Hi Ankal Michuzi na Timu yako,

I hope you are well.

I am writing this email because of an incident that happened to my dear friend on 6th July 2012 at Mlimani City, Dar-es-salaam.TZ.

Mtu asiemjua alimsimamisha kwa kumuita kwa jina lake Mlimani city wakati amemaliza shopping (muda wa saa mbili kasoro usiku baada ya kutoka kazini). Yule kaka akajaribu kumkumbusha matukio mbalimbali ya huko nyuma (kama mtu anayemfahamu).

 Anasema alisogea restaurant kununua maji na hilo ndio tukio la mwisho analolikumbuka. Saa saba usiku amerudishwa nyumbani kwake na gari yake akiwa bado hana fahamu. Wamemchukulia simu, hela na baadhi ya hela zimetolewa kwenye ATM machines. 

Thank God hawakudhuru kabisa. Ila kinachoogopesha ni kwamba huyu mtu alikuwa anajua historia yake (ndugu zake na marafiki zake) na anajua anapoishi. It is very disturbing.

Naomba mufahamishe ndugu na marafiki zenu kuhusu tukio hili. Ubinaadamu haupo tena kwahivyo tuwe makini tukiwa tunatembea huko mitaani...I hope this email will help others to avoid such tragedies!!

Please forward this email to your friends and families!

STYLE YA PILI

Kutoka kwa Mdau Andrew

Kuna utapeli wa aina nyingi sana hasa parking ya Mlimani City! Wenye magari kuweni makini sana! Juzi naingia kwa gari naondoka jamaa akanifuata ati anataka msaada nikamwona mapema kabisa anavyobadilisha sura ili aoenekana mhitaji msaada! 

Nikamuwahi nikafunga vioo! Nikashusha kidogo nikamhoji akadai ati anaomba japo nauli arudi gerezani! (Just imagine the way he confused himself kwani nilimchenjia ni balaa) Sasa gerezani umetorokaje, kwanza huna uniform, then umefanikiwa kutoroka bado unataka urudi, LOL!

 Nilipotafakari na kumsimulia jamaa yangu akadai ndiyo janja yao, anakuomba msaada na ukishampatia anakushukuru kwa kukupa mkono, hapo ndipo inakuwa imekula kwako kwani wana kitu cha nja kali kama kisindano kidogo wanakuchoma nacho mnapopeana mkono then from there unapoteza fahamu, na ndipo wenzake wanatokea. 

Unapakiwa kwa gari wakidai ndugu yao kazidiwa, unapelekwa kusikojulikana, wazee wanasepa na gari! BEWARE tupunguze ukarimu waTZ, wema usizidi uwezo!

tuwe makini jamani....

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 19, 2012

    Jamani Ahsanten sana kwa hizi taarifa!Mimi ngoja niwaasendie home!
    Lakini kitu nilikuwa nawaomba kwa nini msisaidie umma wote wa kitanzania habari hii kwa kutoa katika gazeti au TV pia na Redio?Ili watu wote wapate taarifa kabla hawajazurika,,hapo mtakuwa mmefanya jambo jema mno,na Mwenyezi Mungu atakulipeni ujira mkubwa mno!
    Watu wengi awaingii Internet kwa hiyo ni wachache tu watakaojuwa na kujuza wenzio
    Mwenyezi Mungu akuzidishieni,na Atuepushe na hao MAIBIRISI!,,Washindwe na walegee!!
    Walaniwe hao!
    Ahlam...London

    ReplyDelete
  2. Jamani kila kukicha wezi wanaongezeka, na siku hizi wanaiba mchana mchana.

    Huko Kipunguni-Gongolamboto, waliniibia mimi, wife aliondoka kwenda gengeni, kumbe kuna jamaa anamfuatilia akiwa kachora raketi na mwenzake aliyekwenda nyumbani, kwahiyo yule anayemfuatilia wife, akawa anamuelekeza mwezake aliyepo nyumbani, wapi wife yupo, na ili kama ataonekana kurudi nyumbani amtipu mmwenzake kuwa akimbie.
    Yule liyekuwa huko nyumbani akavunja mlango kwa kutumia pisipisi akaingia ndani na kuchukua vitu, ...na huyu anayemfuatilia wife kazi yake ni kumpa taarifa yule aliyoko nyumbani kuwa sasa basi au kama kuna hatari nyingine yoyote...
    Wife alipofika nyumbani anakuta mlangi upo wazi, na alipoingia ndani vitu vingi , na pesa hakuna....

    Sasa jamani hawa watu wakichomwa moto kuna dhambi kweli!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 19, 2012

    Well noted.Asante sana na pole kwa aliyepatwa na hiyo kashkash,hawa ni wauaji na hawana huruma.Kama haijakukuta wewe,au mtu wako wa karibu unaweza usielewe ushenzi wa hawa watu.Ni washenzi,walishamlisha ndugu yangu hizo dawa kwenye Soda ya Fanta wakamwibia kila kitu na kumtelekeza.Ni wanyama,ndiyo maana wakati mwingine sisi raia tukiwadaka tunawapa kipondo cha mbwa mwitu.

    David V

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 19, 2012

    Kuna uwezekano mkubwa watu wanaopanga na kusimamia matukio haya ya utapeli ni watu/ndugu/jamaa/marafiki au majirani zetu kabisa na wanatoa information zetu kwa watu wanaokuja kutekeleza utapeli huu. Kuna haja ya kufuatilia pia nyendo za majirani zetu, marafiki,ndugu na watu wengine tunaohisi wanaweza wakawa vyanzo vya habari zetu kama majina, sehemu tunazofanyia kazi au shughuli zinazotuingizia kipato.Haiwezekani from nowhere mtu akapata habari zako na akaweza kukufanyia unyama kama huu!!!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 19, 2012

    Ni sawa kujihadhani, tena ni jambo jema sana. Ila pengine alimaanisha Gerezani maeneo ya Kariakoo na sio jela. Yote na yote, siamini pia kuwa alikuwa muaminifu.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 19, 2012

    Asante sana mdau kwa hizi habari. Mungu akubariki!

    ReplyDelete
  7. Ancle Michuzi, mimi nimepatwa na janga la kuibiwa line yangu ya simu hivi karibuni tu, fuatana nami nikujuze yaliyojiri ilikuwa jioni ya saa 12 hivi za mtu mmoja akanipigia simu na kuniita kwa jina langu kabisa, nikajaribu kutafuta njia ya kumtambua sikuweza akaanza kutiririka na maneno akanieleza ya kwamba yeye anafanya kazi Airtel hivyo alikuwa anahitaji kujua taarifa zangu basi alipoikata ya kwake simu yang ikapoteza network usiku kucha siku iliyofuata nikelekea kinondoni Airtel kufika kule simu yangu bado ilkuwa inatumika na mtu mwingine halafu simu hiyo ilijaribu kuingilia password yangu bila mafanikio, niliona kila kitu kigumu lakini nimefanikiwa kuirudisha namba yangu na everything is under control. Nawatahadharisha jamaa wengine wasifikwe na hayo.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 19, 2012

    Hii mbona bado haijakaa sana sawa ?? yaani mtu anakuchoma na kitu chenye ncha kali,halafu unakosa fahamu,kisha wenzake wanakuja na kukusambaratisha ?????. kwanza kabisa hiyo dawa ya kukupoteza fahamu inachukua muda mrefu kukuingia kwenye system yako ya mwili,hapo tayari bado muda unao wa kujihimu aidha kukimbia au kupiga mayowe,hapo sehemu ya parking lazima na daima huwa kuna watu,kwa hiyo huyo mharifu anaweza kudhibitiwa mara moja. Mimi naondoka sasa hivi kuelekea huko M.city ninahamu sana nikutane na hawa jamaa, nitawafahamisheni.Zebedayo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...