Afisa elimu wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni,Bibi Lucina Shayo akifafanua jambo ndani ya ukumbi wa Mila.
Uongozi wa RAAWU tawi la Makumbusho ya taifa, ujiutembeza uongozi wa RAAWU taifa kujionea mazingira ya kazi ya Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam.
Mwenyekiti kamati ya wanawake RAAWU taifa Bibi Radhmina R. Mbilinyi akiongea na wafanyakazi wa Makumbusho ya Taifa.
Katibu wa RAAWU kanda ya Mashariki Bw Joseph Sayo akiongea na wanachama wa chama hicho cha wafanyakazi Makumbusho ya Taifa.
Baadhi ya wajumbe wa RAAWU tawi la Makumbusho ya Taifa, wakiusikiliza kwa makini uongozi wa RAAWU taifa.
Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu,Sayansi,Teknolojia,Habari na Utafiti (RAAWU) nchini wametakiwa kuzisoma sheria na kanuni za kazi ili kuzijua haki zao za kikazi wawapo kazini ili kuepuka unyanyasaji unao fanywa na waajiri wasio fuata tararibu,wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa RAAWU wanawake taifa alipo kutana na wanachama wa chama hicho cha wafanyakazi tawi la Makumbusho ya Taifa Nchini katika ukumbi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam.
Akijibu moja ya swali lililoulizwa na mmoja wa wafanyakazi wa Makumbusho Tanzania lililouza nini kifanyike pale uongozi wa juu unapo wanyima haki zao za kupata likizo pamoja na malipo stahili waendapo likizo,kiongozi huyo wa RAAWU Taifa alieleza kuwa wafanyakazi wengi wananyanyaswa kutokana na kutokuwa na ufahamu juu ya haki zao za msingi,hali inayo sababishwa na kutozielewa sheria za kazi, pia aliwataka kuacha uwoga na kukitumia chama chao vyema katika kutoa malalamiko yao pale wakuu wa taasisi wanapo shindwa kuwatimizia haki zao zamsingi ili RAAWU ichukue hatua zinazo stahili kabla tatizo halija kuwa kubwa.
Nae katibu wa RAAWU kanda ya Mashariki, Bw Joseph Sayo, aliwataka viongozi uongozi wote nchini kuacha kukichokoza chama hiki kwa kuto watendea haki waajiriwa ili kuipunguzia ama kuiondolea serikali migogoro isiyo na tija na wafanyakazi wake, alisema kuwa RAAWU aitokuwa tayari kumvumilia kiongozi yeyote wa aina hiyo na itachukuwa hatua zinazo stahili kwa viongozi wowote watakao bainika ili kuwajengea mazingira bora ya kazi wanachama wake hapa nchini.
Akizungumza na muandishi wa habari hizi baada ya mkutano huo, katibu wa RAAWU tawi la Makumbusho ya Taifa nchini, Bw Amini Ndossa aliushukuru uongozi wa RAAWU taifa kufanya ziara katika tawilao kwani mkutano huo umeweza kuwapa ufahamu wanachama juu ya taratibu wanazo paswa kuzifuata pale wanapo zulumiwa haki zao mahala pakazi na pia kuwatoa uwoga wanachama hao wa kudai haki zao pale wanapo ona uongozi wa mamlaka husika imeshindwa kufanya hivyo.
Uongozi wa RAAWU taifa upo mkoa wa Dar es Salaam kwa ziara katika matawi mawili kati ya matawi yake yaliyopo jijini hapa kwa lengo la kuimarisha uhai wa chama na kusikiliza kero mbali mbali zinazo wapata wanachama wake mahali pakazi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...