Kwa niaba ya Mtandao wa wanataaluma Tanzania (Tanzania Professionals Network- TPN) nachukua nafasi hii kumpongeza Mzalendo Asah Mwambene (41) kwa kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo).

Kabla ya uteuzi huu Mwambene alikuwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano , Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, pia aliwahi kufanya kazi TSN.

Mwambene ni Mzalendo wa kweli na ni mdau wetu muhimu katika kuleta maendeleo endelevu Tanzania na amekuwa akifuatilia na kushiriki shughuli zetu za TPN.

Ni matumaini yetu kuwa utatimiza wajibu wako vizuri na kwa weledi wa hali ya juu kwa kuzingatia misingi ya taaluma ya habari kwa manufaa ya watanzania  wote.

Kila la heri na Mungu akubariki.

PHARES MAGESA
RAIS - TPN

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Kwanza naomba kuungana na wengine kutoa hongera
    Pili naomba sana wanaoshona nguo zenye bendera ya Taifa wazingatie mpangilio wa rangi, kama sijakosea Blue hukaa chini, hata ukiangalia bendera inayopepea Blue iko chini. Maelezo zaidi yatolewe na wadau wanaojua kwa undani kuelezea hili.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...