Matayarisho ya mwisho ya Mashindano ya 12 ya Mbio za Hisani za Mbuzi yatakayofanyika Septemba 1 mwaka huu jijini Dar es Salaam yanaendelea.

Tukio hilo la kifamilia linalofanyika kila mwaka tayari limeshafanikiwa kukusanya kiasi cha Shilingi milioni 544 (zaidi ya dola 345,000) kutoka kwa karibu makundi 50 ya wahisani wa ndani tangu lilipoanza mwaka 2001. (Tazama maelezo chini kwa mbio za mwaka huu.)

Zaidi ya watu 3,000 hushiriki kila mwaka, huku pia wakijifurahisha kwa kutabiri mbuzi atakayeshinda, wakishiriki kwenye mashindano ya mavazi yenye muonekano wa aina yake na kujiaribu ladha ya vyakula mbalimbali vya kiasili na vinywaji wakiwa na familia na marafiki zao.

Yeyote anaweza kushiriki na kushinda zawadi mbalimbali za kuvutia, ikiwa ni pamoja na zawadi kubwa kwa mwaka huu kutoka Shirika la Ndege la Uingereza (British Airways) tiketi ya kwenda na kurudi Uingereza. 

(Tazama orodha nzima ya zawadi .)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...