THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA MINISTRY OF NATURAL RESOURCES AND TOURISM



TAARIFA KWA UMMA
HAKUNA MPANGO WA KUWAHAMISHA WAMASAI

Wizara ya Maliasili na Utalii inasisitiza kuwa hakuna mpango wowote wa kuwahamisha Wamasai 48,000 kutoka Serengeti, wala popote pale nchini, ili kupisha shughuli za uwindaji.

Hii ni taarifa ya pili kutolewa na Wizara kukanusha kampeni ambayo inaendelea kusambazwa kupitia mtandao wa kompyuta wa Avaaz inayowataka watu wajiorodheshe kupinga kuhamishwa kwa Wamasai kutoka Serengeti.

Hata hivyo mtandao huo umeendelea kusambaza habari hizo na kuwataka watu wajiorodheshe ili kupinga mpango huo na kuiandikia Wizara wakiitaka iusitishe. Hata hivyo sasa wamebadilisha tamko lao na kusema kuwa walipotaja Serengeti katika taarifa yao ya awali walimaanisha kuwa ni eneo lote lililoko kwenye Mfumo ikolojia wa Serengeti (Serengeti ecosystem). Hali hii inafuatia Taarifa ya kwanza iliyotolewa Agosti 15, mwaka huu ambapo Wizara ilikanusha kuwepo kwa mpango huo.

Wizara imewataka watu na Jumuiya ya kimataifa kutopoteza muda wao kujiorodhesha kupinga kuhamishwa kwa Wamasai maana wamepotoshwa kwa kuwa hakuna mpango kama huo popote pale nchini Tanzania. Uwindaji wa kitalii hufanyika katika Mapori ya Akiba na siyo katika maeneo wanayoishi wananchi, hivyo shughuli hiyo haiambatani na kuhamishwa watu.

Watu wote ambao wamejiorodhesha baada ya kupotoshwa na mtandao huo wanaalikwa kuja nchini kama watalii ili waitumie fursa hiyo kujionea wenyewe taratibu za uhifadhi zilivyo nchini na kujidhirisha kuwa taarifa iliyotolewa na mtandao huo siyo ya kweli.

Imetolewa na

George Matiko
MSEMAJI
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
Tarehe 24 Agosti 2012
Simu: +255 784 468047

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Watanzania wenzangu,

    Kikulacho ki nguoni mwako, mara zote unapoona jambo limekutokea ujue pana mtu wa karibu yako anaefanya athari.

    Sio rahisi upate athari kutoka kwa mtu wa mbali.

    Haya madai ni 'Propaganda' zisizo na mshiko wala tija, wala ushahidi yanayokusudia kuwapa kufikia malengo yao hao wanaosambaza hizi Propaganda.

    Madai haya ya kuwahamisha Wamasai yanasambazwa Duniani na majirani zetu ndugu zetu wanaotupaka mafuta kwa mgongo wa chupa sio wengine bali ni JAMHURI YA KENYA!

    ReplyDelete
  2. Kenya inatapa tapa sana na inakosa usingizi juu ya Tanzania na mali zake!

    Tanzania imejaaliwa saana na vitu vingi tu, Kenya hamuwezi kuziba jua kwa ungo!

    Hizi tunajua ni Propaganda zenu.

    ReplyDelete
  3. JAMHURI YA KENYA:

    Muangalie kwanza maslahi ya wananchi wenu ambao zaidi ya 85% ni (land less) yaani hawana ardhi kutokana na Misingi yenu mibovu ya Ukabaila,Umangimeza na Ubeberu.

    Ardhi ya Kenya nchi nzima inamilikiwa na watu wasiozidi asilimia 15 ya wakenya wote na hivyo zaidi ya Wananchi wa KENYA 85% ni masikini kapuku wasio na hata ahadi ya kuwa na uwanja wa ukubwa wa kaburi moja!

    MTATUE TATIZO LA UMASIKINI WA ARDHI WA WAKENYA HAO ZAIDI YA 85% KWANZA HALAFU NDIO MJE KUENEZA PROPAGANDA ZA MALIASILI NA MAZINGIRA KTK AFRIKA YA MASHARIKI.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...