMA IKIANDAMANA ,RAIA WA TANZANIA WANAPIGWA KAMA NYOKA KILA KUKICHA KAMA WAKIANDAMANA. NCHI SIO YA VIONGOZI TU,NA WALIOKUWA NA PESA PEKEE, HAPANA! MKULIMA , MLALA HOI, ASIEKUWA NA AJIRA, WAZEE, WATOTO, WALEMAVU, NA ELIMU, AFYA,MIUNDO MBINU, BARABARA, MAJI, UMEME, AJIRA NDIO MAMBO YA KUJADILIANA NA BUNGE LA UK NI USO KWA USO !, KIONGOZI LAZIMA ASUTWE KAMA KAKOSEA SIO KUFUKUZWA CHUMBA CHA BUNGE KAMA MTOTO WA SHULE, HIO NI TANZANIA TU NDIO HAYO MAMBO YANATENDEKA KWA RAIA WAKE

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 14, 2012

    Demokrasia ipi hiyo
    unayoizungumzia mdau na wakati kutoa mawazo yetu bado tunaogopa.
    Wengi wetu tunafikiri maendeleo ni kupanua barabara na maongezeko ya magorofa:
    GNP is still drooping,currency falling, half of the population is under 15 yrs .
    Baadhi ya viongozi wanapokuja ulaya na kundi hata kutusikiliza hawawezi, what they always keep saying is ``you guyz hav to come back `` come back??where Daktari anataka kutolewa roho na bado anashtakiwa.where Dito anaua na kushinda kesi,where Richmond case inaishia hewani.is this a democratic country??
    wanavyuo wanalalamika kila kukicha, posho za kujikimu tu hazitoshi,je watawezaje kufanya tafiti mbalimbali na kuwa washindani ktk ulimwengu huu wa kileo ? tutaendelea kuwahitaji wa china mpaka lini ? kwenye nchi yenye kila kitu wananchi tunakesha taifa kumuomba Mungu , are we serious??

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 14, 2012

    Tanzania ni (laboratory) maabara ya maisha kila mtu anafanya majaribio (research). sasa hivi tunachunguza je kama tukifukuza madaktari, hatukuwa tumetatua tatizo? Hakutakuwa na madai ya madaktari, wagonjwa wote tutakufa, viongozi watabaki kwasababu wanatibiwa nchi za nje, wataishi kwa raha, usumbufu utapungua kwao kwa kuwa hakutakuwa na wananchi wa kuwaongoza wala wakuwahoji watakapokuwa wanatafuna pesa ya nchi vile watakavyo, majengo ya mahosipitali yatabadilishwa kuwa ya starehe. mwisho itakuwa rahisi kwao kugawana mali ya nchi kwakuwa watakuwa wachache.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 14, 2012

    huko UK hakuna mabwepande?

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 14, 2012

    Na wewe unayejidai mUK,pamoja na kukaa huko umekosa busara za kuelewa siasa za hao wazungu na watanzania,hao lazima wasikilizwe na wao wanalijua hilo,madaktari hapa wanajua kwamba kama huduma zinaendelea hakuna mtu atakusikiliza.Mwezi iliopita kulikuwa na mgomo wa marubani wa shirika la ndege india,wote walifukuzwa na kuajiriwa wengine,waliofukuzwa waligoma kula na walikuwa tiyari kufa.Siasa zinatofautiana sehem na sehem,mimi nashindwa kuelewa watu wenye mawazo mgando kama wewe huoni taabu wanayoipata,wagonjwa kila siku wanaenda nje na kugundulika wanachoumwa ni tofauti na walichoandikiwa tanzania,vifaa hamna hata kama daktari anauwezo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...