Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akikabidhi sehemu ya tende kwa Masheikh wa Mji wa Monduli kwa ajili ya Ftar katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.kutoka kushoto ni Sheikh wa Mto wa Mbu,Sheikh Nasib Idd Nasib Mnyema,Katibu wa Bakwata wilaya ya Monduli,Idd Idoya,Ustadh Swalehe Ramadhan na sheikh wa wilaya ya Monduli Sheikh Mwinshehe Mwinyimgeni Salum Simba.Makabidhiano haya yamefanyika leo asubuhi nyumbani kwa Mh. Lowassa,Monduli.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa akipena mikono na Mashekh wa Wilaya ya Monduli baada ya makabidhiano ya katoni kadhaa za tende pamoja na jozi 100 za kanzu kwa ajili ya Waislam wa Monduli.Akipokea msaada huo, Sheikh wa wilaya ya Monduli Sheikh Mwinshehe Mwinyimgeni Salum Simba, alimshukuru mh Lowassa kwa utaratibu wake huo ambao amekuwa akiufanya kila mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan kwa Waislam wa Monduli.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Kweli huu mwezi wa kutoa.

    Ankal hii hata kidini inakubalika saaana tu. Kuna watu wanaweza kuona ametoa kwa ria(kutoa kwa kujionyesha).

    Kutoa huku ni kule kunakowataka na wengine waone na wafanye hvyo.

    mdau zenji

    ReplyDelete
  2. LOWASA WEWE NI MTU MWEMA UNADEAL NA MAMBO YA MUNGU TU,,,
    UBARIKIWE SANA!
    NDO INAVYOTAWIKIWA KUMTUMIKIA MUNGU WAKATI UNA NGUVU ZAKO,SIO WAKATI UMEZEEKA AU UNAUMWA,,ETI NDO UNAMKUMBUKA MUNGU.
    UISLAM UNASEMA SWALI KABLA HUJASWALIWA,TUMIA NGUVU ZA UJANANI KABLA YA UZEE,KUMBUKA WENZIO UKIWA NACHO SIO WAKATI UMEISHIWA UNADAI OOH NINGEKUWA NA KITU NINGEKUSAIDIA,, HA HA HA KWA MUNGU HIYO HAIPO,,WATU WENYE UWEZO UKIENDA KUMUOMBA MSAADA ANADAI ETI AMEPELEKA WATOTO SHULE MARA OOH NI MEISHA SAIDIA WENGI,,
    UKIONA MTU KAKWIJIA ANATAKA MSAADA KWAKO UJUE NDO HUYO HUYO MWENYE SHIDA,NA KATUMWA NA MOLA,LABDA AWE YULE YULE UNAEMJUWA KUWA NDO ZAKE KUOMBA OMBA HATA KAMA HANA SHIDA
    ,,LOWASA UBARIKIWE SANA

    AHLAM,,LONDON

    ReplyDelete
  3. safi sana lowasa.....mungu akupe kila la kheri na uzidi kutenda mema na mungu atakupa nguvu amin

    ReplyDelete
  4. napenda ka utamaduni ketu ka kushirikiana.God bless our country na mafisadi waige kuwaonea imani wenzao

    ReplyDelete
  5. Mpaka kieleweke Lowassa, you are our president ....

    ReplyDelete
  6. Ni vyema kutoa hasa ktk Kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu tukimrejea Mwenyezi Mungu!

    ReplyDelete
  7. Hatuitaji misaada ya Huyu mshenzi.tusiwe vibaraka vya tende na kanzu

    ReplyDelete
  8. nakuunga mkono mdaau wa mwisho poa ile mbaya

    ReplyDelete
  9. NAUNGA MKONO MDAU WA 07:59:00 PM.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...