Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari, leo katika ukumbi wa Sekretarieti, kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam.(Picha na Bashir Nkoromo).

NA MWANDISHI WETU

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye amewataka Chadema kwenda mahakamani haraka badala ya kusubiri kuombwa radhi kama walivyotaka ili kusafishwa dhidi ya madai ya chama chao kupewa mabilioni ya fedha na mataifa tajiri.

Aidha amemtaka Katibu Mkuu wa chama hicho Dk. Wilbrod Slaa kuiomba radhi CCM la sivyo itamburuza mahakamani kudai fidia ya sh. bilioni 3 na shilingi moja, kwa kuituhumu uongo kwamba imeingiza silaha kutoka nje ya nchi tena bila kulipia ushuru.

Nape alisema hayo leo Agosti 27, 2012, kweneye mkutano wake na waandishi wa habari, uliofanyika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba mjini Dar es Salaam.

"Bila shaka mmesikia jana Chadema wakinitaka niombe radhi au wananipeleka mahakamani kudai fidia ya sh. bilioni 3, kwa madai eti nimesema Chama hicho kinapata mabilioni ya fedha kutoka kwa mataifa tajiri. Mkubwa hatishiwi nyau, nawataka waende haraka mahakamani wala wasisubiri hizo siku saba", alisema Nape.

Alisema, CCM inao ushahidi wa kutosha kuhusu madai aliyotoa Nape dhidi ya Chadema na kwamba huyo tayari kutoa uthibitisho huo mahakamani badala ya kuomba radhi.

"Nadhani wakienda mahakani itapendeza zaidi maana huko ndiko pazuri kutoa uthibitisho kuhusu tuliyosema, na ninawahakikishieni tukishathibitisha na Msajili wa Vyama akaupata uthibitisho huo chama chao kinafutwa", alisema.

Kuhusu CCM kumburuza Dk. Slaa mahakamani, Nape alisema, ameshawaagiza wanasheria wa Chama, kuandaa barua ya kusudio la mashitaka hayo, na Dk. Slaa atapelekewa ili aamue kama ataomba radhi au atakuwa tayari kwenda mahakamani.

"Wakati wanakwenda mahakamani, Chadema wamwambie babu yao ajiandae kuomba radhi au kuburuzwa mahakamani kuilipa CCM fidia ya sh. bilioni 3 na shilingi moja kwa kuizushia CCM uongo kwamba inaingiza silaha nchini tena", alisema Nape.d

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Che GUevaraAugust 27, 2012

    Nape, adui yenu mkuu sio CHADEMA bali ni watu ndani ya CCM ndiop wametufanya hata HARUFU ya CCM hatutaki kusikia tena!

    MAJIZI yote yapo ndani ya CCM wachache wanaiba na kugawana mali zetu na wala CCM haichukui hatua kwani inaonyesha ndio DIRA yenu ya WIZI!

    Bora tujaribu CHADEMA huenda neema itakuja na tumepania kuwapiga chini CCM uchaguzi ujao.

    ReplyDelete
  2. Mi nashauri Bw. Nape uwahi mahakamani tuu!! si mliona mlivyoumbuliwa na Lisu about majaji? na ushahidi wa Lema kuhusu Pinda na Arusha mbona mkauzika?? Nenda tuu baba uone yatakayokusibu

    ReplyDelete
  3. Hahhaha haahaha siasa bwana ingia ufe...

    ReplyDelete
  4. MkomunistiAugust 28, 2012

    hahahaaaaaaaaaaaaaaaaa! CCM Kwishineyyyyyy!

    Lakini mliyataka kwa kutufanya mambumbu miaka yote hadi Mungu alipoamua kututukia "MASIHA' ambae ni CHADEMA

    ReplyDelete
  5. mbona tuhuma za container la silaha kimya. Chadema inaotesha mti juu ya mbuyu na mvua haikunyesha hivyo haitaota.

    ReplyDelete
  6. Is Nape a good force or a bad force for CCM?

    ReplyDelete
  7. HAHAHA WACHA NICHEKE MIMI MAANA JINSI TULIVYOCHOKA NA NYIE CCM MUNGU NDIO ANAEJUWA

    YANI TUTAJITAHIDI KWA UWEZO WOTE NA KWA MAOMBI KUPITIA KWA MUNGU TUHAKIKISHE TUNAWATOA CCM MADARAKANI

    KAMA MDAU ALIETANGULIA HAPO JUU WACHA TUJARIBU KWA CHADEMA MAANA CCM HATUJAFANIKIWA KWA ZAIDI YA MIAKA 50

    CHAMA CHA CCM NI MAFANIKIO YA WATU FULANI NA SIO KWA MAFANIKIO YA TAIFA ZIMA

    WEWE NAPE WACHA KUJITAFUTIA MATATIZO NI BORA KUANZA KUOMBA URAFIKI NA HAO CHADEMA MAANA IFIKAPO 2015 TUNACHUKUA NCHI NA TUTAWAFIKISHA MAHAKAMANI MPAKA MAKADA WENU WA CCM

    NDUGU WOTE MLIOPO UGHAIBUNI WAKATI NDIO HUU WA KUIPA CHADEMA MADARAKA ILI TUWEZE KURUDI NYUMBANI

    WENGI WETU TUMEKIMBIA NCHI NA KUHAMIA UGHAIBUNI KUTOKANA NA UGUMU WA MAISHA YA NCHI YETU ULIOTOKANA NA UONGOZI MBAYA WA CCM.

    ReplyDelete
  8. Nape is a 'hovyo hovyo' force for CCM and the country!!

    ReplyDelete
  9. nape nnauye huu ni ushauri wangu wa bure, hapa unashindana na nguvu ya umma wa watanzania na si chadema peke yake na ndiyo maanakila ukiongea wa wanakuona kama nahodha wa meli iliyotoboka ukiwashauri abiria kwamba haitazama. watu wamechoka na siasa zenu za maneno. hivi unaona jinsi watu walivyo maskini huko vijijini,hivi umeona hali ya wodi za mama zetu wanapojifungulia?ndio maana kila mtu hakusikilizi unachokisema maana mwenzetu sijui unaishi tanzania ipi

    ReplyDelete
  10. Michu, huyo mtoa mada hapo juu alitaka kusema ( KUTUTUMIA MASIYA) naomba labda computer zako ziwe na spell check, ili hawa waliokimbia umande, nao tuweze kuwaelewa. Zebedayo msema kweli

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...