· Mkurugenzi Mkuu wa Chemi cotex Industries Bw. Lakshmi Narayan Rathi akitoa kombe kwa washindi wa Whitedent School quiz 2012 kwa Shule ya Pendo English Medium school jijini Mwanza leo
Washindi wakitambulishwa huku wakishangilia
· Mkurugenzi Mkuu wa Chemi Cotex industries Bw. Lakshmi Narayan Rathi akikabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni moja kwa washindi Pendo English Medium School.
Chemi & Cotex industries Ltd, watengenezaji wa watunga ya dawa za meno za Whitedent na bidhaa nyingine za usafi wa kinywa ya leo ina furaha kutangaza fainali ya Whitedent shule squiz 2012.
Washindi wa squiz hii mwaka huu ni Pendo English Medium kutoka Mwanza, ambayo ilichukua kombe la whitedent Squiz mara baada ya kuwabwaga Shule ya Msingi Yombo Vituka Dar es sallam katika fainali hizo.
Timu hiyo ilijishindia kompyuta 9, printer pamoja, vocha za shilingi milioni 1 milioni kwa ajili ya kununua vitabu vya shule, baiskeli kwa ajili ya wanafunzi walioshiriki mbali na vocha zenye thamani ya shilingi 200,000 kwa ajili ya kununua vitabu, Shule ilipatiwa kompyuta 4, printer 1 na vocha za manunuzi za shilingi 400,000 kwa ajili ya kununua vitabu na saa, Vocha ya 100,000 kwa ajili ya kununua vitabu kwa wanafunzi walioshiriki.
Zawadi nyingine walizopewa wale walioingia katika hatua ya nusu fainali na robo ni kompyuta, taa za nishati ya jua, mipira, dawa za meno, miswaki mbali na T-shirt na kujishindia vyeti vyote hivi vikiwa na thamani ya shilingi milioni 30.
Hotuba ya kuhitimisha kutoka Chemi & Cotex kwa wanafunzi mjini Mwanza iliwapongeza wanafunzi wote na shule zilizoshinda kwa ushirikiano wao wa hali na mali katika mashindano hayo na kwa umma pia ikiwa ni pamoja na ziara hasa katika vituo vya mayatima, Dar na Arusha .
Shindano hili lilihusisha wanafunzi wa darasa la sita wenye umri kati ya miaka 12-13 kwa kuzingatia jinsiaili kuweza kukabialiana na changamoto na wote walipewa zawadi mbalimbali.
Zaidi ya hapo shindano hili lilishirikisha zaidi shughuli za kijamii ambapo washiriki waliofanikiwa kuingia hatua ya robo fainali na nusu fainali walipata fursa ya kutembelea vituo vya yatima kujua maendeleo yao kielimu zaidi na pia kuwapatia zawadi mbalimbali kutoka Chemi & Cotex. Tunayo furaha kubwa kutangaza kuwa chemsha bongo mashulen i imehitimishwa rasmi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...