Wa-ndugu,
Salamalekoni
Poleni kwa Mfungo wa Ramadhan kwa wale mnaofunga.
Nawaomba muwe wa-kweli na hakimu wa haki, katika hili Mtaliamuaje?
Nawaomba muwe wa-kweli na hakimu wa haki, katika hili Mtaliamuaje?
Kumbukeni Huu sio Mgomo wa Madaktari au Waalimu, this is different story, bond or contract all together; hakuna muajiriwa wala muajiri hapa, AU yupo?Utafanya nini kama umeitwa kusawazisha mgogoro huu? Siku ya Ijumaa John aliamka mapema kuliko kawaida na kujiandaa kwenda kazini. Siku hiyo alikuwa anahitajika kazini mapema kuliko kawaida. Ingawa mke wake alikuwa akifanya kazi katika ofisi iliyo umbali mfupi tu kutoka ofisi kwake hakuona sababu ya kumsubiri ili waondoke wote. Katika harakati za kuwahi, bila kujua John akanyanyua simu ya mkononi ya mke wake na kuitia mfukoni. Hakuweza kuitambua mara moja kwa sababu walikuwa na 'handset' zinazofanana. Baada ya kuondoka ndipo mke wake alipogundua kwamba mumewe ameondoka na simu yake. Hata hivyo hakuwa na la kufanya; akachukua simu ya mumewe na kwenda nayo kazini kwake ili endapo mumewe atampitia ampe simu hiyo.
Akiwa kazini ndipo John alipogundua kuwa ameondoka na simu ya mkewe. Wasiwasi ukaanza kumuingia maana alijua mkewe anaweza kusoma meseji za mapenzi zinazotumwa na wapenzi wake wa nje (nyumba ndogo). Hata hivyo hakuwa na uwezo wa kurudi nyumbani. Mke wake pia alikuwa na hofu kuu, maana nae alikuwa na mabuzi kedekede (mabwana) aliokuwa akiwachuna. Mambo yalianza wakati John alipopokea sms iliyokuwa imetumwa kwa mkewe kutoka kwa mtu ambae namba yake ilihifadhiwa kama Peter - Tax. sms hiyo ilisomeka "Hi sweetie, za asubuhi? 4me niko ok, just mad! mapenzi yangu kwako yananiua...hasa baada ya jana kunipa.....hapa moyo wangu unaruka kichurachura... Mara moja John akakumbuka kwamba siku iliyopita mkewe alichelewa sana kurudi, na alipofika alidai kichwa kinamuuma sana na alipitia zahanati (dispensary) kupima maralia. Saa moja baadae ikaingia sms nyingine kutoka kwa mtu mwingine ambae namba yake ilikuwa imehifadhiwa kama Mary -Saloon. sms hiyo ilisomeka "Hi baby mie niko poa, but sijisikii vizuri pasipo mkono wako kupapasa kifua changu...wewe ndie una control every part ya moyo wangu. See u at lunch..." John alikuwa karibu apasuke kwa hasira.
Kazi zilikuwa hazifanyiki ofisini, na tayari akawa anafikiria kumuomba bosi wake ruhusa ili amfuate mkewe akamfundishe adabu. Kabla hajafanya hivyo ikaingia sms nyingine kutoka kwa mwenye namba iliyohifadhiwa kama Nyanso - duka la vipodozi. Sms hiyo ilisomeka "Ma luv I wish ungekuwa big G ningekuwa nakutafuna kila wakati, ninapokuwa nawe najiona kama malaika...na hasa ninapo kumbuka unavyokula soseji...Have a good day ma luv.
Mpaka hapo John hakuweza kujizuia, Jasho lilikuwa likumtoka kwa wingi wakati kila mtu ofisini alikuwa amevaa koti kutokana na baridi ya kiyoyozi. Wafanyakazi wenzie walikaribia kuita ambulance kwa kudhani jamaa amepata shinikizo la damu.
Mkewe nae hali yake ilikuwa taabani. Alikuwa amekwisha pokea sms tatu kutoka kwa wanawake tofauti. Ya kwanza ilitoka kwa mtu ambae namba yake ilihifadhiwa kwa jina la 'OCD - Oysterbay Police'. Sms hiyo iliandikwa hivi "Hi darling..unaendeleaje? me niko sawa pamoja na mwanao hapa. Anakupenda sana na kila wakati anakutajataja. Itabidi uhamie hapa tukae pamoja...see ya baadae".
Jane alichanganyikiwa kupata habari kwamba mumewe ana mtoto mwingine nje ya ndoa." Ndio maana kila siku hana fedha...." alifikiria.
Lakini kabla hajajua afanye nini ikaingia sms nyingine kutoka kwa Ramadhan - Kinyozi. Sms hiyo ilisomeka " siwezi kulala usingizi bila wewe...Kila ninapojitupa kitandani ndani ya jumba hili ulilo ninunulia najisikia kulia machozi ya furaha. Rav 4 uliyoninunulia kila msichana kazini ananiuliza nimeinunua wapi lol...Thanks darl, g'day". Sms ya mwisho ilitoka kwa Jimmy - muosha magari. Iliandikwa "sasa honey? Ope uko poa, mi niko fit hapa hm, lakini nimekumiss sana. But honey kuna dola tunadaiwa za project like 40k nitacome unishow vile tutalipa. Nice day, love you kwa sana..." Jane akapata jibu kwa nini siku zote mumewe hana pesa kabisa licha ya kuwa na kazi ya maana sana na miradi kibao. Jioni walipokutana nyumbani hakuna aliyekuwa akizungumza...Kila mtu alikuwa kanuna huku akimuangalia mwenzake kwa mashaka.
--Hebu niambieni, hapo mtu unaanzaje kusuluhisha (au wengine hamlioni sooo hapo?)--Je unyumba hapa bado upo??? (bond, contract)?? au ndiyo Maiyolo ngaji?DOC.


I love your hand writting.I wish you could teach Other people how to write.
ReplyDeletecommon man,this is kind of nonsense, kwanza is too long na pia hakuna geni hapa ,haya mambo ni kawaida sana kwa jamii zote duniani, mpaka Rais Clinton alifumaniwa ikulu ana tafuna karani wake. Yaani wewe mtoa mada hii, ndo unaamuka usingizini ??? au una umri gani !!!! dont waste our time dude. grow up kid. Zebedayo msema kweli
ReplyDeleteduh hii noma lkn hakuna ndoa tena maana kila mtu ana kula uroda njee ya ndoa.ikiwa watasameheana waombane radhi na ikiwa kwali wana takana kila mmoja wasirudie tena mchezo huwo.wabaki wamalize maisha na yule aliye zaa naye itabidi mtoto amtizame kipesa hadi akuwe.
ReplyDeletealiyenunua cheni kanunua cheni bandia na aliyetoa pesa katoa pesa bandia bongo Dar-es-Salaam))
ReplyDeletewell mimi ningewasaidia hivi ,kwanza unamwambia kila mmojaamrudishie mwenzie simu yake na kisha afungue inbox yake ajisomee mwenyewe sms zake, hapo utaona kila mmoja ananyanyuka bila hat kumwangalia mwenzake yani watapiga kimya hao hakuna atakayethubutu kumuuliza mwenzie tena utashangaa watakavyokuwa wanaheshimiana kama maafande manake kila mmoja ataona lake kubwa kuliko la mwenzie
ReplyDeletemwandiko gani huo wa kuku kajampa ,are you kidding me ??
ReplyDeleteMungu ni mwema sana, ndiyo maana dunia bado imesimama, haijaporomika kama enzi za Sodoma na Gomora. Uzao Shetani lusifa sasa ni mkubwa kuliko ule wa Abraham. Kila mmoja wetu aliye muasi Mungu kwa kupindisha maadili ya maisha, anamtumikia shetani au mashetani japo atawaona wamefanana na binadamu. Yesu ndiye pekee wa kuwatoa katika lindi hili la Jehanamu. Mimi Yesu nalishatoa huko.
ReplyDeletestory za kufikirika hizi, tumezikia saaana! Coming technology hizi story zime-replace hadith za sungura na fisi, Juma na Rosa n.k.
ReplyDeletengoma droo,kila mmoja ametoka nje ya ndoa.wakae watulie.
ReplyDeleteNi mpango wa Mungu kuwafungulia mlango wa ufahamu hawa wanandoa maana wangeenda mbali zaidi.Kwa hakika kila mmoja amekosa na cha msingi ni kuombana msamaha na kama ukikubalika basi wawekeane ahadi kwa mungu kwamba hawatarudia tena. Ila tu kitu kimoja ni kwamba wana kosa moja common la kutenda nje ya ndoa ila huyu mwanamke yeye alikuwa anakula nje na pengine alikuwa anapewa mshiko au assets hapa haijulikani. Lakini mwanaume pamoja na kula nje alikuwa na makosa matatu ya ziada. Moja kuzaa nje ya ndoa; pili kumjengea changu nyumba na kumnunulia gari; na tatu kulipa madeni. Wasisahau pia kupima UKIMWI
ReplyDeleteMr and Mrs Smith style is the solution,
ReplyDeleteCase rahisi sana hiyo! Ingekuwa cheating ni ya upande mmoja ndio pangewaka moto. Lakini hiyo ngoma ni draw! Labda cha kufanya mama kukamilisha hiyo game yao ni kwa yeye kutafuta naye katoto ka nje, maana mwenzake ana hiyo bonus! Halafu hapo ndio wasameheane na wachukue watoto hao wa nje waishi nao! Huku wakijiandaa kuanza kutumia ARV maana hapo piga ua UKIMWI wameshaukwaa.
ReplyDeleteNgoma droo hapo, ila inawezekana kuna tatizo kati yao wote wawili, labda hawaridhishani katika tendo la ndoo hivyo basi nitawashauri mwanamke aingine unyagoni kwa makungwi na mwanaume apelekwe mkoleni yaani wote wakafundwe ki unyumba zaidi
ReplyDeleteLooh!jamaa mkali anamchukua mpaka OCD?inabidi ocd avue kofia?
ReplyDeletetypically maisha ya vijana na wazee saivi, uwe umeoa au umeolewa ngoma ndio hiyo hapo ni kumuomba mungu sana maana tulipo na tunapoelekea ni pabaya sana, ni hayo.
ReplyDeletezebedayo ar u rilly serious?nyie ndo mnaotoka nje ya ndoa halafu ukiulizwa ,,,not guilt.....imekula kwako baba hiz si hadith za sungura na fisi ila ni reality ambayo wewe hutaki kuiona....wewe ndo grow up and START ACT LIKE A MAN.....
ReplyDelete