Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Yohana Sefue (aliyeketi katikati) akiandika baadhi ya maswali aliyoulizwa na Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI wakati alipozungumza nao jana mjini Dodoma. Aliyeketi kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu wa TAMISEMI Bwana Jumanne Sagini na kulia ni Mkurugenzi wa Utawala wa Ofisi hiyo Bwana Victor Kategere.
 Baadhi ya Watendaji Wakuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI wakimsikiliza Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Yohana Sefue (hayupo pichani) wakati alipofanya ziara ya kuitembelea Ofisi hiyo iliyopo mjini Dodoma. Hii ni mara ya kwanza kwa Mkuu huyo wa Utumishi wa Umma Serikalini kuzungumza na watumishi wa Ofisi hiyo tangu alipoteuliwa na Mhe.Rais Jakaya Kikwete kushika wadhifa huo
 
  Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI wakimsikiliza Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Yohana Sefue
 

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Yohana Sefue akizungumza na Viongozi na Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI ambapo aliwataka wachape kazi kwa bidii katika kutoa huduma bora kwa wananchi. Alisema sura ya Serikali unaweza kuitambua kupitia Ofisi hiyo ambayo ndiyo yenye jukumu la usimamizi na uratibu wa Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...