HABARI YAKO NDUGU NAOMBA UNIWEKEE TANGAZO ILI  KATIKA  BLOG  YAKO.
KUNA KIJANA  WA  KISOMALI  ANAUTAFUTA UKOO WAKE  NIKIMAANISHA NDUGU ZAKE   POPOTE  PALE WALIPO
KIJANA HUYO ANA UMRI WA MIAKA  KATI YA 27 AU 28 NA  BABU  YAKE ANAITWA ABDILLAH   ALLY   ALIKUWA ANAMILIKI  HOTEL YA  MBARAKA HOTEL  HUKO MOMBO NCHINI TANZANIA  MIAKA  YA  NYUMA  (MWAKA 1984) NA BABA YAKE MZAZI ANAITWA  HUSSENI ALLY    AMBAYE NI MTOTO WA  MMILIKI WA  HIYO  HOTEL (MZEE ABDILLAH ALLY).KWA  YOYOTE ANAEUFAHAMU  UKOO  WA MZEE  ABDILLAH  ALLY  ANAOMBWA  KUMSAIDIA  KIJANA  HUYU AWEZE KUWAPATA   NDUGU  ZAKE.KWA  MAWASILIANO .

Mobilenumber

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Ahh hili tangazo lilipendeza sana lingetoka mapema maana jana kulikuwa na mkutano wa siasa pale kulikuwa na wasomali kibao. Ilifaa baada ya kutoa kadi wanatangaza na ndugu anayetafuta ukoo wake siajabu walikuwepo mle nduguze. Anyway watapita tu hapa kusoma

    ReplyDelete
  2. Huyu nae, mbona kajificha ficha chini ya mti badala ya kuleta picha kama ya passport?

    ReplyDelete
  3. Kwani yukwapi huyo ndugu, ni rahisi kama yuko mkoa wowote na anajua kiswahili aende hoteli yoyote ya wasomali akiuliza na kuacha namba yake atapata ndugu zake. Natumaini utapata ndugu zako. Shukran ndugu yangu,

    ReplyDelete
  4. Sasa kama unajua ana Hotel Mombo kwanini usiende huko? Itakuwa bado wapo hapo hapo au watu wanawajua.

    ReplyDelete
  5. UBALOZI WA MUDA WA NDUGU WASOMALI:

    Kama wewe ni Mtanzania na mwenye asili ya Kisomali cha kufanya ni kupeleka taarifa hizi maeneo haya ambayo yanakuwa kama Ubalozi wa muda wa Wasomali:

    Eneo la Kariakoo Dar Es Salaam,

    (1.)AL-URUBA HOTEL, DAR ES SALAAM
    (2.)MASJID QIBLATAIN,DAR ES SALAAM
    (3.)MTAA WA LIVINGSTONE,DAR ES SALAAM

    ReplyDelete
  6. Hofu yangu isije kuwa amejiunga na Al-Shabaab

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...