Ankal,
 
kumekuwa na mjadala mrefu kuhusu kodi za TRA kwa biashara na kuagiza magari.Wadau wengi wamelalamika hapa wakisema TRA wezi..hii ni hatari kwani kama mtu mmoja amekula rushwa toka kwako, hilo lisiwe ni kigezo cha kusema wote TRA ndivyo wanafanya kazi.
 
Sasa TRA ina mtandao wake ww.tra.go.tz ambapo wameweka bayana gaharam za kulipa kodi, ama biashara au gari, ukubwa wa injini, umri nk na kukwambia fanya hesabu. Na wametoa kielelezo hili kutoa mwanga, kama hiyo haitoshi wameweka calculator ya ktumia Excel.
 
Zaidi ya hapo wameweka simu za kuwasiliana naoa ambazo mtu unaweza kupiga bure kama ifuatavyo:
 
0800-110-016 for TTCL and Vodacome Subscribers
0786-800-000 Airtel Subscribers
 
No Swahili pages on the website though ( 'cause English ndiyo lugha ya serikali, sasa wale waosha vinywa kila mtu akiandika kwa Kiingereza basi wanakuwa wepesi kusema andika kiswa hili).

La kuongezea, huku zamanai Ankal uliweza kuleta mjadala huu toka kwa mdau na mwanasheria mmoja alisema unaweza kulalamika kama umepewa kodi kinyume na sheria, na hizo sheria zipo wazi katika mtandao wa TRA, sasa tuache kupakana matope..
 
wapo watumishi wanao kula rushwa, na labda walio wengi lakini wapo wasio kula rushwa na la zaidi, sera ya TRA na serikali ni kuwa haki itendeke na kam sio, kuna simu hizpo za bure, kuna mahakama, kuna wanasheria kuna blog zitumie.
 
 
Sasa kama ambavyo tumesikia, hawa jamaa walio wengi wanafnay kazi nzuri ya kusaka na kukusanya kodi vizuri kiasi cha kusifiwa kimatafia..sasa suala la pesa hiyo inaishiwa wapi, siwezi kujibu wakati utnaona treni ina mabehewa yameoza  wakati wabunge wananunua magari mapya. Sasa kama wananchi kelele zetu tuzielekeze kwa hawa wabungue, wakienda wakalala, kura hatuwapi na hapo mwisho.
 
Zaidi tujue kwa sasa kuna hili la kutoa maoni ya katiba mpya, hivi vitu vyote vinaweza kuwekwa mfano, kusema sherio zote ziwe katika kimakonde kuliko Kiingereza kwa sababu huyo wa kwanza mzalendo, wapili mkoloni, au mwenza katika uchumi..uchaguzi ni wa mtanzania.
 
Kuhusu kazi nzuri ya hawa jamaa na serikli kwa ujumla angalia hapa:
 
Basi tuache kelele bila utafiti.
 
Mdau Bakorea

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 25 mpaka sasa

  1. Mwanzi nilipoanza soma hii taharifa nikajua ni public release ya TRA. Nilipoendelea kusoma nikaona haiweaekani TRA waanze kuongelea tuwawajibishe wabunge wtu...hawataki kazi eeh.

    Sasa mtoa mada wewe ni agent wa TRA?

    Kama siyo kwa nini TRA hawachukui muda kutuelimisha kama ulivyofanya wewe kama wana nia ya dhati ya kusafisha jina lao na kuacha kuwalinda vibaka wanaojiita wafanyakazi wa TRA na kuchafua TRA?

    Kwetu sisi hayo ma ranking ya dunia ya kwanza hayatuhusu...tunaongelea TRA tokana na experience yetu na maumivu...kama imekuwa ya kwanza sijuhi ya mwisho kimataifa who cares???

    ReplyDelete
  2. hamna lolote web site link yenyewe imekosewa.

    mie gari langu waliliweka storage muda mrefu makusudi ili nilipie storage

    ReplyDelete
  3. Bakorea asante umeleta hoja nzuri,ingawa ulikuw na harakaka ya type.Kwa ujumla TRA wanafanya kazi nzuri sana hata kama bahadhi wachache wanaokula rushwa,lakini kwakweli wanafanya kazi na kidogo wamefanya mambo yamekuwa rahisi kwenye kulipa kodi..Na siku hizi wamekuwa wakarimu kweli kwa wateja,yaani wamekuwa kama customer care services.Keep up TRA.Tunataka kuelewa zinakokwenda hizo fedha hadi tunashindwa kukarabati hayo mabehewa tunashindwa kununua ndege hata 2 mpya(mpya ndiyo) za ATCL.Watumishi wa UMMA kupata mishahara midogo,n.k

    David V

    ReplyDelete
  4. Sasa mbona hii site haifunguki?

    ReplyDelete
  5. Nashukuru sana mdau Bakorea kwa kutupatia website ya TRA ambako kuna data kamili kuhusu ushuru na gharama mbalimbali za kulipa ili kulitoa gari bandari ya dar es Salaam Tanzania hasa kwa magari ya kutoka nje ya nchi.
    Nimepata maelezo ambayo nimekuwa nikiyatafuta kwa muda mrefu.

    ReplyDelete
  6. Wafanyakazi wengi wa TRA ni wala RUSHWA hilo lipo wazi na watu wote wanalifahamu hilo,Na akaunti zao wanazoweka pesa huwa wanafungua kwa majina aidha ya ndugu zao au watoto wao ili wasiweze kujulikana wana pesa nyingi,maana akaunti zao huwa zinakaguliwa,Jingine linanishangaza sana kama mtu ukitumiwa nguo na ndugu yako kutoka nje eti ni lazima uzilipie kodi!Sasa mbona sisi tukiwatumia ndugu zetu vitu kutoka Tz kwenda ulaya,hao ndugu zetu hawalipishwi kodi?Sasa inakuwaje mtu ulipie kodi kwa nguo za kuvaa mwenyewe?Inashangaza sana!Ndiyo maana tunasema wafanyakazi wa TRA ni wezi!

    ReplyDelete
  7. Hao Jamaa wanakula rushwa wala hakuna la kuwatetea. Watu wataendelea kuilalamikia TRA kama shirika linaloshughulikia mambo ya kodi. Mtu unaenda kulipa kodi kwa TRA sio mtu fulani.
    Kama ninavyo fahamu Kiswahili ndio lugha ya Taifa na mawasiliano kwa Watanzania. Kiingereza sio lugha rasmi kwa Tanzania. Kiingereza kinatumika mahakamani zaidi kutafsiri na kuandika sheria.
    Watanzania wengi wanawasiliana kwa kutumia kiswahili, kwa hiyo jambo lolote serikali inahitaji kuwasiliana na wananchi ni bora kutumia kiswahili. Kasumba chafu sana kwa watu wachache wanaofahamu kiingereza kuwaburuza mamilioni ya watanzania kwa kigezo ambacho hakina msingi. Watanzania wangapi wanatumia kiingereza katika mawasiliano yao ya kila siku? Ni lini tutathamini kilicho chetu watanzania? Shida tupu kila kukicha.

    ReplyDelete
  8. Mdau uliyeleta mada nakukubalia kwa jambo moja kwamba wala rushwa TRA wapo lakini sio wote. Pengine wewe ni mmoja wa wachache wasiokula rushwa ndo mana imekuuma hao wadau walivyo-generalise.

    Lakini sikubaliani na wewe unaposema kiingereza ni lugha ya serikali - sio kweli kabisa hapa umepotosha. Mimi nafanya kazi ofisi ya Serikali na hiyo hiyo serikali huwa haipendi kuona tunahutubia kwa kiingerza pale wanapokuwepo.

    ReplyDelete
  9. Mimi iranichukuwa Muda sana kuniconvince ubora wa TRA baada ya kutaka kurudiswa kwa kutohudumiwa pale Mwenge dirishani kuna jengo la kisasa nilikuwa naingiza pesa zaidi ya laki moja ila fisadi mwenye uchu wa sh 5000 tu aliamua kukwamisha kazi mpaka hapo alipopewa mlungula.Ofisi yenyewe wanashughulikia Tin niliumia sana.Je mapato mangapi yanakoseshwa kwa uchu wa vi hela vichache? Baadhi ya maeneo yana maagent kabisa wa kurahisisha kazi huku PCB wakikoroma usingizi mzito

    ReplyDelete
  10. Lakini jamani mimi sijaleta gari bongo lakini watu wote wanalalamikia hiyo tiahera opss sorry tra. mleta mada hii mimi naona katumwa.mbona anaingiza na kutoa ohhhh mara wengine wanachukua wengine hawachukui. ufupi sisi hatutaki rushwa na malipo mara nne nne. kwa hiyo ndugu samaki mmoja akioza?. Pia documents zikitimia usisumbuliwe sababu usumbufu ni footstep ya rushwa. By salum

    ReplyDelete
  11. Haya zebedayo teteta rushwa sasa tunasubiri.by salum""""" sio salumu" zebe weeee

    ReplyDelete
  12. Watumish wengi wa TRA ni wala rushwa wasitetewe. Hakuna kinachosemwa kama hakipo. Mnarudisha uchumi nyuma kwa kutanguliza vijirushwa vyenu.

    ReplyDelete
  13. Wewe ndau afadhali umeleta mada ya ushuru na TRA. Shida yangu ni huu ushuru wa fire extinguisher za magari. huu ni wizi wa mchana. Gari ina bima ikiungua unalipwa nyingine. Ushuru wa fire extinguisher ni wa nini? Pia kwa nini mumkatie mtu stika ya fire extinguisher kwa kulipia pesa, wakati huohuo ananunua fire extinguisher, sasa hiyo stika ni ya nini? Stika inazima moto? Huu ni wizi mkubwa serikali yetu inatufanyia ndo mana kila kukicha tunaichukia kwa vile inatuongezea umaskini badala ya kutupunguzia. Wahindi wanakwepa ushuru mnawaachia mnakuja kulipizia kwa wanyonge.

    ReplyDelete
  14. Che GUevaraAugust 04, 2012

    Orodhesha wafanyakazi 10 wa TRA then wafuatilie maisha yao utazimia kwa utajiri utakaowakuta nao! Ni MCHWA hawafai!
    Iundwe tume ya kuwachunguza kama haijakuta asilimia zaidi ya 80 ni MCHWA wa kutisha

    ReplyDelete
  15. Tatizo kubwa hapa sio ubingwa wao wa kukusanya kodi nyingi bali namna ya walivyo makatili kwa wenye nchi na wakarimu sana kwa wageni wezi! mtanzania akifungua kaduka leo, kesho asubuhi wapo mlangoni wanataka kodi, penati kwamba alikwepa kodi na rushwa eti ya kumpunguzia penati, wageni wezi wakifungua mitega (sio vitega) uchumi yao wanapewa msamaha wa kodi wa miaka mitano au zaidi!!
    sasa hao wanaowasifu kwamba ni wakusanyaji wazuri wa kodi ni akina nani? si haohao wanaopewa msamaha wa kodi? hata mimi nikipewa msamaha wa kodi na wakawabana hao wanaowasifia nitawasifia kuwa ni wafanyakazi wazuri! wanamshauri waziri aongeze kodi tena kwenye pickup mabasi na malori vitu ambavyo ni muhimu kwa kila mtanzania wanaacha mashangingi ambayo ni muhimu kwa matajiri tu, wanamtoza mtu ushuru wa station wagon kwenye pickup, baada ya kuelezwa ukweli, wote wanagoma kurekebisha, lakini kama ingekuwa the otherway wangerekebisha haraka sana they are 89.79% unfare and killers of Tanzanians and tanzanians prosperity!! na ni wajinga kwani wanashindwa kujua kuwa wanaemdhuru ni mtanzania mwenzao! ahh hii mimbumbumbu inaniudhi mimi!! unakusanya pesa kutoka kwa wanao nyumbani halafu unatamba umeongeza kipato, badala ya kukusanya kutoka kwa majirani ulete nyumbani ndio utambe!!

    ReplyDelete
  16. sasa nyinyi mbona wote mnanena tuuu mm nauliza jambo moja tu..kwani TRA ipo chini ya wizara gani?...kama ipo chini ya wizara ya MWAKIEMBE...basi mambo yote yatakaa sawiya vuteni subra muda si mrefu atawashukia kama mbogo..kwa hiyo nyinyi wadau huu sio muda wa kupoteza wakati...kuanzia sasa wadau wote tukiona kitengo flani hakiendi sawa tumshikie bango WAZIRI MUHUSIKA wadau tuamke..hao wafanyakazi wa TRA ni watu wa kawaida kabisa..AMKA AMKA WADAU tunataka kuona AIR TZ INAKUA NDEGE ZAKE TENA ZA KUNUNUA SIO ZA KUKODI MAMBO YA KUKODI yamepitwa na wakati..RELI PIA TUNAHIJAJI NJIA NYINGI ZIJENGWE MKOA TU MKOA..mabehewa mapya yanunuliwe ya abilia na ya mizigo pia..lamwisho na la msingi TUWAPE SAPOTI MAWAZILI WOTE WENYE UPEO WA MAENDELEO YA TAIFA LAO.ni mm mdau wenu, TAJILI WA MAWAZO...NIPO UK...na zebedayo nakukubali ila huna utajili wa mawazo..hapo nimekupiga 3 bila. SIKU NJEMA WADAU.

    ReplyDelete
  17. Wadau wote,
    1. Mtoa mada ni mbeba boksi mzalendo amba ametumia huduma za TRA miaka takriban miwili. Magari mawilinyalipita kwa kutumia ajent ambaye tuliangalia gharama za kukomboa kupita www.gariyangu.com na ikawa hivyo yalipofika, mojanlikiwa na uchakavu na lingine bila.

    2. Kuhusu website nimekosea, www.tra.go.tz, herufi ya 'w'' ilipungua..unajua tena majuu kusave wakati wote hakuna matanuzi!

    3. Mdau mmojabhakuelewa kuhusu sifa ya TRA kukusanya kodi. Wanaotupa misaada wanapata pesa kwa kuhakikisha kodi inakusanywa. Kabla ya awamu ya mh. Mkapa tulikuwa tunazembea ama tunasamehe matajiri, kumbuka enzi ya Mzee ruksa. Nchi za Nordic zilisitisha misaada baada ya kasheshe ya kusamehe kodi. Mh Mkapa alilivalia njuga na since then TRA imekuwa inaongeza mapato kwa serikali kitu ambacho kinaonyesha rushwa inapungua.

    4. Mdau mtumishi wa serikali hakuelewa kuhusu kukandia matumizi ya kiingereza kuwa ndio lugha ya serikali. Nilimaanisha gazet la Daily News ni la serikali, kimombo. Website ya TRA ni kimombo na sheria tena ambazo zingehitaji kutafsiriwa kwa lugha za makabila kama biblia zilivyo, ziko katika kiingereza. Sasa mlala hoi wa namtumbo na kongowe atajua amevinja sheria gani?

    5. Nawakumbusha mada aliyoleta mdau Mashaka kuhusu wana diaspora kupiga kura, alitaja walipa kofi, wachache.
    Kwa hiyo nchi nyingi zenye rushwa hawakusanyi kodi na wanaishia kuomba omba .
    6. Kuna mdau alileta mada ya wadau wa nje warudi Bongo kwa sababu Bongo mambo kama Ulaya, sasa ranking hiyo inakuonyesha jinsi bado tuko maskini, na Rwanda wanatupita. Kwa hiyo kurudi iwe ni uzalendo sio kwamba nitapata kazibau utajiri uliokwama huku..nadhani mlimsikia Masha kwenye kipindi cha mkasi, yeye ana hela yake, mshahara wa ubunge alisaidia watoto wa jimboni kwake wasome, kwa hiyo alirudi Bongo kwa uzalendo sio utajiri au kusema Marekani limshinda.

    Na tusimsahau Ankal amba tangu miaka ya 80 anaenda Ulaya na angeweza kulowea lakininyumo yumo, kwa kuwa anaona mambo kwake mazuri, na hii ni tathmini yake sio ya jurani au mshikaji katika dhitika lingine.
    TRA kama sehemu ya jamii ya wala rushwa na watoa rushwa itakuwa na samaki waliooza, sio wote..wakondeepfreezer!

    Bakorea omuburi

    ReplyDelete
  18. ha ha haa zebedayo kwenye ishu nyeti kama hizi humuoni, na hata akija hoja zake zimekaa kukejeli na matani matani ila akikua ataacha!

    ReplyDelete
  19. TRA ni WEZI. hainahaja yakutafuta kama mtu anakula rushwa au la. aweamefungua account kwa jina la mama yake au mtoto wake. Anagali tu maisha anayoishi, gari analoendesha, shule wanazosoma watoto zake, linganisha na mshahara wake and walahhhh jibu unalo. na kwa sasa katika serikali hii hakuna mtu anaweza kufanya hilo. Alieweza alikuwa ni Nyerer na Sokoine peke yao kwani maisha yao yalilingana na vipato vyao.
    Turudi kwa TRA----mimi nimeagiza magari kuleta TZ mara kadhaa--kwanza kabisa, malipo yao yapo peged kwenye Dollar(USD), pili ushuru unalipia kutokana na CIF---wao wanapandisha hii CIF. Na hii yule unaeongea nae ndio anauwezo wa kupandisha au kushusha bei ulionunulia regardless receipt yako inasema vipi. Mfano mwingine--nilijaribu kufanya biashara ya kuingiza cement kutoka Pakistan (DG cement). Kufika huku hawa jamaa wakapandisha bei ya cement/ton..tukenda mbaka kwenye website ta DG cement--imeelezwa vizuri kabisa lakini bado wakanipandishia bei na hatiamae nikalipa ushuru umkubwa na faidia yangu kupungua sana. TRA wote ni wezi, wote.....tunakaa nao mtaani, tumesoma nao--tunawajua, ni wezi

    ReplyDelete
  20. Nyie kaeni huko msubiri kulalamika bila uhakika wowote wakati wenye nia na uwezo wa kuingiza magari wanaingiza na kuuza.

    Watu wasiojua kitu na watui wasio na kitu kazi zao kulalamika na kujifanya wanajua kumbe hata utafiti wala ukweli wowote hawana.

    Wachagua majembe wengi tu lakini wakulima wa kweli wachache.Wanalalama kwa kuwa hawajui taratibu kwa kuwa siku zote walizoea kuingiziwa vitu nchini na wazazi wao.

    ReplyDelete
  21. michuzi umebania comment yangu. simply ina facts, halafu hii utaitoa kwasababu ya U-TRA wako!

    ReplyDelete
  22. Yaani huku mitaani ukiona mansion utasikia "si anafanya TRA" yani imefikia kipindi jamii imeamua kukubali kuwa kufanya kazi TRA =Kuwa milionea.

    Wakati ni jasho letu hilo.

    Hata ukienda salon za kike ukiona dada amechafuka kwa gold utasikia "mumewe yuko TRA'" maanake usishangae; TRA=Money
    Fedha za ushuru zinaishia mifukoni mwa watu despite the fact that ni moja ya ofisi inayolipa wafanyakazi wake handsomely ili wawe waadilifu.

    Ndo maana Mkapa alitimua kazi wote mwaka fulani

    Tena nilikuja kuambiwa kuwa hii mijamaa inaiba ikishilikiana na ma agent...utasikia agent anakwambia leta ela bila kitu kidogo gari itaozea Bandarini...Kumbe wote ni mtandao mmoja.

    Ila sishangai kwani watoza ushuru ni wadhambi toka enzi za Yesu

    ReplyDelete
  23. Wewe mdau unayesema ela wanatumia majina mengine kuweka bank hauko sahihi. Hawa jamaa ela wanaweka kwenye mitungi...na kwa kuwa zinakuwa nyingi na wanaona wakitumia kwa vutu vya wazi watagunduliwa...wanaongoza kwa kugawa kwa nyumba zao ndogo; ndugu jamaa na marafiki. Kwa ufupi ni vimwaga ndio maana wakitimuliwa kazi wanaumbuka in less than a year

    ReplyDelete
  24. Bakorea hao unaosema wanatupa misaada ni akina? una maana hayo mataifa ya ulaya? hawatupi misaada, wanatoa pesa hizo kwasababu;
    1. Wanajaribu kuturudishia angalau kidogo ya kile walichotuibia kwa mikataba feki na misamaha ya kodi iliyopitiliza waliopewa
    2. Wana ndugu zao wanaoishi na kufanya kazi katika maeneo hayo wanayotuibia huku kwetu, kama wasipotoa hizo pesa sisi na hao ndugu zao watateseka, kwahiyo hawatoi pesa kwasababu wanatupenda bali kwasababu wanalazimika!! kwa manufaa yao, sisi tunafaidika nazo kidogo kwasababu tu amejichanganya nasi ili kutupumbaza tuwaone kama ndugu zetu.

    ReplyDelete
  25. Kama alivyosema mdau mwenzangu kama atuwekee wafanyakazi 10 tu halafu iwekwe kamati ya uchunguzi kama hamjaaibika!kwakweli kibaya ndugu zangu wa TRA mnawaumiza Watanzania wenzenu inauma sana!ilikuwa musaidie watanzania kujikwamua sio kuwakandamiza!fikiria jamani muuza maandazi wewe unamkandamiza?na kibaya kingine mtu anakuletea risiti na kukwambia wasiliana na kule nilikonunulia hiki kitu lakini bado unampangia wewe unavyotaka!kwakweli nimbaya kaeni mfikirie sana hiki kitu!fikiria watu walivyochoka na nyinyi wewe ulieandika hapa hukupata hata wakuwa pamoja na wewe wote wamechoka na TRA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...