Mrembo Lisa Jensen ambaye ni Redd's Miss World Tanzania 2012 amerejea jijini Dar es Salaam leo akitokea nchini China alipokwenda kuiwakilisha nchi katika mashindano ya Dunia mwaka huu na kupokelewa na viongozi kadhaa wa Kamati ya Miss Tanzania akiwepo Mkurugenzi wa Kino International Agency waandaaji wa Miss Tanzania Hashim Lundenga (kulia) aliyefika uwanja wa ndege wa JNIA Dar es salaam kumpokea.
Redd's Miss World Tanzania 2012,Lisa Jensen akizungumza na viongozi wa Kamati ya Miss Tanzania, kutoka kushoto, Katibu Mkuu, Bosco Majaliwa, Mrembo Amisa Hassan, Mkurugenzi Hashim Lundenga na Ofisa Habari wa Kamati, Haidan Rico
Redd's Miss World Tanzania 2012,Lisa Jensen akila pozi ya picha na mmoja wa warembo waliofika kumpokea Amisa Hassan. Lisa alifanikiwa kuingia Robo fainali za Top Model na kumi na kumi bora ya Shindano la Multmedia Award 2012.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Bure kabisa

    ReplyDelete
  2. Haya mama karibu nyumbani..ila kama nilivyo sema hapo awari usije kututia aibu kama wenzako eti mwanamke mzuri lazima awe na jizungu..hawa wana mawazo mgando tena bure kabisa kwenye jamii yetu...tena wamesoma kidogo hawa wanaojiona eti walimbwende kama wasingesoma sawa ningesema malimbukeni kumbe wala wengi wao wamefika mpaka mlimani universty..ila wanajidanganya kua eti ukiwa na jizungu umasikini baibai kumbe hamna lolote zaidi ya kucheza na mijibwa ndani ya nyumba..ni mm yuleyule tajiri wa mawazo endelevu..sikusoma ila nikio cha jamii...amani kwa wadau wote.

    ReplyDelete
  3. yale yale ya miaka yote ya Lundenga!

    Huyu babu akubali tu kuwa hana ubunifu na umri kwake umekwenda aachie vijana waongoze taasisi hii na asiifanye kama ndio mradi wake wakati hauna tena TIJA kwa taifa.

    ReplyDelete
  4. kuna wamasai kibao kule ngorongoro black beauty wakienda tu hatukosi ushindi yani kama msudani kawa 10 bora top model unafikiri wameangalia nini wameangalia rangi kidogo na unatural,kwanini tusiwapeleke hao tuna ngangania kuwaweka weupe tuu kila sikuu.au aawaachie vijana wenye ujuzi.

    ReplyDelete
  5. kaambulia nafasi ya ngapi?

    ReplyDelete
  6. Ila akipewa Mkibosho basi aendelee mpaka kifo kitakapomfika. Kwani Lundenga ndio kamati nzima.

    ReplyDelete
  7. Lisa did well. Kamati ya Miss Tanzania haikuhamasisa wananchi kumpigia kura kupitia internet kama wenzetu wa China etc. Mie naona kamati inaanza kujisahau au waache kazi tu. GBR

    ReplyDelete
  8. imefika muda Mzee Lundenga akaachia ngazi. ni yale yale ya kila mwaka. awaachie uongozi kwa wengine.

    ReplyDelete


  9. Yaani tena hata msiongee kabisaa kwa sababu Lisa alitakiwa apate support toka nyumbani Tanzania lakini nashangaa hakuna ata mtu aliekua na muda kazi yetu kupiga kelele tuu ebu angalieni facbook fun page yake in only 600 likes sasa mnategemea angeshinda nini hata kwenye multmedia awards??

    South Sudan imeshiriki haya mashindano kwa mara ya kwanza na imefanikiwa kuingia top 10 sasa Tanzania je??

    ReplyDelete
  10. Mdau wa Tue Aug 21, 12:46:00 PM 2012 na Mkibosho, ni kwamba Lundenga ni mmilki wa kitu Miss Tanzania hata kama atakufa bado familia yake ndio itaendesha kampuni na mambo yote ya Miss Tanzania hivyo suala la kuachia ngazi hapa labda abinafsishe. (ILA HAPA IMEKAAJE SIJUI MTU BINFSI ANAMILKI HAKI YA MISS TANZANIA ALAFU ANATUMIA SHINDANO LINAKUWA LA KITAIFA ZAIDI, INA MAANA HUKU KWENYE MA-MISS HAIWEZI KUWA KAMA CHAMA FLANI HIVI KAMA TFF, KUOGELEA, NETBALL ETC ILI KUWE BAADA YA MUDA FLANI UONGOZI UNABADILIKA), Anyway mie Kilaza si mtaalam wa haya mambo ila nimeangalia kwa mtazamo huu)

    Mie mdau Igwamanoni wa Itabagumba

    ReplyDelete
  11. Lisa walimpeleka tu huku miss world hata kujielezea hajui!! Next year wachukue msomi kidogo. Haya mababa demu kaingia mjini

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...