Kwa niaba ya Mtandao wa wanataaluma Tanzania (Tanzania Professionals Network- TPN) nachukua nafasi hii kumpongeza Mzalendo Asah Mwambene (41) kwa kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo).Kabla ya uteuzi huu Mwambene alikuwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano , Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, pia aliwahi kufanya kazi TSN.
Mwambene ni Mzalendo wa kweli na ni mdau wetu muhimu katika kuleta maendeleo endelevu Tanzania na amekuwa akifuatilia na kushiriki shughuli zetu za TPN.
Ni matumaini yetu kuwa utatimiza wajibu wako vizuri na kwa weledi wa hali ya juu kwa kuzingatia misingi ya taaluma ya habari kwa manufaa ya watanzania wote.
Kila la heri na Mungu akubariki.
PHARES MAGESA
RAIS - TPN


Kwanza naomba kuungana na wengine kutoa hongera
ReplyDeletePili naomba sana wanaoshona nguo zenye bendera ya Taifa wazingatie mpangilio wa rangi, kama sijakosea Blue hukaa chini, hata ukiangalia bendera inayopepea Blue iko chini. Maelezo zaidi yatolewe na wadau wanaojua kwa undani kuelezea hili.