Habari Michu pamoja na Watanzania wote?Hapa nimekutumia Picha za MV.MAPINDUZI/MAENDELEO NA PEMBEA ZA KARIAKOO,Naomba sana uniwekee hii mada yangu.
*Hivi karibuni baada ya tukio la kuzama kwa MV.Skagit,Balozi Iddi Seif alifuta usajili wa Meli kama MV.Kalama na nyenginezo kwa kuwa muda wa matumizi yake kutokana na recommendation zilipotengenezwa umekwisha pita kama miaka 2 hivi na hizi Meli ni za 1983,Sasa Swali langu ni hili kwa wahusika wote akiwemo Mh.IDDI
(1).JE,MATUMIZI YA MELI ZA MV.MAENDELEO/MAPINDUZI ni Muda gani? kwa kuwa hizi meli nimezaliwa nimezikuta na nina umri wa Miaka 26 kwa sasa.
(2).La pili matumizi ya MAPEMBEA (mabembea) ya kuchezea watoto pale KARIAKOO-Zanzibar yamekwisha malizika muda wake kwa Mujibu wa Baraza la wawakilishi kikao mwaka 2002 kama sikosei ilithibitishwa kuwa pembea zote za Kariakoo zilitakiwa kutumika kwa muda wa either miaka 10 au 20 je kwa nini zinaendelea kutumika hadi leo na zimewekwa pale tokea miaka ya 70 wakati wa Rais Karume Snr.? Mungu aepushe mbali hatuoni kama majanga tunakua tunasababisha wenyewe?
(3).Na Je Watanzania wafanye nini kupinga matumizi ya (a) Meli (b) Pembea za watoto?
Ahsante nawatakia Ramadhani njema.
MDAU Bradford -U.K
Kwa kawaida meli,kila baada ya miaka mitano (5) years,lazima iende dry dock yaani kwa kiswahili gereji na inapandishwa juu ya mawe au magogo,inatolewa kabisaaa majini, hapa ita chekiwa kila kitu huko chini ,kama vile kuangaliwa unene wa umbile lake yaani unene wa chuma kama kimelika na kupunguza kiwango, wataangalia matenki ya maji yanayoibalance meli ( ballast tanks) itaangaliwa rada yake na propeller. Huko ni nje , injini room nako wata overhaull kila pump na pistoni zote na main bearings zote na wakaguzi waliobobea wa Llyods watahakiki kila kifaa kilichofunguliw.kama kuna kifaa kinatakiwa kibadilishwe basi wao wataamua hivyo. Meli hazina kiwango cha kuishi maadamu zinafanyiwa matengenezo ya kila siku na ukaguzi mzima wa kila miaka mitano, basi ndugu yangu usishangae meli ikapiga kazi kwa muda wa miaka 30.Hata huko UK na Ugiriki ,utakuta meli imetengenezwa mwaka 1964, hapa sija kurupuka tu kuchangia hii mada bali hata data kamili na picha za meli za miaka hiyo ninaweza kuwaomba washikaji wakanitumia,meli hizo zipo kazini hadi leo. Kuhusu hizo bembea za kariakoo,ni vyuma vitupu na minyororo, hapo cha msingi ni kuhakikisha vyuma vilivyochoka vinaondolewa na kuwekwa vipya ,kadharika na hiyo minyororo. Kila kitu ni matunzo na kufuata sheria, wengi wetu wanaweka pesa mbele na kuweka usalama wa maisha baadaye maadamu yeye habembei hapo. Cha msingi kingine hapa , tuwe na wakaguzi ambao watakuwa held resposible, siyo hao wenye meli, huyo atakayeikagua hiyo meli na kutoa leseni kwamba iko Oke kuendelea kupeta baharini,kumbe imeoza ,basi huyo ndiye ange swekwa lupango,maana huenda kala rushwa,kadhalika na hiyo bembea,hii iende sambamba na mabasi yetu yanayo ua watu kila baada ya wiki. Kwa hiyo mshikaji ,meli ya mwaka 1983 hiyo yaani bado kabisa ,kama kweli kuna mainjinia wenye vyeti halali na wanajua walifanyalo na pia imehakikiwa na Lloyds International na ina IMO registration. Asanteni ,ikiwa maoni yangu yamesaidia kukuelimisha. Nakutakia Christmas, oups!! samahani ,Ramadhani njema . Zebedayo msema kweli.
ReplyDeletewewe mdau wacha kuzungumza usichokijua na inaonekana ni muda mrefu sana huko znz kwa taarifa zako mapembea ya kariako ni muda mrefu hayatumiki na yapo katika mchakato wa kuvunjwa eneo lote na kutengenezwa upya tenda ipo ZSSF km hujui na pili mapinduzi haipo ni muda mrefu kwa kifupi tu ilishazama ktk bahari ya seyshell muda mrefu sana km huna la kuzungumza katafute mchanga ukachezee na vifuu
ReplyDeleteMdau wa Bradford UK,
ReplyDeleteMV SKAGIT ,MV.KALAMA, zilikuwa na muda wake maalumu wa kutumiwa.
''ISIPOKUWA KAMA UNAVYOONA TOKEA ULIPOZALIWA HAKUKUWA NA REKODI YOYOTE YA MAAFA'' kwa vyombo kama MV,MAPINDUZI,MV MAENDELEO NA MAPEMBEA YA WATOTO KAROAKOO-ZANZIBAR havina muda wa mwisho kwa matumizi ni kuwa vimekuwa vinaenda kwa Rehma ya Mwenyezi Mungu !!!
Mdau wewe endelea kukaa Bradford na usahau kwenu kabisaa; meli ya MV Mapinduzi iliuzwa na ikaenda kuzama mbele ya safari huko... Maendeleo hata hizo safari zake sijui kama zipo tena.. Mapembea tumeshayasahau na kiwanja kilitaka kuuuzwa/kukodishwa kile sasa hayo matumizi sijui umeyaona yanatumika huko Bradford au vipi?
ReplyDeleteKazi njema mkuu, watumie Pound hao wanaokuomba.. lakini hata hivyo vile vitu ni vya muda mrefu kweli
Mtoa mada pole kwa kutoa mada ya jambo usilolijua, mapembea ya kariakoo ilitangazwa tenda tokea mwaka jana kwa wanaofanya biashara ya chuma chakavu ili kuyaondosha, beba box huko uliko usirukie yasiyokuhusu
ReplyDeleteJamani jamani,huu ni mwezi mtukufu,tumsamehe huyu ndugu yetu wa Bradford,Huko sasa hivi njaa kali,mimi naona atupe jina lake kamili ili tumtumie hela kwa njia ya M-Pesa.Zebedayo msema kweli.
ReplyDeleteNamuomba Zebedayo aache dhihaka za kijinga.
ReplyDeleteMimi simlaumu sana mtoa mada ila namuomba siku nyingine ajitahidi kuandika habari ambayo yeye mwenyewe anaielewa kuliko kukurupuka kuandika historia.
ReplyDeleteInaonyesha Mdau wa BRADFORD-UK tokea ulipojilipua mwaka 1995 huko UK kwa Tiketi ya vurugu za Uchaguzi Pemba hujakanyaga tena Zanzibar !
ReplyDeleteHii ndio ubaya wa kupokea taarifa za kupitia e-mails, kwa nini usishushe ma-Boxi mgongoni angalau wiki moja ukaja Zanzibar?
wewe wa UK, unasema nini yale yote uliyasema hayapo,meli hazipo mapembea hayana kazi; nyiye mliyokimbia zanzibar kipindi hicho mmekuwa na kasumba ya kupotosha ukweli hamrudi kwenu mkaona maendeleo yaliyopo bali kazi yenu kusingizia uongo tuuu ili muendelee kubaki huko kwa kuiambia uongo serikali ya UK, hamuishi uongo mnajulikana kwa kusema yasiyokuwepo. Rudi nyumbani muone mabadiliko yote unayosea ni uongo mkubwa ni sawa na wenziyo waliyokaa Somali kisha wamerudi hapahapa wakiwa Airport, wanatoa maelezo ya kuwa nchi yao hii ni nzuri na imebarikiwa na Mungu kwa utulivu waliondokea nini.... hivi kweli Tanzania na Somalia ni sawa kweli?ukimbiye tz uende mogadisho ahhh imposible jirekebisheni uongo haujengi usichafue watu kwa maslahi yako binafsi. Elezea jambo la kweli watu walifanyiye kazi kwa kurekebisha kasoro zilizopo.
ReplyDeleteBashir, Serikali na viongozi pia wana sema uongo na kuwa danganya wananchi. Ukweli ni watu wana kosa imani na heshima ndogo kwa viongozi. Wana tumia muda kuji safisha kama siyo mchafu basi chapa kazi wacha kuuza sura. Watu siyo wajinga. Nioneshe muongozi maskini Tanzania?
ReplyDeleteEheee !!! haya ndiyo niliyokuwa nayataka , wabongo kuwakomalia hao waliokimbilia kilichopikwa na wenzao, sasa wamebaki kusema UONGO, UZUSHI, KASHIFA. duh !! leo aisee nimefurahi sana ,mulivyowachambua hao wa UK,maana mimi pekee ninapowasema nimeonekana kama nawachukia eti nimepigwa patresheni ,wala ?? huko UK sijafika na sitaki nifike. sisi tutaijenga nchi yetu kwa moyo mmoja . Yaani wewe mtoa maoni wa mwisho , njoo jioni tufuturu pamoja,niko mta wa makuganya karibu na kituo cha Fire.Zebedayo msema kweli
ReplyDeleteNaam Zabedayo msema kweli leo nilikuwa nataka nikusifie lkn umeharibu mwishoni, comment yako ya kwanza nimeipenda kweli imekaa vizuri.
ReplyDeleteIsipokuwa kila mara umekuwa unataka kuwatumia pesa wadau wa UK kwa njia ya Mpess. Jaribu kufanya utafiti katika hilo au waulize wadua kuhusu hiyo MPESSA yako na huku UK wapi na wapi unahitaji msasa kidogo mkuu.
Mdau UK.
Jamani hizi Pembea za "KIWANJA CHA KUFURAHISHIA WATOTO " a.k.a. "KARIAKOO" hakina hadhi yake tena! Mana si kama kilivyokuwa kipya, hizo Pembea sasa hivi ni 'tetanus' tupu kwa uchakavu uliopelekea kufanya kutu (rust).
ReplyDeleteJamani hiki kiwanja cha Kariakoo ni sawa na kuwakumbusha wale watoto wa zama hizo 'kilio matangani'. Khasa hili pembea la 'vikapu' binafsi linanikumbusha mbali sana, mana ndo ukati huo kiwanja hicho kimefunguliwa rasmi kila kitu humo ndani kuanzia Vigari, Farasi, Mabeseni, Ndege, n.k. vilikuwa vipyaaa na upya wake! Leo hebu patembelee uwanja huo ujionee mwenyewe, pembea takriban zote hazitamaniki kwa uchakavu, hivyo vigari haviruhusiwei tena kufanya kazi, Mabanda yaliyokuwa yakitumika kufanyia burudani mbali mbali na mengine kuuza bidhaa kadha wakadhalika za watoto, sasa karibu yote yamevumbuliwa shughuli za kufanya, mengine yamegeuzwa maofisi n.k. Ila hii yote ni uzembe wa wahusika kushindwa kuki-renovate kiwanja hicho mara kwa mara mpaka kila kitu kinaharibika na kuwa hakifai kabisa mithili ya hiyo M.V.Mapinduzi. Shukran sana Mdau ulotuwekea hizi picha.
naona kila mtu anatapika tu humu ndani hata habari haijasomwa uzuri-imeulizwa muda wa Mapinduzi na Maendeleo haijalishi kama zimezama au la-kwa kipindi hicho zilipokuwa hai
ReplyDeleteNa Mv Maendeleo nasikia inaendelea kutumika bado ila watu wasio na elimu wanaropokwa tu
Mtoa mada orijino
hahaha this guy jamani????? i think kabla ya kuweka comment za mtu mhariri thibitisha kwanza ndio uweke hoja la si hivyo utajiaibisha mhariri wa Blog hii mijitu inakurupuka na kutupotezea muda kusoma. zungumza about Cameron alokwambieni muowane huko na laana zenu...
ReplyDeleteZebedayo huna lolote,unataka kuja UK.Wewe kula vumbi tu huko.
ReplyDeleteMdau hapa Miunda
ReplyDeleteAh juzi tu nilikuweko zanzibar kabla ya ramadhani,humo ndani kariakoo ndio walevi na wakabaji na wauza miili ,munasema hicho kiwanja hakitumiki subiri ifiki wakati wa skukuu ya iddi mutaona.