Katika zoezi la kukusanya na kuwasilisha maoni ya Waislamu juu ya Katiba Mpya vipo vyombo viwili kwa ajili ya Waislamu, vyote vikiwa na azma moja, kulinda na kutetea maslahi ya Uislamu na Waislamu nchini. Vyombo hivi ni:

1. Jukwaa la Waislamu la Kuratibu Mabadiliko ya Katiba Tanzania (JUWAKATA)
2. Mtandao wa Misikiti Tanzania

JUWAKATA imekwishatoa maelekezo muhimu kwa Waislamu katika kijitabu chenye anuani “MCHAKATO WA MABADILIKO YA KATIBA TANZANIA”. Jukwaa limefanya kazi kubwa ya kupita katika mikoa mingi nchini kutupa maelekezo muhimu na mambo ambayo Waislamu hatuna budi kuyapigania yawepo katika Katiba Mpya. Mtandao wa Waislamu wa Mawasiliano na Kupashana Habari umepata nakala ya kijitabu hiki chenye kutoa maelekezo kwa Waislamu.

Mtandao wa Misikiti Tanzania umetoa MUHTASARI WA HOJA NA MAONI JUU YA KATIBA MPYA kama yalivyokusanywa na kuratibiwa kutoka katika semina shirikishi za mtandao wa misikiti nchini. Semina hizi zimefanyika katika mikoa 17 Tanzania Bara na mkoa mmoja Zanzibar. Mtandao wa Waislamu wa Mawasiliano na Kupashana Habari umepata nakala ya kabrasha lenye hoja na maoni haya.

Waislamu hatuna budi kuwasilisha maoni yetu kama KUNDI MASILAHI na sio kama Watanzania, au watu wa wilaya, mkoa fulani au wa kundi la aina yoyote katika jamii ambalo halijinasibishi moja kwa moja na Uislamu. Katika kufikia lengo hili Mtandao umeambatanisha katika waraka huu MUHTASARI WA HOJA NA MAONI YA WAISLAMU JUU YA KATIBA MPYA. 

Nia na madhumuni ya kiambatanisho hiki ni kutoa fursa kwa Waislamu katika kila kona ya nchi yetu ya kutoa maoni haya kwenye Tume ya Taifa ya Kukusanya Maoni moja kwa moja kupitia E-Mail Address ya Tume (Anuani ya Tume ya Barua Pepe).

 Unaweza kuchagua idadi yoyote ya hoja na maoni (kwa jozi ya pamoja) na kuyatuma kwenye Tume kwa anuani ifuatayo: Email : maoni@katiba.go.tz

Ili maoni yako yapate tafsiri ya kutumwa na Muislamu kwa ajili ya Uislamu huna budi kujitambulisha kwa:

· Jina lako
· Mawasiliano ya Simu (kama una simu)
· Msikiti Wako Unakoswalia (Muhimu Sana)
· Wilaya na Mkoa (Ulipo Msikitin wako)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. tunashukuru kwa ufafanuzi huu mzuri

    ReplyDelete
  2. AHSANTE LKWA TAARIFA, TUNAOMBA TUWEKEWE PAHALA/TOVUTI YA KUPATA SOFT COPY KWA KUWA WENGINE HAWAKO TANZANIA. UTUWEKEE ANUANI YA TOVUTI HAPA HAPA KWA MICHUZI TUTAIPATA MUUMBA AKIPENDA, KAZI NJEMA NA TUITAKAIE KHERI NCHI YETU

    ReplyDelete
  3. Naona kama vile tunahitaji umoja, dunia sasa ina move katika umoja zaidi ikiwemo nchi za mashariki ya kati, watanzania tu embrace tolerance ambayo tumejaliwa kwa muda mrefu tangu enzi ya seyyid sayid alipokuwa ruler wa zanzibar.Hivyo tu refrain from elements ambazo zitaleta mgawanyo.

    ReplyDelete
  4. MBONA DINI ZINGINE HAJUSHUGHULISHI NA KAMPENI ZA AINA HII, shida gani ?

    ReplyDelete
  5. kwani katiba ni ya waislamu, wakristo, wengineo au wasio na dini au ni ya watanzania?

    ReplyDelete
  6. Mmmhh....no comments

    David V

    ReplyDelete
  7. 1}Utambuzi wa uwepo wa Mungu
    2}Kurejesha mahama ya kadhi kisheria
    3}Ubaguzi wa swala la mapumziko
    4}Adhabu ya kifo ibaki palepale
    5}Haki za kibinadamu zizingatie maadili yakitanzania au yakiafrika
    6}Nafas mbalimbali za zizingatie na uwiano wadin mbili hiz
    7}Tanzania ijiunge na OIC
    8}Tuwe na mfumo wetu wakislam
    9}Tuwe na uhuhuru na Haki kamili ya uwakilishi wakidin popote pale
    10}Sheria ya ugaidi ifutwe

    ReplyDelete
  8. hayo mawazo ni mchemsho usio na elimu na mishiko mnaturudisha karne ya 14, Hatuhitaji udini katika katiba mpya, mnashindwaje kujiundia mahakama yenu chini ya Bakwata mnataka kodi ya walalahoi iwaendishee mahakama?? Mbona makanisa wanamabaraza yao na hawaombi kodi yamabaraza yao? Bado unataka serikali ikusaidie kukuesabie waumini wako? si aibu kubwa? wakristo wanajijua wako wangapi katika makanisa yao, hata ukiwauliza data za ubatizo, makanisa mangapi, waumini waliopoteza maisha bado watakupa kwa mwaka, ndoa nk...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...