Orly Ilemba, akiwa nje ya nyumba aliyokuwa akiishi na marehemu kaka yake, Patrick Mafisango baada ya mwenye nyumba kutoa nje vyombo vya ndani kutokana na deni la pango.
Baadhi ya vyombo vya ndani vya aliyekuwa kiungo mahiri wa Simba, marehemu Patrick Mafisango vikiwa nje ya nyumba aliyokuwa akiishi katika eneo la Keko Bora jijini Dar es Salaam, baada ya mwenye nyumba kuvitoa nje kutokana na deni la pango.
Na Andrew Chale
FAMILIA ya aliyekuwa kiungo mahiri wa mabingwa wa soka Tanzania Bara, Simba, marehemu Patrick Mutesa Mafisango iko katika wakati mgumu baada ya kutimuliwa katika nyumba waliyokuwa wakiishi, Keko Bora jijini Dar es Salaam.
Familia hiyo, ilitolewa nje vifaa katika nyumba hiyo na mmiliki wake, kutokana na kudaiwa kodi ya pango aliyokuwa akiudai kwa muda mrefu uongozi wa Simba.
Akizungumza kwa masikitiko makubwa jana, mdogo wa marehemu Mafisango, Orly Ilemba, alisema, mwenye nyumba huyo, Chingweni Mtoro, aliwafuata asubuhi na kutaka chumba chake kabla yakutoa vitu hivyo nje ya chumba na kuweka kufuli jipya.
“Nipo nje tokea asubuhi, hatujafanya lolote, zaidi nalinda vitu vya marehemu, viongozi wa Simba kila nikijaribu kuwapigia simu hawapokei mpaka sasa sina la kufanya,” alisema Ilemba.
Alifafanua kuwa, viongozi hao wa Simba walijua mwisho wa kukaa humo, lakini wameshindwa kushughulikia suala hilo mapema mpaka wanakutwa na aibu hiyo.
“Lakini mwenye nyumba huyu, alisema mkataba huo ulitakiwa kufika mwisho Agosti 8, kamawalivyokubaliana na viongozi wa Simba, lakini mpaka jana viongozi hao hawakuweza kumalizana naye ndio maana kaamua kufikia hatua hii,” alisema kwa masikitiko.
Mdogo huyo wa marehemu Mafisango, yupo nchini kwa ajili ya kusubiria rambirambi, ambazo klabu ya Simba iliahidi kuzitoa.
Juhudi za kuupata uongozi wa klabu ya Simba, kujua wana taarifa na wanachukua hatua gani, zilishindwa kuzaa matunda kwani wahusika, hawakupatikana.
Mafisango kati ya nyota mahiri waliochangia kwa kiasi kikubwa timu hiyo kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu msimu uliopita iliyofikia tamati Mei 6, alifariki dunia Mei 17, 2012 kwa ajali ya gari, eneo la Keko, jijini Dar es Salaam.
Juhudi za kuupata uongozi wa Simba kuzungumzia hali hiyo ilishindikana baada ya baada ya simu msemaji wa klabu hiyo, Ezekiel Kamwaga kutopatikana kwa siku ya jana.
Sasa kuhusiana na suala hili Simba Sports Club inahusiana vipi na jukumu hili? Mimi ninadhani kinachowahusu Simba ni kuilipa familia ya Mafisango haki zote zinazohusiana na mchezaji huyo na sio kuendelea kugharamia makaazi ya jamaa zake.
ReplyDeleteNadhani madaktari ku mstari wa mbele katika mapokezi ya Bwana Ulimboka ni sawa, ila huyo Bwana Markus mchochezi yeye anahusiana vipi na suala hili kama sio kuleta fitna na chuki? Tunataka amani itawale Tanzania.
ReplyDeletehttp://www.dailymail.co.uk/news/article-2187110/David-Simpson-Now-I-just-want-home-First-interview-British-pilot-brutal-African-jail.html?ICO=most_read_module
ReplyDeleteSamahani haiendani na ya mchezaji mpira mada tofauti.
Jamani hiyo link hapo juu wazungu wengi wakifungwa wanaachiwa kwa ufisadi wa nje na nchi zetu za africa sababu nchi zao zinaandika stori za uongo kama stori ya link hiyo juu kwanini nchi za Africa wanawaachia hawa? Hata Zebedayo msema kweli ataikubali hii.
Naomba kuuliza jamani huyo mafisango si alikua sio mtz sasa vipi hapo alihama na ukoo wake wote huko kwao..simba ilisajiri mchaza mpira mmoja tu ambae ni huyo marehemu...sasa hao wengine wametoka wapi?..utakuta hawana hatakibali cha kuishi hapo tz..mm siwaelewi kabisa watz wanavyo ishi...waulizeni kwanza hao ndugu zake marehemu je wanaishi kiharari hapo tz..nakama hawana vibari muaite polisi wawakamate ili waludishwe kwao...amkeni watanzania kwenye usingizi...juzi nimesikia barozi wa marawi hapo tz akiwaambia wamarawi wanaoishi hapo..eti nchi ya tz mtu mgeni haulizwi utaifa wake labda mpaka ufanye kosa..kwa kweli nilistuka sana..ndio maana wageni wanazagaa wanavyo taka..tena hawana vibali vya kuishi..kamavile hatuna wizara ya mambo ya ndani..au polisi...jamani polisi wa tz mkajifunze kwa wa south africa..jinsi wanavyo wasaka watu wageni usiku na mchana...south africa..wanajeshi wanakamata watu wageni toka mpaka ni..wanawapeleka polisi na polisi wanawahifadhi vituoni mpaka emigresheni itakapokuja kuwahoji kwa nn mmekuja south africa..hivyo wezetu ndivyo wanavyo fanya..na nikosa la jinai raia yoyote yule kumuhifadhi mtu mgeni..kitu ambacho hapo tz hakipo..amkeni watz kumuhifadhi mtu ni kosa la jinai..asanteni wadau wote...na amani kwenu..ni mm mdau wenu..tajiri wa mawazo endelevu..niko uk.
ReplyDeleteSasa kama hamjalipa pango la nyumba mlitegemea nini? Lipeni hela muendelee kukaa. Simba inakujaje hapa? Je, hapo Simba inadaiwa na marehemu? Basi kama ni hivyo fuatilie hizo haki Simba halafu mlipe pango. Jambo dogo jamani sio kila kitu serkali tuu. Manake hamkawii kusema serikali iingilie kati.
ReplyDeleteSaafi sana wanajisahau sana hawa dogo wakishapata jina. Wanatumia pesa kwenye matanuzi na kusahau kuna mauti.
ReplyDeleteKha! Wakongo wanapenda kujipweteka wewe kakako/mumeo kafa wakati maiti inapelekwe si ubebe na mzigo uende? Au basi mumeo alivyokuwa hai au sijui kakako ulikuwa unamtegemea kwa kila kitu? hata kuhamia room moja umeshindwa ukiwa una fikiria kwa kwenda.. jamani mie Yanga ila kwa hili natetea Simba
ReplyDeleteMtowa maoni hapo Juu unalala mika kuwaa jamaa alikuwa sio Mtz inakuwaje familia yake aimebakia hapa ?sasa lakini si sote wafrica ndugu kuna ubaya gani wakibakia kwa ndugu zao wakiafrica wewe unataka wende wapi
ReplyDeleteHujafa hujaumbika, leo kwangu kesho kwako! hakuna anaejua kwa nn hao jamaa waliendelea kuwepo hadi sasa. Hata kama Mafisango (RIP) alikuja kucheza mpira, haimaanishi hana ndugu. kila familia ina mipango yake! Hakuna anaejua walimtegemea kwa kiasi gani! Tuache kutoa conclusions ambazo hazina uhakika! Kwa nn wasisaidiwe wakarudi kwao! By the way, kama ile rambirambi haijatoka, kwa nn isitumike kuwarudisha? (mtizamo tu). Vinginevyo, kama binadamu wengine waliokumbwa na matatizo, nao wanahtaji kusaidiwa!
ReplyDeleteEddy
Van.
Simba hawana kosa hapo.Wachangiaji wengi hapo juu wameshaongea niliyotaka kuongea.
ReplyDeleteDavid V
Jamani nyie wote mliongea hapo juu mbona hamuelewi somo. Tatizo ni kwamba Simba kama muajiri wanapaswa kukabidhi vitu vya marehemu pamoja na pesa za rambi rambi kwa familia au msimamizi wa mirathi wa Mafisango. Sasa inaonekana Simba bado wanazungusha kukabidhi pesa za rambi rAMBI NA NDIYO MAAN HATA HIVYO VITU VYA MAREHEMU BADO VIKO KWENYE HIYO NYUMBA WALIYOKUWA WAMEMPANGISHIA MAFISANGO.
ReplyDeleteIkumbukwe Mafisango ni international player ambaye Simba ndio wanaohangaikia pango la nyumba la mchezaji mgeni so simba walitakiwa wakati wanapeleka msiba kongo wapeleke na vitu vya marehemu. SO SIMBA NDIO WENYE MAKOSA.
ReplyDeleteSIMBA S.C.
ReplyDeleteBaada ya Msiba ya mtu aliyekuwa muhimu sana kwa Klabu yenu Marehemu Patrick Mutesa Mafisango ambaye alipigana kiume mkapata Kombe la Ubingwa 2012 hapo 6 Mei 2012 na kama ilivyokuwa ahadi akaitwa siku 11 baada ya Ushindi wenu.
Kwa vigezo hivyo mlistahili kuheshimu na kuthamini mchango huo huku Mhanga wake akiwa ndani ya Kaburi mbele za haki.
Ama kweli thamani ya mtu ni akiwa hai,
Jamani Friends of Simba mpo?
Au Urafiki wenu ni wakati mtu akiwa hai?
Hii ndio bongo masharobaro wanasema bongo new york, mbona kazi, ndio maana wacameroon wamezamia UK baada ya olimpic kuisha, namna hii.
ReplyDelete