Sasa kama huyu jamaa hapa anajiamini kitu gani mkapa anaamua kuweka pozi hapa barabarani???au ndio kwamba anayajua sana magari na hayawezi kumfanya lolote?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Barabara nzuri kuliko nyumbani, maisha si mazuri. Hata mimi napenda kupumzika kidogo, na nikigongwa pengine ni nafuu kwangu maana nitahudumia na hivyo kuwa na uhakika wa angalau mlo mmoja kwa siku. Nikifa pia ni sawa tu kwa kweli.

    ReplyDelete
  2. Hawa jamaa inaelekea wanasubiri usafiri na kwa bahati mbaya sehemu kubwa ya nchi yetu hamna vituo vyenye kumuwezesha abiria kuketi na kusubiri usafiri. Inaelekea alisimama kwa muda mrefu na akajionea bora aketi hapo ili basi lisimpite. Ni hatari lakini hamna jinsi.

    ReplyDelete
  3. ushamba tu huo unawasumbua.

    ReplyDelete
  4. Sio.... pozi zingine, kiswahili gani hicho. ungeandika... pozi nyingine...!?

    Lakini kwa kuziangalia vizuri na kwa makini, sio kama hao vijana wamekaa hapo na kutuonyesha hayo mapozi yao, la khasaha! Hapo inaonyesha wanasubiri chombo chochote cha usafiri, almuradi waweze kuondoka pahali hapo. Ukiangalia hiyo gari ndogo picha ya mwanzo, imewapita au pengine dereva hakutaka kusimama au kakataa kuwapakia. Tukiangalia hiyo picha ya pili, kijana anaonekana kama anajaribu kukisimamisha chombo kingine cha usafiri ambacho kinakuja mbele yake (hakikuonyweshwa hapo kwenye picha). Hivyo kichwa cha habari hakiendani kabisa na picha halisi zinavyojieleza hapo, vinginevyo tutaanza kutowa 'comments' za kuwananga hawa vijana pasina sababu yeyote ya msingi. Nadhani ni utofauti tu wa mazingira, sio kila sehemu kuna 'bus stop' maeneo mengine watu wanasubiri usafiri au kusimamisha magari kwa mtindo huo, hakuna geni hapo.

    ReplyDelete
  5. Vibaka hao shauri yako wewe jifanye kusimama au punguza mwendo uone.

    ReplyDelete
  6. Jamaa anaombea agongwe ili ndugu zake walale barabarani kudai matuta, alafu magari yatembee polepole wauze nyanya zao. Akili kwa kichwa bwana!

    ReplyDelete
  7. Che GuavaraAugust 07, 2012

    Bange hizo na sio bure

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...