Mtuhumiwa wa wizi wa umeme,Bi Siwamini Muhammed akitoa maelezo kwa wakagazu wa umeme na askari kabla hawajamchukua na kwendanae kituo cha polisi Kilwa Road.
Mtuhumiwa wa wizi wa umeme Siwamini Muhammed, akiwa chini ya Ulinzi wa jeshi la polisi na wakaguzi wa Shirika la umeme Tanesco baada ya nyumba yake ilioko Mbagala kizuiani kukutwa ikiwa imeunganishwa umeme kwa njia ya wizi kabla haujafika kwenye mita nakuutumia bila kuulipia.
Askari akitimiza wajibu wake wa kuwalinda watuhumiwa wa wizi wa umeme waliomo ndani ya gari kabla ya kuwapeleka kituoni.

WATU saba wanashikiliwa na jeshi la Polisi kwa tuhuma za wizi wa umeme baada ya kuwakamata kwenye operesheni ya kukamata watu wanaoiba umeme inayoendelea kwenye kanda maalum ya Tanesco Temeke.

Kwenye zoezi hilo ambalo linafanywa na timu maalum ya Tanesco na kusaidiana na Jeshi la Polisi kumegundulika wizi wa aina mbalimbaliikiwemo wakujiunganishia umeme kwa kupitisha waya chini ya aridhi na kujiunganishia kabla haujafika kwenye mita na kusomwa.

Zoezi hilo ambalo leo ilikuwa ni zamu ya eneo la Mbagala Kizuiani liliwapa wakati mgumu wakaguzi wa mifumo ya umeme wa shirika hilo baada ya kufika mtaa wa CCM eneo hilo la kiuzuiani na kukuta nyumba zaidi ya 6 wakitumia umeme kutoka kwenye nyumba moja huku wakiwa wamejiunganishia kwa kuchumbia nyaya chini ya aridhi na wakaguzi hao kuamua kukata kabisa waya zake na kuwashikilia watuhumiwa wa wizi huo.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo Meneja wakanda hiyo ya Temeke Richard Malaamia, amesema tatizo la wizi nikubwa kwahiyo wanalazimika kufanya zoezi hilo kuwa endelevu hadi wananchi watakapojenga mazoea kutumia umeme kwa kufuata utaratibu.

Malamia amesema wisi wa umeme uekua ukisababisha hasara ya Tsh 89Millioni kwa mwezi na kulikosesha mapato shirika hilo.

Hata hivyo wakaguzi wa mifumo ya umeme walimweleza mwandishi wa habari hizi kuwa wao binafsi walidhani tatizo la wizi wa umeme lipo zaidi kwa watumiaji wakubwa lakini kkutokana na matukio wanayoshuhudia inawapa wasiwasi kuwa kuna idadi kubwa zaidi ya watu wanao iba umeme hata kwa watumiaji wadogo kabisa.

Mkaguzi Daniel Maswi alisema, tabia ya kujiunganishia umeme kabla ya kufika kwenye mita ni hatari na inaweza kusababisha hatari hata ya kulipua nyumba kwani nyaya zinazo tumika ni hafifu mno na umeme unaopita ni mkubwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 13, 2012

    Nchi za watu askari mwanaume hawezi kumkamata mwanamke bila kuwa na askari wa kike,je bongo inaelezekaje askari mwanaume kukamata mtuhumiwa wa kike?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 13, 2012

    mnawakamata wanyonge tu , kuna wahindi matajiri hapa dar na mnawajuwa wanaiba kila leo ila hawakamatwi na wanalindwa

    mtu maskini kama huyu ndio mnamkamata

    kweli mtanzania kichwa cha mwandawazimu

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 13, 2012

    Ni wakati muafaka kila wizara ianze kusimamia sheria ili wananchi wazoee ingawa ni chungu

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 13, 2012

    Askari wa kiume anaweza kumkamata mwanamke ila katika kumfanyia ukaguzi mfano mwilini ndo haruhusiwi.
    S.26. Whenever it is necessary to cause a woman to be searched, the
    search shall be made by another woman with strict regard to decency. (Criminal Procedure Act of Tanzania 1985 R.E.2002)

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 14, 2012

    Jamani huu ujanja BONGO ni wa leo msitake kuonyesha vitendo kwa wanyonge kuonyesha mnawajibika kwa sababu uchaguzi unakaribia kichefuchefu

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 14, 2012

    Mmegundua wizi wa umeme wa simu je?Watu wanalamba saaaana tu TTCL BILI ZINAENDA KWA MASHIRIKA YA UMMA, MAWIZARA, NA HATA WATU BINAFSI WANAUMIZWA SANA TU.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 14, 2012

    Jaji kwa kweli huyu mama na wengine usishughulike nae, na wale wa Jamaa waliokatizia pesa za Rais imekuwaje, hata mwela hawajui, ila hawa wadogodogoo ndio wakutiwa ndani...........mama hakuwa na cha kuwapa hata buku ingetosha.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 14, 2012

    Jamani kama mtu ni mhalifu acheni sheria ichukue mkondo wake. Mkimtetea kwamba eti ni mnyonge asikamatwe huo hautakuwa utawala wa sheria. Jambo la msingi ni kushinikiza hao mnaowaita matajiri nao watafutwe, wakamatwe kisha wachukuliwe hatua. Pia mimi nina shida na watumishi wa TANESCO ambao wanapewa umeme bure. Hii ni kuongezea gharama wateja kwani bili zao inabidi tugawane sisi. Hii si haki kabisa. Hivi vijiupendeleo visivyo vya kawaida kwa baadhi ya watumishi ndivyo vinaleta hasira kwa watumishi wa sekta zingine ambao wanaona kama hawatendewi haki mfano madaktari na waalimu wa vyuo vikuu. HAKIIIIIIIIIIIIIII?...... SAWA KWA WOTE.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 14, 2012

    Yule mzungu wa Maeneo ya moshi baa mbona hamumkamati? yeye anatumia umeme wa wizi tangu 2004. au kwa kuwa ni mzungu? mnaishia kukamata watu maskini tu. AMA KWELI DUNIA YOTE IMETAWALIWA NA SHETANI

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 14, 2012

    ..ONEA BUZI..GOMBE OGOPA eeh!!

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 14, 2012

    Safi sana mdau wa Fri Jul 13, 11:46:00 PM 2012 kwa jibu lililosimama dede.
    Watu wanaiba umeme sababu umeme ni anasa kwa nchi yetu, gharama za kuupata ni kubwa mno na taratibu zake ni za muda mrefu mfano mimi nilitaka tu kubadirisha mita toka conversion kwenda LUKU huu sasa ni mwezi wa 10 kila nikiulizia naambiwa mita hakuna,pia na zile za kila siku zipo juu sana ndo maana watu wanashawishika kuiba. Sababu kubwa hapa ni kwa serikali kupuuzia suala la umeme na kuacha watu wachache wajinufaishe kupitia mgongo wa zabuni ambao umesababisha shilika hili kuelemewa na mikataba yenye gharama kubwa matokeo yake shirika linakosa fedha za kujiendesha. Ifike wakati kila mtu ajaribu kutii sheria na taratibu kuanzia mteja, mfanyakazi wa Tanesco na menejimenti yao pamoja na serikali ili kuweza kufanya gharama za umeme ziendane na maisha halisi ya mtanzania. Japo ni kweli nishati ni gharama lakini tuna uwezo wa kuzipunguza ziendane na uhalisia wa mazingira yetu kwani tatizo kwetu ni teknologia tu hapa resources zote tunazo hapahapa nchini.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 14, 2012

    wacha wakamatwe. Mwizi ni mwizi, si mwafrika si mhindi, madhali amegundulika atakamatwe. Nyie endeleeni na ubaguzi wenu. Tunasubiri hiyo serikali yenu ikija kama wahindi hamjawaona wanaondoka polepole na hivyo wameshawashtukia wameshakaa on your mark, get ready to go.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 14, 2012

    bora waondoke kwani umesikia hii inchi ni yao, warabu waende oman na waindi waende kwao india, hakuna watu wabaguzi na wezi kama hao. mbaya zaidi wanaiba mabillioni ya fedha alafu wanapeleka india au huko uk ambapo wengi wao wanamajumba huu sio ubaguzi hii ni reality.. kwanza mtu mweusi hawezi kuwa mbaguzi na hilo neno racist au mbaguzi miminilikuwa hata silifahamu mpaka pale nilipokutana na hawa watu tofauti ndipo nikajifunza hilo neno.. anyway mada ipo pale pale ni vyema wanavyo fanya na itakuwa vyema kama idara zote za serekali itafanya hivyo kisha utaona wahindi na warabu wangapi watakimbia hii inchi..

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 14, 2012

    Xenophobic comments from anonymous wa Sat Jul 14, 07:02:00 PM 2012!
    Katika Dunia ya leo ya Globalisation haya mambo yanapigwa vita sana. Pia kumbuka rasist ni rasist bila kuzingatia rangi yake.
    Hapa hoja nadhani tujadili kuhusu uwajibikaji maana sheria tunazo nzuri tu na pia tuna mifumo mizuri tu vichwani mwetu na vitabuni tatizo ni uwajibikaji na uzalendo.
    Hao wahindi unaosema wezi wanafanya hivyo kushirikiana na ndugu zetu wenyewe, pia na kutofuata taratibu na sheria zetu ndo kunapopelekea watu kuiba umeme kama hivyo, wakubwa pia kuliibia shirika la Tanesco pesa zake sababu hizo hizo.
    Sasa tunafanyaje mimina wewe kuondoa hili tatizo je ni kwa kuuana kama walivyotaka kufanya kwa Dr.Uli? au kwa kupeana sumu kama ilivyokua kwa kina Mwandosya na Mwakyembe? au tunafanyaje ili haya mambo ya kukamata mama zetu kwa ajili ya kudokoa punje ya mchele kwenye kontena la futi 40 la mchele ?

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 14, 2012

    msishadadie na kujifanya kumtetea huyo mwizi kwani umeme unaoibwa ni mwingi sana unaweza kulingana na unaolipiwa. Hivyo wizi ukidhibitiwa matumizi yatashuka na watu wengi watapata umeme na TANESSCO watapata fedha na gharama zitapungua. Mimi hata kama ni ndugu yangu ameiba nitamripoti kwani anasababisha mimi namlipia kwa matumizi yake ya anasa ya umeme.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...