Licha ya kuwa ametoa mchango mkubwa wa sanaa katika tasnia ya Muziki hapa nchini, wasanii na waandaaji wa matamasha mbali mbali waliokuwa wakimtulia wamemtelekeza msanii maarufu Bi Fatma Binti Baraka (Bi. Kidude) kutokana na hali yake ya kuumwa.ambapo hadi sasa yupo kitandani na hajiwezi.
Ankal naomba uwafikishie ujumbe huu wasanii wote na waandaaji wa matamasha waliokuwa wakifanya kazi na bi Kidude kwani anaumwa sana.
Mdau wa Globu ya Jamii
Zanzibar



Pole sana Bi Kidude, Mwenyezi Mungu akujalie kipindi hiki kigumu upate kupona na kurudi kwenye tasnia. Kaka Michuzi tuwekee namba ya simu ili tuweze kurusha michango ya kumwezesha apone
ReplyDeletePole sana Bibi yetu Bi Kidude. Mwenyeez Mungu atakujaalia hujambo na kukupa takhfif, kawaida kwa maradhi kuingia huwa ni rakhisi sana, lakini kutoka inachukuwa muda na yataka stahamala, tunakuombea kwa Mola upone haraka INSHA ALLAH.
ReplyDeleteNa nyie wasanii mnaodaiwa mlikuwa mkimtumia kwenye matamasha yenu kucha kutwa, mbona hamko usoni kutaka kufaham hali yake na khasa kwa sasa hivi anavyoumwa. Mnadaiwa mmemtelekeza, hivyo sio vizuri siyo uungwana. Pole sana Bi Kidude, aso mtu ana MUNGU na kuuguwa katu sio kufa, uguwa pole na Mola akupe hujambo upone haraka INSHA ALLAH. Pia tunakutakia EID MUBARAK njema, japokuwa upo kitandani, tuko pamoja bibi yetu.
Kwanza, Anon Sat Aug 18, 07:28:00 PM 2012 acha unafiki, tafuta namba mwenyewe kimya kimya umtumia au ujue utakachofanya.
ReplyDeletePili, sio vizuri kurusha picha ya namna hii hewani, kama story ingewekwa bila picha, maana ya kusema hivyo kila mtu aiulize nafsi yake itamweleza maana ya kukataa picha kama hii.
Tatu, tuone unafiki wetu tulio nao binadamu!! Nikiwa mzima, msururu wa watu, nikiteleza, watu walewale wanaangalia pembeni!!
Mwisho, tuombe kwa Mwenyezi Mungu amwezeshe Bibi yetu kupata faraja na maana ya hatua hii katika maisha wakati wataalamu wakifanya kila liwezekanalo kitaaluma kumponesha!!
mwenyezi mungu akujaalie upne bibi haraka na akupe upeo wa kumkubuka allah isiwe tena kwenye kuutumia mda wako kwa mambo yasiyokuwa na maana na hayakusaidii kitu
ReplyDeletekumbuka na umri ulio tena siwakuingia tena kwenye mambo haya ya kidunia na yakitoto
mrudie mungu wako kwa kufanya IBADA kwa wingi sana huu wote ni mtihani mdogo sana pengine itakuwa ni funzo utakapopona bibi
Tunaomba namba ya simu na mtu wa kuwasiliana nae,
ReplyDeletewadau
FFU
Pole sana bikidude mwenyenzi mungu hatakupa nguvu na hutapona
ReplyDeleteKweli weka namba yake ya m-pesa, yake please maana wa bongo mtaweka zenu na kufanya mradi
ReplyDeleteAib mara elf
ReplyDeleteShame on all of us. This poor soul has been EXPLOITED all these days. Helping some clever humanoids to collect millions for themselves. Now she is all alone and no one to care for her. Aibu kuu.Serikali ya mapinduzi should step in and help her for she was a national beacon of light.Mungu akusaidia bibi yetu.
yaani Unamuomba MUngu Ampe salama arudi kwenye tasnia sio Umuombee amrudie Mungu na kustaghfiru?
ReplyDeleteHuu ni wakati wa kurudi kwa Mungu na sio kwenye tasnia za kipuuzi kwani hizo hazitomsaidia kitu Mungu ni mwingi wa rehema na hupokea tobakwa waja wake,Ewe MUNGU mjaalie apone na akurudie wwewe na umsameh makosa yake(amin)
ReplyDeleteEnd of an era is approaching, she has done her time.
Mlio karibu nae niko na hakika you recite madua na Quran to her.
Na kumkumbusha shahada.
Ni kweli bibi yetu anahitaji dua nyingi, ili apone na amrudie mwenyezi mungu subhana wataala. Huu umri aliofikia, sio umri tena wa kufanya fujo(shughuli za anasa au kuwaburudisha watu kwenye mikutano ya anasa) majukwaani na kumkwaza mwenyezi(ukweli hamna umri unaoruhusiwa kufanya anasa au kushiriki). Mwenyezi ametoa mtihani mdogo na endapo atampa nafasi nyingine, basi arudi kwake haraka iwezekanavyo. Tunakuombea bibi. Iddi Njema wadau!
ReplyDeleteWabilah Taufiq
Tafadhali tuangalieni lugha zetu zisichafue hali ya hewa. (Namlenga sana Anony. Sat Aug 18, 10:07:00) unapotosha kabisa. ujumbe wako unaonekana unamtakia bibi yetu mabaya kwa jinsi kiswahili chako kilivyo. Umeandika hivi " ....mwenyenzi mungu hatakupa nguvu na hutapona"... jinga sana wewe. chunga lugha yako.
ReplyDeleteMadudu, takataka,uozo wa maneno ya watoa maoni hapo juu wengi wao hata hilo la msingi sijui kama mmefika, hutaona watu kama Mashaka wanajitokeza kusema upuuzi kama wenu, au kina David V. Ovyooooo. Kosa gani kafanya huyu bibi, mpaka unasema arejee kwa Mungu wake, eti tasnia ya muziki ni mambo ya kitoto. Kwani, unajua kwamba baada ya muziki alikuwa hasali ???? jibu swali weye mwenye akili zilizo ndogo kuliko za inzi. Halafu , kwani kuugua ni kosa ??? na unaposema wamemterekeza ,una maana gani ??? Nakushukuru sana Ankal huchagui comment za wasomaji,kwa maana hiyo huna ubaguzi, nafikili unafahamu wazi kwamba ,kwenye msafara wa mamba, konokono,vyura kenge huwa hawakosi, Ubarikiwe .Zebedayo msema kweli
ReplyDeleteI hope she recovers quick!
ReplyDeletein my opinion people like her should be treated like a treasure to the govt. Hence the govt should take lead in helping her. She has done a lot for the country in terms of helping Sanaa.
Mdau Iringa
Bibi umetuwekea mengi juu kama nchi, kuumwa kwako ni kwetu, maumivu tunayasikia wote. Tutajaribu iwezavyo kukusaidia katika ugonjwa. Tunaomba nusura ya mwenzi tuvuke salama. Twakupenda na hata katika ugonjwa Eid Mubaraka
ReplyDeleteMwalimu wa Mwalimu Nyerere kafariki bila kupata mafao yake sasa mlitegemea huyu Bi Kidude afanyiwe nini na serikali hii? Bi Kidude hakuwa mfanyakazi wa serikali na hakuwa na mkataba wa ajira na mtu yeyote. Hapa ni suala la ubinadamu tu kwamba watanzania wenye mapenzi tumchangie apate matibabu na matunzo muafaka. Nimemuona Bi Kidude katika video za wasanii wengi, je wakowapi hao??
ReplyDeleteEVERYBODY JUST SHUT THE FUCK UP AND LETS DO SOMETHING ALREADY!! BLAMES AINT GONNA HELP HER, LETS COLLECT WHATEVER WE CAN MANAGE AND CHANNEL THROUGH HERE KWA ANKAL MSAADA UTAFIKA TU, HATA TUKITAKA AENDE ABROAD. ANKAL PUT A MOBILE NUMBER WHERE WE SHOULD RAISE FUNDS FOR OUR LEGEND BEFORE ITS TOO LATE. SHAME ON ALL WHO EXPLOITED THIS POOR SOUL, IT WILL HAUNT YOU FOR THE REST OF YOUR LIVES! Sorry for the language Ankal, it had to be said like it is!
ReplyDeleteGive them the privacy they need to give her health and to support her sojourn to the next world if thy Lord so wishes. Voyuersm and negative comments are hurtful at times like these
ReplyDelete