Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Clouds Media Group,Joseph Kusaga akizungumza na Kiongozi Mstaafu wa Freemasons Afrika Mashariki,Sir Andy Chande ofisini kwake mapema leo mjengoni hapo,ambapo baadaye pia alifanya ziara fupi na kujionea vitengo mbalimbali vya kampuni hiyo namna ambavyo vinafanya kazi.
Mazungumzo yakiendelea ya hapa na pale.
Kiongozi Mstaafu wa Freemasons Afrika Mashariki,Sir Andy Chande akisikiliza jambo kwa umakini.
Mkurugenzi wa Clouds Media Group,Joseph Kusaga akiagana na wageni wake mara baada ya kufanya mazungumzo nao mapema leo,kwenye ofisi za kampuni hiyo,Mikocheni jijini Dar.
Mkurugenzi wa Clouds Media Group,Joseph Kusaga akiagana na mgeni wake Kiongozi Mstaafu wa Freemasons Afrika Mashariki,Sir Andy Chande.
Kiongozi Mstaafu wa Freemasons Afrika Mashariki,Sir Andy Chande akiondoka taratiibu mjengoni Clouds Media Group mapema leo mara baada ya kufanya ziara fupi kwenye ofisi hizo na kujionea mambo lukuki yanayofanywa na kampuni hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Kiongozi mstaafu wa freemasons Afrika Mashariki. Imerudiwa mpaka inachusha kusoma. Tunajua freemasons wapo na kwetu wengine si jambo la kutuhangaisha akili zetu.

    sesophy

    ReplyDelete
  2. Wabongo bwana.Freemasonswapo krne kadhaa lkn wabongo wakipata jambo inakuwa tabu kila kona.Watu wenye kufatilia mambo kwa umakini wanajua uwepo wa Fremes siku nyingi na nini wanafanya na wla hatutegemei kumsikia Chande ndio atufahamishe bcoz as usual atakachofanya i kile kile wanachotumia kuficha agenda zao na kusema ni Charity Organization,uwongo mtupu.We know them in and out.

    ReplyDelete
  3. How and what do you know about Freemasonsuniformed idiot???
    Yaani ninashangazwa kweli na ushamba na upumbavu wa Wabongo!!!! It's disgusting!!

    Someni, oneni, sikieni na elemikeni jamani.
    Otherwise we Tanzanians we will forever remain East Africa's leading idiots.....What a shame!

    ReplyDelete
  4. KWANI KIONGOZI WA SASA WA FREEMANSON NI NANI?

    ReplyDelete
  5. Acheni ujinga wenu nyie anony. wa kwanza hadi wa tatu! kama mnajua kuhusu freemansos tuelezeni tujue ukweli sio kulaumu kwa kutokujua kwetu.
    Tuambieni nini idiology yao ili tuwe macho nao na sio na nyie kutuchanganya! pambaf nyie

    ReplyDelete
  6. Katika maendeleo ya upataji habari tuliyo nayo sasa hivi usitegemee kuambiwa. Vyanzo vya habari ni vingi sana. Mnasubiri kuambiwa tu. Hao watu ni waovu wakubwa na atakapokuja kuwapa story zao atakuja kuwadanganya tu na hatasema ukweli. Someni, tatizo ni uvivu wa kusoma. Kila ukweli wa hao jamaa umeanikwa kwenye internet. Tatizo interenet inatumika tu kuangalia ngono, kutafuta wanawake/wanaume mtandaoni, kucheza gemu na upuuzi mwingi tu na hamsomi vitu vya maana kama hivyo kujua maadui wa ukweli ni kina nani na nani wako nyuma yao kuhakikisha wanafanikisha kafara zao.....SOMENI kila kitu kipo msisuburi huyo Chande kuwahadithia atawadanganya tu...

    ReplyDelete
  7. Kalagha BahoAugust 23, 2012

    We Mkibosho, na wengine mnaoshabikia simulizi za kizushi kuhusu Freemasonry mkielewa mnaelewa?

    Maana mwelewa huwa hasubiri kuelezwa, anafanya utafiti wake mwenyewe na anagundua ukweli uko wapi. Hata pale anapokwama maswali anayouliza unakuta yamekwenda shule maana ameshachimbua chimbua kidogo.

    Kiufupi magazeti ya Udaku na wachungaji na mashehe wamesambaza uzushi kibao kuwa Freemasonry ni dini ya kishetani. Kuwa ukijiunga Freemasonry unakuwa tajiri mkubwa mara moja.

    Huo ni uongo. Lengo ni kupotosha umma kwa makusudi wanayoyajua wao.

    Freemasonry ni fraternity au brotherhood ya kawaida tu kwa wale wanaojua fraternity na brotherhood ni vitu gani. Na ina historia ndeeeefu sana zaidi ya karne 10, kwa hiyo haya mnayoyasikia Bongo yasiwasumbue.

    Fuatilia habari za Freemasons toka nyuma, toka ilikoanzia kwa Wazungu, halafu ndipo mje kuoanisha na uzushi wa wabongo.

    ReplyDelete
  8. wee anony hapo juu fala nn? kama freemason ni fraternity au brotherhood nenda kajiunge bas! au tayari ushajiunga siku nyingi na ushamtoaga mama yako mzazi kafara nini? hiyo ni dini ya kishetani ndio na ni kweli ilianza muda mrefu sana ila siku hizi ndo inazidi kupanuka zaidi tena haswa huku kwetu Africa, kweli wee ndo mkibosho kilaza mkubwa wewe! hovyoooo! endelea kuabudu mashetani moto wa jehanam unakungoja siku ya mwisho.

    ReplyDelete
  9. Sir Chande ameonekana akiwa na watu wengi sana maarufu hapa nchini,kuanzia viongozi wakuu wa kitaifa mpaka wafanyabiasha mashuhuri,mbona hamtuelezi nini wanazungumza,mmekalia freemanson tu??ivi Watanzania tumerogwa na nani kazi kushupalia ujinga tu.

    ReplyDelete

  10. Anon wa aug 23 12:33PM.

    TRUE!!!

    Heheh

    ReplyDelete
  11. Mi ninahisi hao Clouds wanaitangaza hii Free Masons indirectly, maana hii naiona mara ya kadhaa sass yupo huko Clouds mstaafu wa free Masons. Fanya kazi kwa bidii utapata utafanikiwa, kuwa karibu na watu waliofanikiwa na pia punguza starehe na ngono..ukifanya hayo utafanikiwa tu na kuwa na raha maishani, otherwise jiunge na Mafreemasons kwa utajiri wa haraka na masharti ya roho yako kama haufuati masharti.

    ReplyDelete
  12. Ninachoshangaza jamani hulka ya ukaaji.Huyu kuswaga alivyokaa eti nne imekuwa sita hebu kalia kiti kiuungwana wanaopiga nne miguu yao inaruhusu na kiti hakiwi cha chini mno kama cha kwako.Ni kuiga mkao wa JK?

    ReplyDelete
  13. Kalagha BahoAugust 24, 2012

    Thu Aug 23, 01:57:00 PM 2012

    Kwani umeambiwa "fraternity" maana yake "lazima ujiunge"?

    Mbona unaongea kama mtu asiyefikiri kwa umakini?

    Kuna vyama na makundi mangapi hapa nchi ambayo hujui shughuli zao na hujajiunga?

    Ndo maana nikasema kwa wanaoelewa "fraternity" ni nini. Haya mambo wenzetu Ulaya na Marekani ni ya kawaida sana, huku bongo ndio watu wanashangaa shangaa na kudanganyana.

    Tafuta vitabu kama "Freemasonry for dummies" na "The Templar's Code" visome vitakupa mwanga kidogo pa kuanzia.

    Usinunue CD uchwara za msikiti wa kwa Mtoro na wachungaji feki ambao ukiwauliza wamejuaje hawakwambii kinagaubaga.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...