Mbunge wa Kigoma Mjini Mh. Peter Serukamba akipokea i-pad aina ya Samsung Galaxy kutoka kwa Meneja wateja wa mikataba wa Vodacom Tanzania Bi.Melinda Siara Kamukara Bungeni Mjini Dodoma. Mh. Serukamba ni miongoni mwa Wabunge wanaotumia na kufurahia huduma za mawasiliano za Vodacom chini ya utaratibu wa malipo ya baada.
Ofisa huduma za kiufundi kwa wateja wa mikataba wa Vodacom Bw. Dia Misana akiwaelekeza waheshimiwa Wabunge Raya Khamis (Viti Maalum - Chadema) na Francis Mkosamali (Kibondo - NCCR-Mageuzi) mwenye shati jeupe ambao ni wateja wa malipo ya baada wa Vodacom Tanzania namna ya kujiunga na kufaidi huduma bora za Intaneti za Blackberry (BIS) kupitia mtandao wa Vodacom katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma.
Kutoka kulia Meneja wa Mahusiano ya nje wa Vodacom Tanzania Bw.Salum Mwalim, Melinda Siara Kamukara na Dia Misana wa kampuni ya Vodacom wakiwahudumia wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ambao ni wateja wa mkataba wa Vodacom Tanzania.Zoezi hilo limefanyika Bungeni Mjini Dodoma ikiwa sehemu ya kujali wateja wake ambapo wabunge zaidi walijiunga na huduma hiyo.
Hakuna I-pad aina ya Galaxy tablet mkuu. Ulitakiwa kusema, TABLET aina ya Samsung Galaxy.
ReplyDeleteChiggs
Brother Michu hakuna iPad ya Samsung Galaxy, hizo ni bidhaa mbili tofauti.... iPad ni bidhaa ya Apple na Galaxy ni Bidhaa ya Samsung. Tafadhali rekebisha kaka.
ReplyDeleteMdau kutoka kilwa masoko, kwa Bibi Manyau
Jamani..... msipotoshe.....!!! Huwezi kuwa na I-pad aina ya Samsung Galaxy....... I-pad is a trade mark... Samsung Galaxy ni trade mark... They are known as "tablets"... jamani lugha ! Jamani lugha....
ReplyDeleteHii kali, ipad aina ya Samsung Galaxy!.....
ReplyDeleteNimeona kitu kimoja ambacho naona mara nyingi sana katika blog mbali mbali (na hii ikiwemo) matumizi yasiyo sahihi ya lugha. Maelezo katika mojawapo ya picha yanasema ... akipokea i-Pad aina ya Samsung...
ReplyDeletei-Pad ni "brand name" ya tablet computer inayotengenezwa na Apple. Hivyo sio sahihi kuiita tablet computer ya samsung kama i-Pad.
Michuzi,
ReplyDeleteiPad aina ya Samsung??? Kwi kwi kwi; kali sana hii, sijawahi kusikia kuna iPad aina ya samsung. iPad ni bidhaa ya apple, naona lugha hapa gongana kabisa. Hizi ni tablet computers, sema naona jina la iPad limetawala sana ila hii ni brand name, wasichanganye hao. Nadhani wanauza bidhaa bila ya kuwa na maelezo sahihi ya nini wanachokiuza. Ndo tunajifunza mumo humo lakini.
Na we mzee wa libeneke nunua iPad ya Nokia basi. Kwe kwe
Power of a brand...iPad =TABLETS, Kazi ya Steve Jobs RIP ni nzuri.jamaa was a genius.chairmannwb@gmail.com.HUREEE TO APPLE
ReplyDelete