Sehemu ya  Wanaharakati wa amsha amsha ya tamasha la Serengeti Fiesta 2012 wakiwa wamepozi mapema leo mchana mjini Moshi,mara baada ya kumaliza awamu yao ya kwanza ya kuruka hewani na amsha amsha ya tamasha hilo kwa wakazi wa mji wa Moshi,kutoka kulia pichani  ni Bonge,Eric Kusaga,Simon Malenga sambamba na Millard Ayote wote kutoka Clouds FM.Tamasha la Serengeti Fiesta ndani ya Moshi linatarajiwa kurindima ijumaa hii ndani ya Chuo cha Ushirika,ambapo kiingilio kimepangwa kuwa ni sh 5000 tu kwa kila mmoja,kama vile haitoshi kutakuwepo  na wasanii lukuki wa bongofleva akiwemo na aliyeshiriki shindano la Big Brother Stargame,CMB Prezzoo.
Mtangazaji wa kipindi cha Amplifaya kutoka Clouds FM akizungumza na mmoja wa mashabiki wa kituo hicho cha redio,mapema leo mtaa wa Ghala mjini Moshi,ikiwa ni sehemu ya mchakato mzima wa amsha amsha ya tamasha kubwa la Serengeti Fiesta,ambalo linatarajiwa kufanyika mjini humo siku ya ijumaa katika chuo cha ushirika.wasanii watakao shiriki kadhaa ni Joh Makini,Mwana FA,Linah,Godzilla,Juma Nature,Ommy Dimpoz,Bob Junior,Sheta,Ferooz,Richard Mavoko,washindi wa Supa Nyota na wengineo kibao.
Washkaji nao hawataki kupitwa kabisa na shughuli nzima ya mambo yanayoshushwa na Clouds FM,hapa walikuwa wakisikiliza kipindi cha amsha amsha ya tamasha la Serengeti Fiesta 2012 lililokuwa likirushwa live hewani ndani ya mji wa Moshi mapema leo mtaa wa Ghala.Picha zaidi Bofya hapa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...