MPAMBANO wa ndondi baina ya mabondia Maneno Oswald na Rashid Matumla ambao ulifanyika ukumbi wa maraha wa Dar Live Mbagala, jijini Dar es Salaam, katika kuadhimisha sikukuu ya Idd el Fitr, ulishuhudia Oswald akimchakaza Matumla kwa pointi.
Mbali na mpambano huo uliofanyika usiku wa kuamkia leo, kulikuwa pia na burudani za aina mbalimbali, likiwemo disko la watoto ambao pia walifurahia kuogelea katika bwawa maalum na michezo mingine mingi. Kwa upande wa muziki kulikuwa na shoo kali zilizofanywa na wanamuziki Juma Nature, Mwasiti Almasi, Estelinah Sanga ‘Linah’, Maunda Zorro na kundi zima la Jahazi Modern Taarab likiongozwa na mfalme, Mzee Yusuf.
(Picha: Musa Mateja na Richard Bukos/GPL)
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI.


Huyo Matumla na kitambi chote hicho jamani. Hizi ngumi jamani nzito acheni umri umeshaenda.
ReplyDeleteMatumla kwishiney! Achana na makonde sasa, jaribu kazi nyingine hata kubeba mizigo itakulipa
ReplyDeletemambo ya aibu kuingia ulingoni na shepu kama hii.Watu tugome kwenda kulipia ngumi za wanamasumbwi ambao wanaganga njaa ambao hawako makini na kazi zao. Huyu jamaa ameenda kupigania uzoefu tu
ReplyDeletematumla umezidi bora ulivyobondwa, pumzika sasa kila kitu kina mwisho eboh!
ReplyDelete