Ankal na wadau wote wa globu ya jamii. 
Pokeeni salamu zangu kutoka maeneo ya sinza jijini Dar. Ama baada ya yote ningependa kujadili nanyi mawili machache ambayo nadhani ni muhimu kwetu kama watanzania

Nilienda TRA ku-renew road licence ya gari yangu dogo Toyota-Vitz kama ninavyofanya kila mwaka. Katika kufanya kwangu malipo, Vile vile nililazimika kulipia huduma ya moto ambayo zamani nilikuwa nikiilipia Tsh 3,000/ leo hii hiyo huduma imepanda hadi 40,000/ kwenda juu. Malipo yanaongezeka kulingana na ukubwa wa injini ya gari lako

haya malipo ya moto yaliongekeza kwa 1,400%. sijui ni mfumko wa bei au tatizo lilikuwa wapi. Hata zimbabwe sidhani wamefikia hapa

Waungwana swali langu ni kwamba, Jee hii huduma ya Fire ya nini wakati hatuna hata zima moto moja kwenye maeneo mengi ya jiji letu? Vijini ambako hatuna magari ya zima moto hii huduma tunayoilipia gharama kubwa hivi itawasaidiaje?

Hizi gharama zilipitishwa ndani ya bunge letu. Sijui waheshimiwa pale dodoma waliliona hili au ndo yale yanayowakumba wavuja jasho ambayo waheshimiwa hawajali?

Naomba maoni yenu kuhusiana na hizi gharama kwa sababu bei inapopandishwa, ina maana kwamba gharama za uendeshaji zimepanda na huduma zinazofuatia zinakuwa bora zaidi. Sijui hii ya moto imekaaje

mdau
Dar es salaam

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 39 mpaka sasa

  1. Kaka hili ni tatizo mimi sijawahi kuilipia tangia wameanzisha hayo mambo ya fire sijui vitu gani. Kwanza hata sijui maana yake ni nini. Nasikia kweli uwezikurenew road license mpaka ulipie hiyo. Hii ni wizi kawaida ukiwa unaona kama unavyoweza kwenda Kariakoo na ukachukuliwa hela mfukoni. Ila nasikia kwa Vitz ni Tshs. 20,000/=.
    Pole sana kaka, nchi hii ndivyo ilivyo....Ensi yahwa balumuna!

    ReplyDelete
  2. Lipeni kodi acheni kulalamika. Sasa kama hakuna gari la zimamoto kodi inayokusanywa si ndio itagharimia kununua zimamoto jipya/mapya?

    ReplyDelete
  3. SASA MBONA UNACHANGANYA GHARAMA ZA FIRE NA TRA? WAO WANAHUSIKA VIPI HAPO

    ReplyDelete
  4. Tatizo mawasiliano....imagine unapewa surprise ya 40k dirishani TRA si vyema

    ReplyDelete
  5. Kuna nchi zingine unalipishwa school bus tax ,hata kama hujazaa (eti Mabasi yanayopeleka watoto mashuleni) na wewe unayelipishwa huna mke wala mchumba. Jamani twendeni taratibu. Elfu 40 ngapi umezipoteza kwenye bar ?? au kumnunulia Aisha kangha,hapo aaa!! shwari kabisa hulalamiki,lakini ukiambiwa changia gari la fire ?? oupalai !!!!!! Kilio kikuubwa. Jamani au unataka hao wabeba vijibox watuone tuna shida ?? wakati tunatesa ile mbaya. Waulize watu wa UK,kuna barabara ukipita kila siku lazima ulipie, ndiyo maana wanasema hapo juu ,lipia gari la fire-hata kama wewe hutalitumia mwenzio litamuokoa. Wanasema Tenda wema nenda zako. Zebedayo msema kweli

    ReplyDelete
  6. Wewe unaesema kodi inayokusanywa ndio italipia kununua zima moto ni pumba head sbb raiya sio kazi yake kuchangia kununua zima moto wala hahusiani na kununua zima moto!ulaya watu hawachangii wala kulipia zima moto ukishalipia insurence yako inatosha!tatizo la sisi watanzania niwajinga sana mtanzania mwenzetu akitowa hoja lazima ubishe na umkandamize hatupeani saport kabisa hii point ndio aloitowa meneja wa Globalpublisher juzi katika bifu lake na yule msanii wa uganda na ndio maana tunakuwa chini kila siku!Raiya yuko na haki yakujuwa pesa anayokatwa inafanyiwa nini katika maendeleo sio makodi ambayo hayana kichwa wala miguu!unajuwa viongozi wangapi wako na miradi yao kwa kutumia mgongo wa serikali na watakula mpaka vitukuu vyao!sio haki yakumlipisha haki muuza maandazi wakati wewe serikali unatakiwa umsaidie muuza maandazi ajikwamue sbb huwezi kumpa kazi!Watanzania mjue mbele kiza leo kama mtu ataambiwa alipe kodi 1400% na raiya wanaitikia tu na hakuna chochote anachofanyiwa kizuri basi kama ni miti shamba iko siku itaisha nguvu!

    ReplyDelete
  7. Wizi mtupu! Unyanyasaji pia! Majizi yatajenga mahekalu kwa pesa hizo. Ndio maana mapambano ya kukwepa kulipan kodi lazima yaendelee. Hii ni kama kodi ya maendeleo enzi zileeeeeeeee!

    ReplyDelete
  8. Ndugu yangu uliyeleta hii hoja pole sana kwani hiyo ndo Tanzania. Wengi tumefanyiwa unyama huu. Niliwahi kuugomea wakazuia gari yangu nisiondoke nayo. Jambo la ajabu ni kwamba hakuna elimu iliyowahi kutolewa kwa raia kuhusiana na jambo hili. Nilijaribu kuuliza kwa nini elimu haijatolewa kwa umaa kabla ya kulazimishia jambo kama hilo nikaambiwa wao wanatekeleza sheria za wakubwa zao. Na hapo hapo nikadokezwa na mmoja wao kwamba hilo ni dili la wakubwa huko serikalini. Tanzania inakoelekea ni kubaya kwani viongozi hawajali wanyonge hata kidogo. LAKINI MWISHO WAO UTAFIKA. SAUTI YA WENGI NI SAUTI YA MUNGU.

    ReplyDelete
  9. Hapa kuna tatizo, pesa nyingi watatnzania tunazolipia zinaishia kwenye mifuko ya watu, hizo gharama za fire ni za nini, ndiyo nasikia leo, mbona magari yanungua na kuteketea kila siku huko Dar watu wanabaki wakishangaa. Tanzania kuna uozo wa kila aina. Hao wabunge haya hayawahusu, wanasubiri kuchapa usingizi tu bungeni. Hii siyo sawa. Na wewe hapo juu unayesema lipeni kodi acha kulalamika, tunahitaji maelezo ya kutosheleza, pesa inapatikana kwa shida kwa hiyo inatakiwa itolewe maelezo

    ReplyDelete
  10. Serikali na wabunge tuliowatuma wanalala tu Bungeni kusubiri posho. Hawauni uozo huu. Leo wametoa kwenye magazeti kabisa tangazo.Hata hawa wanasheria wetu sijui wako wapi wasiipeleke Serikali mahakamani kwa wizi huu wa wazi wazi.

    Wabongo tumelala na tutalipa tu mpende msipende.

    Hovyooooo!!!!

    ReplyDelete
  11. Ukisikia hii ndio Bongo Tambarale!

    Nadhani Maafisa wa Mamlaka ya Kodi wanasoma zaidi Ujasiriamali kuliko huduma za Jamii na makusanyo ya Kodi kwa manufaa ya Wananchi.

    Hivi mpaka leo hamfahamu ya kuwa
    TRA na SACCOS ni kitu kimoja?

    ReplyDelete
  12. Ndugu zangu wadau, hizi gharama zimetangazwa kwenye magazeti nchini siku za karibuni. Kwa kulipia TRA ni sawa kabisa. TRA ni sehemu ya kukusanyia kodi kwa maendeleo ya nchi yetu. Hapo ndipo penyewe na sio barabarani kama ambavyo mimi walinikamata mwaka jana barabara ya Msamvu na kudaiwa kwani wakati mwingine unakutwa huna pesa au zikaingia mifukoni mwa wakusanyaji wasiopaswa. TULIPE KODI ndipo tudai huduma bora vijijini na mijini.
    Tena tangazo lilielekeza kwamba baada ya kulipia, usisahau kulipeleka gari lako Ofisi yoyote ya Fire ukiwa na receipt ya malipo kwa ukaguzi na kupata Fire Extinguisher ya size ya gari lako. Hayo ndiyo maboresho. Kama nimekosea mahali, mwenye nakala ya tangazo arekebishe kwa nia nzuri tuu.

    ReplyDelete
  13. Kwa kweli nami hili jambo nimelisikia mimi mwaka jana nilikwenda pale lumumba nikakata Siticker ya Tsh. 5000 gari Aina ya starlet yenye 1300cc.lakini mwaka huu nimesikia tsh.20,000/= kwa gari hilo tena wanadai kama hujalipia tangu zoezi hili lilipoanza utatozwa kwa miaka yote.Kwa sasa unalipia TRA ya hapa samora.Kwa kweli nami bado natafakari sana jambo hili mbona imepanda hivyo?.wao wanadhani mwenye gari yeyote ni tajiri?.Uonevu huu haufai kabisa kwa Serikali yetu hii.Angalia NSSF sasa kivumbi!!!!.

    ReplyDelete
  14. Mdau soma gazeti la The Guardian la July 30,2012 ukurasa Viii kuna tangazo wametoa pia wametangaza kwenye radio kipindi kirefu labda kama kawaida yetu watz si watu wa kusikiliza radio. Kwa 40,000/= ni ya gari ya CC 2501 na kuendelea, sasa hiyo VITZ yako ni CC ngapi? maana wamesema hivi, KUANZIA JULY 2012 HUDUMA ZA FIRE ZITAKUWA ZINALIPIWA TRA WAKATI WA KU-RENEW NA BEI NI;
    CC 1 - CC 500 10,000/=
    CC 501 - CC 1500 20,000/=
    CC 1501 - CC 2500 30,000/=
    CC 2501 na kuendelea 40,000/=
    My take: Unajua wachumi wetu wa serikali wanaangalia pale ambapo kuna mapato ya wazi na wanashindwa kubuni vyanzo vipya vya mapato mfano mzuri kuna wanamuziki, waigizaji ambao wakiwasupport watavuna pia kuna wamilki wa nyumba wanachukua hela nyingi lakini kodi hakuna lakini ngoja uwe na gari au unafanya kazi kwa kuwa ni rahisi kukupata hapo inakuwa kasheshe. Naunga mkono kodi lakini ziangalie hali halisi pia waboreshe kwanza huduma za zimamoto kabla ya kupandisha. HIYO 40,000 kwa VITZ nahisi kama wamekuibia unless VITZ yako iwe na CC zaidi ya CC 2501

    ReplyDelete
  15. Naunga mkono kuwa tatizo ni mawasiliano. Ghafla wanakutega kwa elfu 40, hii budget sio rahisi kwa watu wengi watanzania, wengine mmejisahau mnaishi kwenye 2 percent ya watanzania. Wangetutaharifu nasisi tuwaulize hii yote ya nini. Je, ni sehemu pekee ya kupata pesa za ununuaji magari ya fire? au ni kuchangia ongezeko la posho? kumbuka ukiona minus imeongezeka lazima kunasehemu plus itaongezwa ili kufidia.

    ReplyDelete
  16. Jamani mi sikatai kulipa, ila tunapolipa tunatakiwa kupewa hizo fire extinguisher. Unalipa then ukifika mtaani unauziwa nyingine. Huu sio wizi.

    ReplyDelete
  17. Uncle inashangaza sana sijui nchi yeti inakwenda wapi, mi motor vehicle licence ilikuwa imekwisha kama miezi miwili iliyopita ikabidi nilipe na penati, bahati mbaya siku nalipia ndio utaratibu wa fire ulikuwa umeletwa TRA ilibidi nilipe kwa gari yangu 187500 ikiwa na penati pamoja na 30000 za fire nikaambiwa nije nichukue karatasi zangu kesho yake, kurudi nikakuta nimeongezewa 7500 eti penati ya faya ilioanza kulipiwa TRA siku nilipokuwa nikilipia. Tunakwenda wapi tanzania hii, hata stika hupati. Haya tutafika tu

    ReplyDelete
  18. Watu wanaongea sana tu hivi kale kamtungi ka kuzima moto katafua dafu kweli gari ikiungua ama ni miradi ya watu!!!!!???...mulika mwizi...

    ReplyDelete
  19. kuuliza siyo ujinga ni sehemu ya kujua mengi, nijuavyo mimi,hiyo ya fire huko TRA siyo sehemu yake ila wenyewe ni mambo ya ndani kitengo cha zima moto na wana viwango maalum vilivyowekwa kwa malipo ya kila gari kuna 5000 hadi 50000 na zidi kulingana na ukubwa wa gari. Sasa hiyo ya kulipishwa huko TRA huenda kuna mabadiliko ya kiutendaji ulichokose ni kutokuwauliza maofisa wa TRA ili wakufafanuliye kama kuna kodi mpya kwa kuwa huu ni mwaka mpya wa serikali kuna baadhi ya kodi huongezwa na nyingine hufutwa na mamlaka husika na lazima yawepo maelezo kwa watoa kodi na wakusanyaji. Ungeuliza fire hii ni ipi na ni ya nini siyo kuondoka na kuanza kunungunika pembeni huwezi kulijenga taifa lako kwa kusemea pembeni jitkeze kwa wahusika wakuweke sawa ili uwaelimishe na wengine. Samahani mdau si dhamirii kukukwaza katika hili ila kuwekana sawa sote hii ni nchi yetu hatuna pa kwenda tusaidiyane kuijenga.

    ReplyDelete
  20. Tusishangae sana hii ndio Bongo land. Kwani ule mtungi wa kuzimia moto ndani ya gari utazima nini gari ikiwaka moto? ndio mjue miradi ya watu hiyo!!!

    Nasikia vibali vya wageni ni Dola 2000/= na mbado!!!! tusubirie mengine. Mshahara sijui lini!!!

    ReplyDelete
  21. kama huwezi lipia gharama za kuwa na gari basi panda usafiri wa umma kama daladala au endesha pikipiki/baiskeli.

    huku ulaya kuna gharama kibao za kuwa na gari lako binafsi mfano congestion charges,gari kuhakikiwa ubora kila baada ya kipindi fulani(MOT), parking charges kila sehemu hata vichochoroni.

    Hivyo mdau nashauri gari lipaki nyumbani na tumia usafiri mwingine kwa shughuli zako maana kuwa na gari gharama huziwezi.

    Mdau
    Mpanda Usafiri wa Umma ingawa na gari.
    Jijini London

    ReplyDelete
  22. Kaka nchii hii ndivyo ilivyo,na hakuna hata anayetetea hili,je huko uk wanalipia fire?wadau wauk tupeni data kama na nyie mnalipia fire,kwani sisi tumerithi sheria za uingereza,kwa kweli tunanyonywa sana watanzania.Usipokagulisha gari nje unalipia TBS MIllioni,unacholipia ni ile barua a4,kweli this is a day light robbery.Tutanyonywa mpaka lini jamani?Eddy DSM

    ReplyDelete
  23. MDAU WA 10:55AM AGOSTI 1,2012 SIJUI UPO NCHI GGANI ULAYA AMBAKO UKILIPA INSURANCE BASI GARI LIPO BARABARANI.
    SI TULIOPO UK, GARI LINALIPIWA BIMA, KODI YA BARABARA (ROAD TAX) KULINGANA NA UKUBWA WA INJINI, NA PIA LAZIMA IKAGULIWE UBOR KILA MWAKA (KWA GARI ZENYE UMRI WA MIAKA 3 NA KUENDELEA) IKIWA NI MOJA YA MASHARTI ILI GARI LIWEPO BARABARANI.
    SIKU HIZI HATA KAMA GARI LAKO BOVU NA HUJASIMAMISHA USAJILI DVLA (SORN), LAZIMA ULIPIE BIMA VINGINEVYO LITASOMBWA NA COUNCIL UKAGOMBOE/LIPONDWEPONDWE ENDAPO UTASHINDWA KUGOMBOA.
    KUHUSU KODI YA MOTO, HIYO HULIPWA KWENYE KODI YA KILA MWEZI INAJULIKAKANA KAMA COUNCIL TAX NA HULIPWA KULINGANA NA UBORA W NYUMBA/ENEO UNALOISHI.(BAND TAXES).
    NDANI YA HIYO COUNCIL TAX AMBAYO MIMI NALIPA £129/MONTH, KUNA FEDHA ZA POLISI, FIRE, MOTO NA SHULE.
    ISITOSHE KUNA ADA YA MAJI AMBAYO NDANI YAKE KUNA MAJI SAFI NA MACHAFU. HIYO NALIPA KILA MWEZI £41.
    UKIACHILIA MBALI YA KODI NA ADA HIZO, PIA KUNA DIRECT TAX AMBAYO WAFANYAKAZI WOTE LAZIMA WALIPE (INCOME TAX)+ NATIONAL INSURANCE EARNING (NI) AMBAYO JUMLA NI 32% YA KIPATO CHANGU. IWE KWA WIKI, MWEZI LAKINI JAMAA WANALAMBA KWA NGUVU ZOTE.
    MBALI YA KODI HIZI, KUNA INDIRECT TAX TUNAYLIPA UNAPONUNUA BIDHAA POPOTE PALE ISIPOKUWA SOKONI TU HUKO NDIKO KODI IMPONEA CHUPUCHUPU.
    JAMAA ANAELALAMIKA KUHUSU FIRE TAX TOKA 3000SHS HADI 40000SHS ANA HAKI KWANI ANAHISI KAMA HIZO FEDHA ZINAISHIA KWENYE MIFUKO YA WAJANJA.
    NCHI IMEJAA RUSHWA. VIONGOZI WANAIGA MAMBO YA KODI YA NJE YA NCHI KUINGIZIA SERIKALI KIPATO LAKINI HAKUNA UTARATIBU MAALUM WALA MWANANCHI WA KAWAIDA HAONI MAENDELEO YAKE.
    KUNA MENGI YA AIBU YANAYOTENDEKA HUKO TAMBARARENI KWENU AMBAYO YANAFANYA HATA WAHISANI SIKU HIZI KUKUNJA MIKONO BAADA KUONA FEDHA ZAO ZINAISHIA MIKONONI MWA WACHACHE.
    KODI NILIPAYO HUKU SIWEZI KULALAMIKA KWANI INASAIDIA MTOTO KUSOMA BURE, FAMILY KUPA MATIBABU BURE, HATA NIKISUKUMWA AU KUTISHIWA MBWA, NAITA POLISI WITHIN A SECONDS WAMEFIKA NA KUMTAFUTA MTUHUMIWA.
    NIKIWA NA KESI MAHAKAMANI, WAKILI ANALIPWA NA SERIKALI (LEGAL AID). HIYO NI KODI AMBAYO NALIPA NA FAIDA YAKE NAIONA WAZIWAZI. SIYO BONGOOOOOO. WIZI KUANZIA MUUZA VITUMBUA MPAKA NGAZI ZA JUU.
    ND'O MAANA TUNA VIONGOZI TANGU ENZI ZA UHURU HADI SASA. EAASY MONEY TKA KWA WAJINGA WAJINGA. HAMNIPATI HUKO NG'OOOOOOOOO. WEZI WAKUBWA NYIEEEEEEEE.

    ReplyDelete
  24. BONGOOOO WATU WEZI SAAAAAAANA. MNAJULIKANA KAMA NAIJA 2 KWENYE MITANDAO YA TRIP ADVISOR. HAMNA HAYA HATA CHEMBE. MTU ANAIBA HATA NGUO YAKE ALOIANIKA UWANI.
    YAANI KAANIKA NGUO UWANI, IMEKAUKA ANATAKA APIGE NA PASI YAKE YA MKAA, BASI ATANYATA KWENDA KUICHUKUA HALAFU ANATOKA BARUTI...NDANIIII. HEMA KAMA BADGERS ALOKOSWA NA LORI BARABARANI. KISA...JUST PRACTISING BEFORE DOING IT FOR REAL!!! ENH! F@@K N' HELL

    ReplyDelete
  25. Kha TRA kiboko wazee bongoland mi nilienda kufuatilia document pale mwenge TRA ambako kuna miundombinu mizuri ilikuwa ijumaa na nilikuwa na haja sana na hiyo document.Nilienda dirishani mtumishi wa TRA akasema processing yake haiwezekani kwani nimechelewa.Nikamwomba sana ili anisaidie akang'aka akasema system ndo inafanya kazi akanihakikishia kuwa hiyo haiwezekani kujaza data na kuiprint.Nikaamini na kuondoka.Nikaenda pale nje kuna tumigahawa huku nimenyong'onyea na kuridhika.Mara jamaa mmoja wakati tunaongea akatuuliza kulikoni.akanambia nimpe 5000 nikampa akaenda nikiamini kabisa hawezi ndani ya dakika tano alirudi na document.sikuamini kabisa kwani wanamjua sana kama ndo anaewafanyia kazi.anakabidhi document huku amekunjia elfu Tano na siku zinaenda.Thats true story imenitokea ninaecomment

    ReplyDelete
  26. Weww Mdau Mpanda Usafiri wa Umma London....
    Usibabaishe watu kwa kulinganisha public transport ya Ulaya na ya TZ.
    Wengi tumeishi nchi kadhaa duniani, nyingi zilizoendelea zina sera ya ku discourage matumizi ya magari binafsi... Singapore is a prime example.
    Lakini huduma za public transport ni first class.
    Mie binafsi nisingependa kuendesha/kumiliki gari TZ hususan 4WD vehicle kama huduma na public roads zingekuwa bora.
    Kulipizana gharama za huduma hewa ni utapeli wa serikali kwa wananchi. Siajabu kuna exemptions lukuki za magari ya vizito humo.
    It's disgusting to be forced to pay for a non-existent service....... and without recourse to contest or protest it.

    ReplyDelete
  27. Samahani si mahali pake ila system ya Bongo inakera.Nashangaa jinsi PCB inavyofanya kazi.Zoezi la leseni za magari ni sehemu nyingine hizo departments zimekula pesa za walalahoi kama mchezo.Kila mmoja atakumbuka swala la leseni za madeleva lilivyo leta pressure.Pale TRA kwenye jengo la kisasa mapolisi waliokuwa wakiratibu ni hatari sana.Basi ukienda kuna ukaguzi wa utitiri wa vitu mojawapo likiwa cheti cha macho ila cha kushangaza alternative ya cheti ni sh 5000 Basi watu walikuwa wanapeleka na ukikunjia elfu tano trafic utamsikia anaguna hata haulizi vitu vingine vya msingi hayo nimeshuhudia kwa macho.TZ bado rushwa ni kero.

    ReplyDelete
  28. Hivi hatujailewa Serikali yetu, katika uchumi, serikali inapooamu kuwafanya wananchi wake maskini huweka sheria na kodi za ajabu ajabu tu ili mradi kumfilisi mwananchi wa kawaida. Na Bunge lisipoona hiyo hupitisha na kuwa sheria. Serikali yetu imeamua kutufanya maskini na wanafanikiwa.Je kodi ya fire ni bima? inamsaidiaje mmiliki wa gari kama itatokea limeungua hali gharama za fire zimelipwa?

    ReplyDelete
  29. Serikali ina haki ya kutoza kodi halali. Wananchi wana haki ya kupata huduma. Ndugu yetu ana sababu za msingi kusikitishwa na yaliyomkuta. Huwezi kuhalalisha kupandisha kodi kwa asilimia alfu kutoka mwaka mmoja mpaka mwingine. Kadhalika pamoja na kutozwa kodi kubwa, huduma ya zimamoto ni ya kusuasua kiasi cha kuleta maswali kama hiyo kodi kweli inaenda kuimarisha huduma za zimamoto au inaishia kwenye kulipia safari za viongozi ng'ambo pamoja na posho za vikao. Tatizo tumepoteza kuaminiana. Watunga sheria wetu wanahusishwa na rushwa na wanatunga sheria za kuwapa misamaha ya kodi mbalimbali.
    Watanzania inabidi tudai mabadiliko. Status Quo inatuumiza sasa hivi.

    ReplyDelete
  30. WADAU NATARAJI SERIKALI AU TRA WATAONA MALALAMIKO YA WANANCHI.

    NAOMBA MWENYE KUJUA/ AUR TRA WENYEWE KAMA NIFANYEJE KAMA GARI YANGU IMEPATA AJALI NA HAITATENGENEZEKA KWA MUDA MREFU. NI KATIKA KULIPIA ROAD LICENCE. KWA KUWA IN ACTUAL SENSE SITAKUWA BARBARANI. KULE UK UNADECLARE, ALAFU8 IKIRUDI BARBARANI UNAANZA KULIPIA

    NAOMBA MSAADA

    ReplyDelete
  31. Naona Tanzania na baadhi ya watanzania ni uozo. Mtu kauliza maanz yake anataka kujua, wenye kujua wametoa maelezo na ference nzuri tu ..wewe unayekaa ulaya huna unalolijua kuhusu ulaya na nchi yako.
    Ongezeko la 1.500 % sijawahi sikia , na kwa ubora gani wa huduma hiyo ya fire ?
    Kwa vile wakubwa wameshika mpini wa kisu ..hatuna la kufanya zaidi ya kulipa na kuendelea kupiga kelele.
    Wewe uliye ulaya na matusi yako..endelea kuosha vyoo vya wazungu..ipo siku utarudi home na utajua tunazungumzia nini .
    Mwenye post: pole sana..ipo siku kitaeleweka.

    ReplyDelete
  32. Bashiri Omari kulipia TRA ni maamuzi yaliyofanyika kulipia zote ili kuepuka usumbufu kwa hiyo kama gari lako unalipa laki moja maana yake utalipa laki moja na ishirini alafu TRA hiyo twenty wanaiingiza kwenye akaunt ya fire

    ReplyDelete
  33. TRA ni wezi tu,mimi nina nyumba ya ghorofa ndogo yenye vyumba vitatu vya kulala ,na shemeji yangu ana nyumba kubwa ya chini yenye vyumba 5 vya kulala maeneo ya mbezi,cha kushangaza mimi nalipizwa sh. 80,000/= ya propety tax kila mwaka,Lakini shemeji yangu analipa sh. 10,000/= tu na eneo lake na nyumba yake ni kubwa sana kushinda yangu,kwa kuwa nyumba yangu ni ghorofa basi ni kosa inanibidi nilipie mara nane yake ya kodi!Je hiyo ni sawa jamani isitoshe mie ni mjane na nimeachiwa watoto wangu wawili,Mshahara wangu unakimu mahitaji yetu tu,Likija suala la kulipia propety tax ya nyumba huwa inakuwa tatizo kidogo,Lakini TRA hawaelewi hilo.

    ReplyDelete
  34. Mwenye gari haitaji kulipa kodi ya fire maana tayari kashalipia bima. Wenye kuhitaji kodi ya fire ni wenye nyumba. Lakini serikali imeogopa kuweka sera ya kulipa fire kwa wenye majumba maana kura watakosa. Sasa ndio maana wameingiziwa wenye magari ambao wengi wao wana mshiko hawajali kulipa lipa.

    ReplyDelete
  35. SIKU BONGOLALALA WATAPOAMKA NDIPO HAO VIONGOZI WEZI WEZI WATAPOONA CHA MOTO.
    WABONGO WOTE UOZA. MANENO LIBYA, EGYPT, TUNISIA, BAHRAIN, SYRIA HUKO HALALI MTU.
    MTU KUOSHA CHOO AU KUZOA TAKA, KUFAGIA BARABARA NII KAZI NA INATHAMINIWA NA KILA MTU TOKA MALKIA HADI KINYANKELA. HUKU HAONEWI MTU.
    USIONE MTU ANAFANYA KAZI YA KUSAFISHA CHOO ETI UKAMNYANYASA. UTAMLIPA HELA NA USIPOANGALIA UTASUNDW JELA.
    KUNA BONDIA MONROE BINGWA WA MASUMBWI DUNIANI ANAISHI NOTTINGHAM, KAZI YAKE KUZOA TAKA JIONI YUPO GYM ANAJIFUA. KILA MIEZI 3-6 HUYO PIPANI VEGAS KUZICHAPA.
    KAZI ULAYA KILA MTU ANAHESHIMIKA NA MSHAHARA USIPOANGALIA MNAWEZA KULA SAHANI MOJA KATI YA OFISI NA MUOSHA CHOO AU MPIKA CHAI KANTEEN.
    KWANI BILA MSAFISHA CHOO, HUWEZI KUINGIA CHOONI WEWE! WATU HAWAKOJOI MSITUNI AU VICHOCHORONI KAMA KWENU TAMBARARE KILA KONA. KOJOA KESHO KWENYE CCTV UNASAKWA KIZIMBANI JELA/FINE.
    TATIZO LA WABONGO HASA WALE WEZI WANAOJIFANYA JUU ZAIDI WANALELEWA NA WAKUBWA.
    KINGINE NI SISI WANANCHI TUNASHINDWA KUWA NA MSIMAMO. KWA NINI TUSIGOME KUTOA RUSHWA NA BADALA YAKE TUWARIPOTI TAKUKURU ILI WANASWE! HAO TAKUKURU WENYWEWE ND'O WALA RUSHWA WAKUBWA...KELB WEE.
    NTAKUZUKIA TENA NGOJA NLALE KESHO BOKSI. OVATIME £179.88 AFTER TAX.......KERCHING

    ReplyDelete
  36. Wewe kwanza si mtanzania sms zako unasema bongo kwenu sasa siukae huko ya huku ya nn mshamba wewe mkataa kwao mtumwa huko unatumikishwa ka punda na kodi hiyo ndio inajenga hizo nchi za watu ungejituma nyumbani ili ujenge nchi yako fala wewe kwani huku hakuna vyoo vya kuosha mshamba mkubwa wewe niko nje ya nchi but mm mtanzania na kamwe siwezi ponda nchi yangu nitachangia kutafuta solution sio kusema bongo wezi wote wewe ndio mwizi unajiita mtanzania huku ukienda huko unabadilika sasa kaa huko bongo hakuna dual sitizen ship ole wako ningekujua na ulanyage bongo nyie ndio wenye passport feki

    ReplyDelete
  37. Wewe kwanza si mtanzania sms zako unasema bongo kwenu sasa siukae huko ya huku ya nn mshamba wewe mkataa kwao mtumwa huko unatumikishwa ka punda na kodi hiyo ndio inajenga hizo nchi za watu ungejituma nyumbani ili ujenge nchi yako fala wewe kwani huku hakuna vyoo vya kuosha mshamba mkubwa wewe niko nje ya nchi but mm mtanzania na kamwe siwezi ponda nchi yangu nitachangia kutafuta solution sio kusema bongo wezi wote wewe ndio mwizi unajiita mtanzania huku ukienda huko unabadilika sasa kaa huko bongo hakuna dual sitizen ship ole wako ningekujua na ulanyage bongo nyie ndio wenye passport feki

    ReplyDelete
  38. Wew mkimbizi hii sio sehem yako kama bongo kwetu kinachokuleta humu nn mkataa kwao mtumwa ubabaguliwa huko hujijui jenga nchi yako sio inasifia ujinga hapa lipa kodi ujenge huko kwakiwa huna kwenu

    ReplyDelete
  39. unatumika ka punda huku nyumbani kaxi hautaki mwizi ni wewe ka ushakuwa raia wa uk kinacjokileta kufuatiloa ya bongo nn katupe hoyo pasd frki maana ukija bongo na hiyo ua green ole wako hii ni tanzania mpya

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...