Professor Jay(The Heavy Weight MC) ameamua kuingiza mtaani(kupitia kila aina ya media inayoweza kuwafikia wananchi na mashabiki wa muziki) single inayokwenda kwa jina Hellow. Hii inakuwa single ya tatu kutoka katika album ya JaySco Dagama ambayo ingawa bado hajaamua kuitoa rasmi,ni wazi kabisa kwamba pengine itakuwa album bora kabisa kuwahi kutolewa nchini Tanzania na msanii kutoka kizazi kinachoitwa “Kizazi Kipya” au New Generation.
Hellow unatoka katika kipindi muafaka.Kama unafuatilia sindimba za starehe nchini Tanzania,kilichopo kwenye kona ni msimu mnene wa Fiesta.Hellow,bila shaka,inalenga katika kuhakikisha kwamba,mtaani kila mtu anamwambia mwenzake Hellow.
Hii ni production kutoka kwa Dully Sykes ambaye bila shaka utakubaliana nami kwamba ameitendea haki vilivyo chorus ya wimbo huu.Usikilize Hellow
Read more: BongoCelebrity 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa


  1. Alafu uyu Dully Sykes pozi zake bwana!

    ReplyDelete
  2. DULLY SYKES, MBONA MASHATI YANABANA SAANA. punguza majisifu ndugu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...