Viboko walio kwenye Hifadhi ya Taifa ya Katavi Mkoani Katavi wakiwa kwenye dimbwi wakati wengine wakiwa wametoka nje kwa kuotea jua kama walivyonaswa leo na mpiga picha wetu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 11, 2012

    AHSANTE KWA PICHA HII NZURI, KWA KWELI INAVUTIA PAMOJA NA KUWA SIFAHAMU HAWA WANYAMA WANA UKALI GANI KWA WANADAMU AU WANYAMA WENGINE LAKINI WANAONEKANA WAPOLE NA WANAPENDANA. WATANZANIA TUPENDE KUWATHAMINI NA KUWATUNZA. TULETEENI NA WENGINE WA SEHEMU NYINGINE, SHUKURANI NYINGI KWA ALIYEPIGA NA KUILETA KATIKA BLOG HII.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 11, 2012

    Katavi ndio Mkoa gani, upo jirani na Mkoa gani?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 11, 2012

    Jamani kuna mtu mwenye RAMANI MPYA ya mikoa ya Tanzania Bara? Napenda kujua hii mikoa mipya iliyokuja kipindi cha Mkapa na Kikwete. Please help.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 11, 2012

    Tujitahidi ikiwezekana hawa Viboko wafungwe 'Rimoti kontrol' kuwadhibiti na kuwanusuru na Majangili ili nao wasije wakatoweka kama Faru waliopelekea sasa tunapatiwa Msaada wa mbegu ya faru watatu (3) kutokea Uingereza!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 12, 2012

    Asante mpiga picha..picha nzuri sana.Kila nikivuta kumbukumbu ya somo la picha kidato cha pili inakataa kutoka.Hii ni ground /air Oblique photo(au siyo mzee Michuzi?)..Picha uliipataje hii mkuu?Ulikuwa juu ya mti au kwenye kichuguu?au hewani.Wakorofi sana hawa wanyama ingawa wanaonekana wapole usoni

    David V

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 12, 2012

    Rukwa imegawanywa na kupatikana mkoa mwingine wa katavi

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 12, 2012

    Katavi ni mkoa mpya zamani ulikuwa ni mkoa mmoja na Rukwa, kwa sasa umepaka na mikoa ya Kigoma, Tabora, Rukwa nk.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 12, 2012

    NASIKIA NYAMA YAKE NI TAMU SANA NI KWELI JAMANI?

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 12, 2012

    katavi ipo katika mkoa wa kilimanjaro wilaya ya Vunjo mashariki.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 12, 2012

    Sio wakorofi hawa wanyama, lakini ukiwachokoza huwa wanakuwa wakali sana na wanaweza kudhuru watu hasa ndani ya maji.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...