Askari wa Kikosi Cha kutuliza Ghasia FFU wakiweka ulinzi mkali eneo la Kariakoo baada ya kufunga mitaa ya Kongo na ile ya jirani kutokana na kuibuka vurugu zilizotokana na ugonvi wa nyumba ambayo kwa maelezo ya watu wa karibu nyumba hiyo ilikuwa na mgogoro kwa zaidi ya miaka 20 kati ya wamiliki na wapangaji kutokana na kutengeneza hati feki.
Mmoja wa majeruhi kwenye vurugu hizo akiondolewa eneo la soko la Kariakoo baada ya kuanguka chini kutokana na milipuko ya mabomu ya machozi yaliyokuwa yakitumiwa na askari polisi waliofika kutuliza ghasia katika eneo hilo, ambayo iliambatana na mawe yaliyokuwa yakirushwa na vijana waliokua wakitetea upande mmoja wa ugomvi huo.
Wananchi wakizungumza na waandishi wa habari kutoa maoni yao juu ya mgogoro huo.
Kikosi cha kampuni ya Yono Auction Mart iliyopewa tenda ya kusimamia ubomoaji wa nyumba hiyo chini ya ulinzi mkali wa polisi wakiendelea na kazi kwenye nyumba hiyo iliyopo mtaa wa Kongo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. FFU akina Ras Makunja leo! wapo mitaa ya kwao Kariakoo,inaonekana wazi kabisa akina ras makunja na magitaa yao wapo kwa ajili ya muziki mkubwa

    ReplyDelete
  2. sasa akina Ras makunja inakuaje tena hapa? hii ndio adabu gani? mnawechezesha sebene hadi wazazi wenu kariakoo? au ndio zawadi ya Idd Mubarak? sasa magitaa kama haya hapa ni ya nini?

    ReplyDelete
  3. wabongo tutaepuka ili kama kila mwanafamilia atatafuta chake badala ya kusubiri kurithi au kudhulumu. tutafika kweli mambo ya kugombea cha mtu namna hii? unajua kwanini hatufiki mbali? kaka akiwa nacho familia nzima hawafanyi kazi. kama baba tajiri basi wanae hawasomi. huu utamaduni wa kizamani tuachi. ningependa kufananisha na ughaibuni ambako kila mtu ni mtafutaji ila nwawaogopa 'diaspora haters' who assume everything in developed countries is bad.

    ReplyDelete

  4. Anon wa Aug 23, 07:25:00 AM

    "ughaibuni ambako kila mtu ni mtafutaji"

    Na wale wanaoishi kwa welfare nao je?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...