Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Mhe. John Cheyo, ambaye ni mbunge wa Bariadi Mashariki, akiwa Addis Ababa, Ethiopia kwa ajili ya kikao cha siku 2 cha Kamati ya Utendaji ya Eastern Africa Association of Public Accounts Committees (EAAPAC) kama Mweka Hazina wa Jumuiya hiyo, alipata pia fursa ya kutembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Ethiopia na kukutana na Mhe. Balozi, Prof. Joram M Biswaro ambaye alimuarifu Mhe. John Cheyo (MB) kuhusu changamoto zinazoukabili Ubalozi pamoja na juhudi zilizokwishafanyika kukabili changamoto hizo.
Katika ziara ya hiyo kwenye Ubalozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Mhe. John Cheyo aliupongeza Ubalozi kwa kujenga jengo zuri la ubalozi lenye ghorofa tatu na kusisitiza kuhusu umuhimu wa kusimamia na kutunza mali zote za Serikali zilizopo kwenye balozi zetu kama Sheria za Usimamizi wa Mali na Fedha za Serikali zinavyoelekeza na kuongeza juhudi za Serikali kuwajengea nyumba za kuishi watumishi katika balozi zetu ili kupunguza gharama za kuwapangishia nyumba ambazo huwa ni kubwa zaidi. Aidha, aliusisitizia ubalozi kuboresha mahusiano na ushirikiano na Serikali ya Ethiopia kwa lengo la kuwarahisi watanzania wanaokuja Ethiopia wasipate matatizo katika kuingia na kutoka nchini Ethiopia.
![]() |
Mhe.John Cheyo (MB) akionyeshwa jengo la Ubalozi wa Tanzania lililopo Addis Ababa, Ethiopia. Picha na Mathew Kileo wa Ofisi ya Bunge. |
Ubalozi umechoka sana. Fanyeni ukarabati basi.
ReplyDeleteSubiri huko huko utuwakilishe kwenye maziko ya Zenawi ili Mh. apumzike kidogo
ReplyDeleteHivi Profesa mzima badala ya kuwa unamwaga ' material'class ili kuelimisha jamii unakwenda kulaza elimu yote hiyo ubalozini? tubadilike wajameni
ReplyDelete