Askari wa Tanapa ( kushoto)na wenzao wa Polisi wakila kiapo cha utii kwa amiri jeshi mkuu na taifa baada ya askari wa Tanapa kuhitimu mafunzo ya miezi minne
BENDI YA JKT IKITUMBUIZA
Askari wa Idara ya Wanyamapori wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania ( TANAPA) wakiongozwa na Ofisa wa Polisi , wakipita mbele ya Mgeni rasmi , Mkuu wa Mafunzo wa Jeshi la Polisi nchini, SACP, Elice Mapunda ( hayupo pichani) wakati wa kufunga mafunzo ya miezi minne Juni 29, mwaka huu katika Chuo cha Polisi Kidatu, Wilayani Kilombero, Mkoani Morogoro ikiwa ni hatua ya ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi na Tanapa wa kukabiliana na uharifu wa ujangili nchini.
Askari wa Idara ya Wanyamapori wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania ( TANAPA) ,Prisca Elisia akipokea zawadi ya kufanya vizuri katika mafunzo kutoka kwa Mgeni rasmi , Mkuu wa Mafunzo wa Jeshi la Polisi nchini, SACP, Elice Mapunda ( wapili kutoka kushoto) aliyefunga mafunzo ya miezi minne Juni 29, mwaka huu katika Chuo cha Polisi Kidatu, Wilayani Kilombero, Mkoani Morogoro ikiwa ni hatua ya ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi na Tanapa wa kukabiliana na uharifu wa ujangili nchini.
Askari wa Idara ya Wanyamapori wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania ( TANAPA) wakiongozwa na Askari Polisi kutoka Kikosi cha FFU , wakipita mbele ya Mgeni rasmi , Mkuu wa Mafunzo wa Jeshi la Polisi nchini, SACP, Elice Mapunda ( hayupo pichani) kwa ajili ya kuonesha mazoezi ya kupambana na adui baada ya kuishiwa baada ya wote kuishiwa risasi ‘ mapigano ya singe’ wakati wa kufunga mafunzo ya miezi minne Juni 29, mwaka huu katika Chuo cha Polisi Kidatu, Wilayani Kilombero, Mkoani Morogoro ikiwa ni hatua ya ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi na Tanapa wa kukabiliana na uharifu wa ujangili nchini.
Mazoezi ya kushambulia adui kwa singe.
Picha zote na John Nditi wa Globu ya Jamii, Morogoro
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...