Wajasiriamali Kumi na Moja wa Kikundi cha HANDCRAFTS OF TANZANIA HOT) wakiwa mjini Ndola nchini Zambia, walishiriki Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa nchinihumo. Maonesho haya yalianza tarehe 27 Juni 2012 na yanategemea kumalizika tarehe 03 Julai 2012.

Pichani ni  wajasiriamali wetu katika picha ya pamoja na Mhe. Grace J. Mujuma, Balozi wa Tanzania nchini Zambia.Katika Maonesho haya Kikundi cha HOT kiliweza kujinyakulia ushindi wa Tatu katika kundi la Washiriki wa Kimataifa ikitanguliwa na Kenya ambayo ilikuwa ya Kwanza na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ya Pili. 

Kikundi hiki kilikabidhiwa Kikombe na Mhe. Mhe. Michael Chilufya Sata, Rais wa Jamhuri ya Zambia siku ya Jumamosi tarehe 30 Juni 2012, wakati wa ufunguzi rasmi wa maonesho. 
Ubalozi wa Tanzania nchini Zambia unatoa 
PONGEZI NYINGI KWA KIKUNDI HICHO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...