Mheshimiwa Mbunge wa Same Mashariki, Mama Anne Kilango, akikagua kiwanda kipya cha Tangawizi jimboni mwake kwenye Kata ya Mamba-Miamba, kilichojengwa kwa juhudi zake kubwa akiwa Mbunge wa jimbo hilo. Kiwanda hiki kilichogharimu Shillingi Millioni 400, na ambacho tayari kimeshaanza uzalishaji kinategemewa kufunguliwa wakati wowote siku za karibuni na kuiwa mkombozi wa wakulima wa zao hilo jimboni humo ambao wamekuwa wakiuza tangawizi ghafi kwa kukosekana huduma hiyo adhimu
Mheshimiwa Mbunge wa Same Mashariki, Mama Anne Kilango akikagua sehemu ya uzalishaji wa unga wa tangawizi kiwandani hapo

Mheshimiwa Mbunge wa Same Mashariki, Mama Anne Kilango, akiwa na baadhi ya wafanyakazi na viongozi wa kiwanda hicho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Hongera kwa mama Kilango, huu ndio uwajibikaji tunaoutaka

    ReplyDelete
  2. Haya ndiyo maneno. Mkulima atapata soko na vijana watapata ajira.
    Hongera kwa mama Kilango na jimbo lake lote!

    ReplyDelete
  3. Wapare wameshamchoka huyu. Uchaguzi ujao akagombee Mtera kwa mumewe.

    ReplyDelete
  4. Seeing is believing nadhani wiki chache zilizopita walisema kuwa hakuna kiwanda sasa ameamua kwenda na kuweka ushahidi kuwa kiwanda kipo. Ila ni kweli wapare wa huko wamemchoka tayari

    ReplyDelete
  5. Anon wa Wed Aug 22, 07:19:00 AM 2012 acha chuki binafsi. Ongelea nafsi yako na sio kwa Wapare wote.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...