Mahakama Kuu Kanda ya Tabora imetoa hukumu ya kesi ya ubunge iliyokuwa ikimkabili mshindi wa ubunge jimbo la Igunda Dk. Dalaly Peter Kafumu (CCM).Hukumu hiyo ambayo ilikuwa ni ya kupinga matokeo yaliyompatia ushindi Dk Kafumu imetolewa leo ambapo imemuengua mbunge huyo katika nafasi yake ya ubunge

Shauri hilo lilifunguliwa na mlalamikaji,Joseph Kashindye ambaye alikuwa ni mgombea  mwenzie dhidi ya Dk Kafumu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na msimamizi wa uchaguzi.

TAARIFA KAMILI ITAWAJIA BAADAE KIDOGO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. CHADEMA JUU JUU 2015

    ReplyDelete
  2. Hakika mahakama imetenda haki na akumvua(KUMFUMUA) Kafumu ubunge wake,na sasa tusubiri Sep 20 pale Arusha kwenye rufaa ya Kamanda Lema.
    Pepoz............Power we acha tu mpaka kieleweke.

    ReplyDelete
  3. Jamani CCM wenzangu mbona tunakwenda kama hatuna macho???? tukifanya chaguzi ndogo CHADEMA wanachukua viti, tukishinda sisi kumbe tumefanya mizengwe kulikoni na nini outcome ya 2015 TUTASHINDA????????

    ReplyDelete
  4. Kafumu kafumuliwa na kashindye kashinda!

    ReplyDelete
  5. Safi sana, Magamba chiniiiiii!

    ReplyDelete
  6. slowly the court is giving me hope that justice can sometimes be done in Tanzania.

    ReplyDelete
  7. Utawala wa sheria ndio utakaoliokoa taifa la Tanzania , hii ni hatua muhimu kuelekea kuwa na katiba mpya, ifike mahali jamii yetu bila kujali cheo cha mtu SHERIA KWANZA vyeo baadae hapo tutakuwa salama. Ifike mahali mahakama ifanye kazi yake bila shinikizo la mtu au chama fulani kwani katiba yetu ni yetu sote na pawapo na dirisha la rufaa watu wasisite kuitumia . Mungu ibariki Tanzania.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...