Uchumi unaofuata sheria za kiIslam unakaribishwa nchini Ireland amesema waziri wa mambo ya jamii wa Ireland Miss Joan Burton (pichani). Waziri ameyasema hayo kwenye mkutano wa kimataifa unaohusu masuala ya uchumi na ujasirimali unaofuata sheria za kiIslam ulioandaliwa na Irish Business Executice Forum (IBEF). Waziri huyo alinukulia akisema ‘Serikali imeweka misingi itakayoziwezesha uchumi unaofuata sheria za kiIslam zikiwemo benki za kiIslam kutambulika.

Aliongeza kwamba tunafahamu kwamba kazi kubwa bado inatakiwa ifanyike hususan ktk nchi ambayo kuna changamoto nyingi za kiuchumi. Tuna sheria nyingi zinazohusiana na swala zima la uchumi wa kiIslam na kuna yale maswala yanayohusiana na sheria za kiuchumi za benki kuu ya Ireland. Waziri amesisitiza kwamba kuna sheria ambazo zitabidi ziongezwe ktk wakati wa baadae ili taasisi za kiislam ziweze kufanya kazi zake kwa ufanisi. Waziri mwengine wa Ireland Mr Tom Woods amefafanua kwamba uchumi wa kiIslam ni moja kati ya area inayokua sana ktk soko la kiuchumi duniani na serikali yake imeahidi kufanya kila linalowezekana kwa ajili ya kuindeleza sector hiyo nchini Ireland. Akilielezea hilo kwa ufasaha zaidi alikumbusha kwamba mwaka 2008 kulianzishwa timu maalum nchini Ireland ambayo imebobea ktk maswala ya uchumi wa kiIslam kwa ajili ya kulishughulikia swala hilo.

Dr. sheikh shaheed Sataedien President of Muslim council of Ireland na (IBEF) aliuliza baadhi ya maswali kam vile je inawezekana uchumi kukua na wakati huohuo tukaendela kuhifadhi mazingira, vipi serikali zinaweza kuongeza kipato inachokihitaji kwa ajili ya huduma za afya, jamii, na nyenginezo, nini hasa serikali inatakiwa ifanye ktk uchumi wan chi, je tutakuwa ktk hali nzuri zaidi kimaisha kama kodi zikipunguzwa na maswali mengine mengi. Kwa maelezo zaidi kuhusu benki zinazofuata sheria za kiIslam ingia www.ijuebankyakiislam@blogspot.com


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 17, 2012

    alhamdullilah!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 17, 2012

    Hayo ni maendeleo mazuri tunashukuru

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 17, 2012

    Nilipozuru Ireland 2007, nilikwenda kuswali katika msikiti wa ijumaa wa Dublin ijumaa moja. Nilishangaa kuona jinsi Wa-Irish wengi walivyosilimu. Nilibahatika kuongea na wachache baad ya swala ya ijumaa. Hao waliniambia kuwa "they have been looking for meaning in life" na hicho ndicho kilichowapelekea kusilimu. Aidha, katika Waislamu wa USA, kwa sasa Wamarekani weupe Waislamu wamewazidi idadi Waislamu weusi wa USA, tofauti na miaka ya 1960's. Hii inaonyesha kuwa wenzetu wa nchi za magharibi wako wazi zaidi (more open)katika suala la kutafuta ukweli kuliko sisi Waafrika ambao tuna tendency ya kuacha chuki ifunike rationale yetu.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 17, 2012

    Msingi mkubwa ktk Mfumo wa Fedha na Uchumi wa Kiislamu unaotakiwa kuzingatiwa na Mifumo ya Riba ni:

    1.Kuondoa RIBA (100%) au angalau kuipunguza kama alivyoishauri nchi ya Uingereza Mkurugenzi Mkuu wa IMF Madame Christine La Garde.

    2.Kuwa wazi kwa Uendeshaji,ushirikishwaji na haki (Transparence,involvement and Fair)
    Mfano ktk mfumo wa Kiislamu Benki inashirikiana na Mteja hatua hadi hatua badala ya kumwachia mzigo peke yake na wao kungoja gawio la riba wakati wa marejesho ya Mkopo.

    3.Mzigo wa hatma ya biashara au dhamana (Uncertainity and guarantee) kubebwa ba pande zote Mkopaji(Mteja) na Mkopeshaji(Benki),,,WAKATI KTK MIFUMO YA RIBA MKOPAJI NDIO MWENYE KUUBEBA MSALABA WA DENI NA HATMA ENDAPO MAMBO YATAENDA MRAMA.

    4.Mifumo ya RIBA ijifunze ya kuwa kuendesha biashara kupata faida na kuimairika biashara hakutegemei kiwango cha Riba kinachotozwa kama inavyothibitishwa na Mfumo wa Kiislamu unaoimarika bila kutumia Riba ikizingatiwa No. 1 hadi No. 3 hapo juu.

    ReplyDelete
  5. Agathon MbundaJuly 17, 2012

    Mimi naitwa Agathon Mbunda. Dini ni mkristo. Je ninaweza kufungua account ya Kiislamu? Au account hizi ni exclusive kwa watu wa dini ya Kiislamu? Kama ndivyo, je inanibidi nisilimu ili niweze kufungua account ya kiislamu?

    Nitashukuru kwa majibu ya uhakika.

    Amani ya Bwana iwe nanyi!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 17, 2012

    Ndugu Mbunda Uislam hauna ubaguzi katika mambo yake Mtu yoyote anaweza kufungua a/c bila kujali dini yake hutolazimishwa kusilimu au kuingia msikitini.baki na imani yako.Ila watatokea watakao kwambia unaanza kuvutwa na majini ya waisilamu kwahiyo akili kichwani kwako.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 17, 2012

    si silama kusilimu

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 17, 2012

    Ukweli unazidi kufichuka kuhusu mfumo mzuri wa Uchumi,kama alivyosema Rais wa zamani wa Ufaransa Nicolas Sarkozy kwamba ili"kuondokana na tatizo la uchumi duniani tutumie mfumo wa kiuchumi Kiislam usiokuwa na Riba",ambapo ktk biashara faida na hasara zinachangiwa sawa na pande zote mbili.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 18, 2012

    Ndugu Agathon Mbunda,

    Upo huru kutumia Mfumo wa Kifedha na Kiuchumi wa Kiislamu huku ukiwa u Mkristo, pia achana na fikra finyu za Mdau mmoja hapo juu Anonymous wa Tue Jul 17, 07:34:00 PM 2012 anaesema ...''si salama kusilimu''

    Uhuru wa ki Imani na matashi binafsi vinazingatiwa sana ktk Dini ya Uislamu na mara zote Uislamu unapendelea mtu aingie katika Dini ya Kiislamu kwa Imani na ridhaa yake mwenyewe na sio kwa kushinikizwa,kuhimizwa au kwa kutishwa kwa kuwa kama itatokea hivyo Imani itakuwa sio thabiti.

    Hivyo faida za kutumia Mfumo wa Kibenki na Kifedha za Misingi ya Kiislamu vipo kwa watu wa Imani zote hata wale wasio na Dini kabisa kwa sababu HIZI KANUNI ZINALETWA KWETU NA MWENYEZI MUNGU KWA WATU WOTE.

    Kama unavyoona nchi zilizokuwa na Makao Makuu ya Ukristo kama Uingereza,Ufaransa,Italia, Ujerumani, Ireland zimeruhusu Mfumo huu utumike nchini mwao.

    Hata Mashirikisho makuu ya Kidunia kama IMF,World Bank,UN na mengineyo yanerihdia Mfumo wa Kiuchumi na Kifedha wa Misingi ya Kiislamu na kuthibitisha ndio inayolenga kutatua matatizo ya kiuchumi Duniani na kuondoa kiwango cha Umasikini kwa mafanikio makubwa!

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 18, 2012

    Wakristo Wakorofi wachache 'Vibwetere wa hapa Tanzania' ninyi mnaujua Ukristo zaidi ya Ufaransa,Ujerumani,Ireland,Italia,Marekani na Uingereza?

    Wakristo Wakorofi wachache wasio waelewa wa hapa Bongo mnaweza kupingana na Uislamu zaidi ya Israel?

    Wewe Anonymous wa Tue Jul 17, 07:34:00 PM 2012 ...''si salama kusilimu'' na Anonymous wa Tue Jul 17, 08:44:00 PM 2012...''dah''::::

    Tazameni hao Wajanja wenu Uingereza, Ujerumani,Italia, Ufaransa,Israel na Marekani ziliko UN,World Bank na IMF kwa wenye akili sana zimekubaliana na Mfumo wa Kiuchumi na Kifedha wa Kiislamu itakuwa ninyi Vibwetere???

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 18, 2012

    Chezea Uislamu weye?

    Ninyi anonymous wa Tue Jul 17, 07:34:00 PM 2012 ...''si salama kusilimu'' na Anonymous wa Tue Jul 17, 08:44:00 PM 2012...''dah''

    Ebo!, mnaguna nini sasa hapa?

    Ninyi wajinga wawili hapo juu, achilia mbali huko Majuu hapa hapa nchini Tanzania Wakurugenzi wengi wa Mabenki ni Wakristo wenzenu na wasomi zaidi na Wakristo zaidi kuliko ninyi mabwege wawili wanaelewa wazi ya kuwa MISINGI YA KIFEDHA YA KIISLAMU KTK BENKI NI ZAIDI YA KILA KITU!

    Itakuwa ninyi Wakristo wawili wajinga wenye akili finyu ambao hata hamjatahiriwa?

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 18, 2012

    Chezea Uislamu weye?

    Enyi Anonymous wa Tue Jul 17, 07:34:00 PM 2012...''si salama kusilimu'' na Anonymous wa Tue Jul 17, 08:44:00 PM 2012...''dah''

    Angalieni huko Majuu ni mbali hapa hapa Tanzania Wakurugenzi wakuu wa Mabenki wengi ni Wakristo wenzenu, Wasomi na Wakristo wazuri zaidi yenu ninyi Mabwege wawili hapo juu, Wakurugenzi wa Mabenki hapa nchini wanaelewa wazi Mfumo wa Kibenki wa Kiislamu ulivyo na manufaa,

    Itakuwa ninyi Wakristo wawili wajinga ambao 'hamjatahiriwa' mnaobisha hapa?

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 18, 2012

    Kutekeleza Mfumo wa Fedha wa Kiislamu:

    Tatizo kubwa linatokana na mtazamo potofu juu ya Uislamu unaoletwa na watu wachache wanaoitumia Dini kwa malengo binafsi mfano Magaidi.

    Mfumo wa Kifedha wa Kiislamu ukitumiwa na asiye Mwislamu haimaanishi ya kuwa mtu huyo ameingia ktk Uislamu kwa kuwa kuingia ktk Uislamu kunatakiwa na vigezo vya makusudio kwa Shahada na ridhaa binafsi!

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 18, 2012

    Tue Jul 17, 07:34:00 PM 2012 ''si salama kusilimu''

    Mas Kila,,,Tue Jul 17, 08:44:00 PM 2012 ''dah''

    Wakristo wawili nyie wakorofi mkakate (mazo...{6}...a) yenu halafu mbaki kwenye Imani yenu ndio mkatae Misingi ya Benki ya Kiisilamu!

    Hata kama mktitaka hakatazwi ,mnalazimishwa?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...